Bunge si chombo sahihi kujadili na kuazimia kuhusu ripoti ya CAG,lipo biased

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ukitafakari kwa kina utaona hakuna umuhimu wa ripoti ya CAG kupelekwa Bungeni. Spika wa Bunge amekuwa mtu wa Kwanza kudharau kazi ya CAG ambayo wapo wataalamu wanalipwa kuifanya.

Aliikataa bila sababu za msingi ripoti ya Prof. Assad CAG mstaafu na leo ameonyesha wazi kutokubaliana na ripoti ya Sasa ya CAG.

Namna alivyozielekeza kamati za bunge zikachambue hii ripoti ni kama kaonyesha kabisa kwamba ana mtizamo hasi dhidi ya ripoti hii huku akidai Kuna watu wanapotosha.

Kwa aina hii ya viongozi ambao kwao kila Jambo analifanya Jambo binafsi badala ya Jambo la umma nivigumu kwa taarifa hizi kufanyiwa kazi.

CAG ameeleza kwenye taarifa zake kuwa moja ya changamoto anayokabiliana nayo ni mapendekezo ya taarifa za ukaguzi kutofanyiwa kazi na serikali.

Je, kwa mfumo huu Kuna umuhimu wakuwa na ofisi ya CAG? Kuna umuhimu wakutumia mabilioni kuwalipa watu ambao kazi zao hazifanyiwi kazi? Kwanini tunafanya ukaguzi?
 
Mbowe kabla hata ya kujisafisha na uongo wake wa kulewa na kuangushwa na konyagi kisha kulitangazia taifa kwamba amepigwa na wasiojulikana, amekuja na igizo jingine kwamba alifilisiwa na akaunti zake zote zilifungwa na TRA!!

Kama ni kweli alikuwa wapi kuyasema haya? Badala yake akawa anaitisha press conference akiwa amevaa gloves feki huku akiwa amejifungia kwenye lockdown hewa.

Ina maana Mbowe alikuwa tayari kuita waandishi wa habari na kuwaelezea alivyokimbia bunge na kwenda lockdown uchwara kuliko kuwaelezea alivyofungiwa akaunti zake zote ikiwemo ya mshahara?

Mbowe hili ni taifa la watu wanaojitambua na kamwe hutafanikiwa kwenye hiyo biashara yako mpya uliyokula 10% ili ulete chanjo ya corona nchini.
 
Mkuu unaongelea hili bunge lililotokana na uchafuzi mkuu wa 2020 na chama chakavu kuibuka na ushindi wa 99.9999%, au kuna bunge jingine.
 
Back
Top Bottom