Bunge Syllogism na Mahakama. Mahakama Inaonewa au Bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge Syllogism na Mahakama. Mahakama Inaonewa au Bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Aloysius, Aug 1, 2011.

 1. Aloysius

  Aloysius Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati fulani tulifanya mjadala: Je ni haki Mahakama kuamua baadhi ya maswala ya kisiasa? Mfano lile la Ugombea binafsi. Sheria iko wazi kazi ya Bunge nikutunga sheria na kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria. Ndio maana Mahakama ikarudisha swala hilo Bungeni. Kwakuwa Ibara za Katiba zinaipatia Bunge kwa niaba ya wananchi nguvu yakutunga na kutungua katiba na sheria yoyote. Kwakuwa katika nadharia Bunge ndio chombo kinacho wakilisha wanchi kikamilifu. Maanake kama Mahakama ikizidisha nguvu zake nakuwa kana kwamba wametunga sheria wao, italeta picha kuwa hio ni sheria baina ya mahakama na serikali, huku ikiwa, Katiba ni makubaliano baina ya wananchi ( wanawakilishwa na bunge) na serikali, hivyo mabadiliko yoyote yanapaswa kufanywa kwa makubaliano ya asasi hizo mbili.
  Tatizo: Bunge limeweka mbele maslahi ya chama kuliko wananchi, hakuna UWIANO wa wawakilishi kwa muktadha wa kichama.
  Suluhisho: Hapo ndipo idea ya syllogism inaingilia kati; Kama wananchi hawaitaki katiba. Na kama wao ndio wanawaweka wabunge ambao ndio watunzi wa katiba. Basi wawaondoe nakuwaweka wabunge ambao watatenda matakwa yao.

  Syllogism inacho kisema hapa, sawa na msemo wa kiswahili usemao: Ukipenda boga penda na... Hivyo kama wananchi wataendelea kuiweka serikali ilioko madarakani katika madaraka basi hitimisho langu nikuwa wanapenda yote serikali inayotenda au Serikali yao inawatendea mengi mazuri kuliko mabaya. NASIO KUTAKA KULISHA MAHAKAMA KAA LA MOTO.
   
Loading...