Bunge uchwara lataka EPA na Richmond ziwekwe kando

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,144
Posted Date::6/16/2008
NEC yazika mzimu wa Richmond
*Baadhi ya wabunge watetea watuhumiwa rasmi

*Wataka mijadala ya EPA, Richmond iwekwe kando

* Wengine wataka wachukuliwe hatuza zaidi

*Kikwete awaruhusu kuikosoa serikali kwa hoja

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

KUNDI la wabunge na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliopangwa kutetea Kampuni ya Richmond Development wamejitokeza rasmi jana kwenye kikao chao.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zilithibitisha kuwa kundi hilo liliwashambulia wabunge wanaotaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya watu waliohusika na Richmond na uchotaji fedha kutoka kwenye Akauti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwa mmoja wa wajumbe wa NEC, Mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Manyara alikuwa wa kwanza kuchangia hoja hiyo, akitaka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wa Richmond na EPA na kwamba, wananchi hawatawaelewa kama itaishia kwa waliotuhumiwa kujiuzulu.

Mbunge huyo alisema, wananchi wanahitaji hatua zaidi kwa wahusika badala ya kuishia kujiuzulu na kwamba, hali hiyo itakuwa ni kuimarisha CCM.

Mbunge kutoka Mkoa wa Singida (jina tunalo) aliongezea kuwa zinahitajika hatua za makusudi, kurejesha imani ya wananchi kwa chama chao kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zimedai kuwa, mwelekeo wa upepo kwa wabunge wanaotaka kuchukuliwa hatua, ulibadilishwa na kiongozi mmoja wa Jiji la Dar es Salaam ambaye alitaka wabunge wasilaumu, badala yake wakisaidie chama kujijenga.

"Niko Magogoni, nataka kuvuka kwenda Kigamboni, nahitaji kivuko imara kitakachonifikisha ng'ambo. Wabunge wa CCM hamsaidii chombo kuwa imara kama mtaendelea kushutumiana," alinukuliwa Kimbisa.

Msumari wa moto uliongezewa na Mbunge mmoja wa Kigoma (jina tunalo), aliyesema mwaka 2010, wananchi hawatahoji Richmond wala EPA zaidi ya kuhoji barabara na maji.

"Mwaka 2010, wananchi hawatatuuliza Richmond wala EPA, watatuuliza maji na barabara tulizowaahidi ziko wapi?" alisema Serukamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa mmoja aliwacharukia wabunge hao akidai kuwa wanalipwa vizuri, lakini wanashindwa kutetea chama, wakati viongozi wa chama wako taabani.

Mbunge wa jimbo moja mkoani alimsifu mmoja wa watuhumiwa wa Richmond kuwa, anakisaidia chama na kutoa mfano wa Uchaguzi mdogo wa Kiteto akisema walikuwa hatarini kushindwa kama si msaada wa mtu huyo.

"Kule Kiteto nilipofika nilimwangalia Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM), naye akaniangalia, ilikuwa wazi tushindwe, lakini tukasema inahitajika helikopta tukampigia simu mtu huyo (jina tunalo) helikopta ikafika kesho yake," alisema Komba.

Pia hoja hiyo ilichangiwa na Mbunge wa jimbo moja mkoani Tabora, ambaye aliunga mkono kuwatetea watuhumiwa hao wa Richmond.

Habari kutoka ndani ya kikoa hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi walikana kuhusika na Richmond, huku Lowassa akisema alijiuzulu ili kulinda maslahi ya chama.

Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema, kila mtu ana mawazo na hakuna anayeweza kuwasilisha aliyotumwa na kundi fulani na kwamba, yaliyowasilishwa yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.

Rais Kikwete aliwataka wabunge wawe na uhuru kuikosoa serikali bungeni, lakini kwa hoja na kwamba kusema hivyo haina maana kuwa ana lengo la kuwanyamazisha.
 
Back
Top Bottom