omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,325
- 2,498
Wanajf, nimekutana na hii habari na naona kwa kiasi kikubwa sana inafanana na kilichotokea hapa kwetu. Kwa wale wananofuatilia mustakabali wanchi tunaweza kuangalia hii hali. Msijali hii tafsiri isiyo rasmi.
Wabunge jana walizuia uundwaji wa wilaya mpya 25 zilizopendekezwa mpaka serikali ionyeshe uhalali wake na ni jinsi gani inajipanga kupata pesa za kuziendesha. Wabunge walio katika kamati za Utumishi wa umma na Serikali za mitaa jana walikutana na waziri wa Serikali za mitaa Adolf Mwesige na kuzuia uundwaji wa maeneo mapya ya utawala bila ya kuainisha ni jinsi gani serikali imejipanga kuziendesha (kipesa).
Wawakilishi hao wa wananchi pia wameitaka Serikali kutoa taarifa juu ya ni jinsi gani inaendeleza wilaya zilizopo. "Tunataka kujua ulingano na uhalali wa kuunda wilaya zaidi wakati hatujui ni jinsi gani pesa za kuziendesha zitapatikana" Mbunge wa IgaraMagharibi Raphael Magyezi (NRM) amesema. "Tunataka mchanganuo kamili wa mgawanyo ya fedha na uthibitisho kuwa hatutengenezi matatizo makubwa kwa nchi hii."
Wabunge wanaitaka serikali kwanza kuonyesha uhalali wa gharama za maeneo hayo mapya ya utawala na kama yanapelekea hasa kwenye ubora wa upelekaji huduma kwa jamii.
My take:
1. Hivi wakati hizi wilaya na mikoa mipya inaanzishwa hapa Tanzania ni nani walishauriana na kukubaliana kufanya
waliyoyafanya? Na bunge letu lina nafasi gani katika hili suala?
2. Je, kwa gharama za kuendesha hizi wilaya na mikoa wakati hospitali za mikoa hazina hata x-ray (sijataja shule na
mengineyo) ni sawa?
3. Je, kama kuna makosa ya kimaamuzi tumeyafanya, hatuwezi tukarudi nyuma kidogo badala ya kuendelea nayo? (maana
wahenga husema "tujifunze kutokana na makosa")
Nawasilisha
Source: http://www.monitor.co.ug/News/Natio...+costs/-/688334/1462620/-/xs3ojj/-/index.html