Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 137
- 179
Salaam Wana JF,
Nianze kwa kusema kuwa wale wanaodhani Bunge letu ni Jumba la Sanaa wanakosea kimantiki na pengine hawajui Majukumu ya Mhimili huu na mipaka yake, Bunge lina utakatifu wake na upekee katika ustawi wa haki na Maendeleo kwa watu, Bunge Ni moyo wa nchi kiutawala.
Hatahivyo Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la wakosoaji hasa mitandaoni wanaohoji ubora na Uimara wa Bunge letu la Sasa, wapo wanaodhani Bunge limepoteza utamu na Radha kwa sababu ya uwepo wa wabunge wengi wa Chama kimoja, hoja hii ni dhaifu kwasababu wingi wa wabunge hao umetokana na Wananchi kupitia mfumo wa sanduku la Kura unaosimama katika mfumo wa vyama vingi.
Tunaweza kuhoji ubora wa Bunge endapo tu wawakilishi wa Wananchi wameshindwa kutimiza wajibu wao, Aidha tunaweza kuwa na mashaka na Bunge endapo tu Bunge lenyewe kupitia taratibu na kanuni zake kama muhimili unaojitegemea umeshindwa kuishauri ipasavyo serikali kutimiza wajibu wake katika mifumo ya utawala, uwajibikaji na uongozi bora.
Je, kama Bunge hili la Job Ndugai limeweza kuwa sehemu ya kutimiza wajibu wake kama Bunge la Wananchi nongwa inatoka wapi? Wapo wanaobeza weledi wa Spika Job Ndugai katika kusimamia chombo hiki, Ukweli ni kuwa Ndugai amefanikiwa na kuonyesha uwezo, weledi na nia ya kulitumikia Bunge kwa usawa, utashi na uzalendo kwa Watanzania wote.
Aidha sijaona tatizo la Bunge letu la sasa kwa ujumla wake, tusihukumu mhimili wa Bunge kwa sababu ya mawazo ya mbunge mmoja ambayo pengine yanamapungufu yake kimaudhui, Duniani kote Kila Bunge lina mifumo na taratibu zake kulingana na kanuni walizojiwekea na kamwe mifumo ya kiutawala haiwezi kuwa sawa Wala Demokrasia tunayoidai haiwezi kufanana kati ya taifa na taifa.
Ni vema tukosoe kwa kujenga hoja mbadala na si kubeza na kutusi, Aidha tutambue Bunge letu ni imara na linaendeshwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni zake na Wala si Jumba la Sanaa Kama wengi wanavyoamini.