Bunge nje ya bunge-oktoba -novemba, 2008 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge nje ya bunge-oktoba -novemba, 2008

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Oct 30, 2008.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Oct 30, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  AWALI ya yote katika Bunge nje ya Bunge kipindi hiki nitakuwa na safu ya kugusia:


  1. Yaliyostahili kuwa kwenye Bunge la Mkoa;
  2. Yanayostahili kuwa ndani ya Bunge la Kitaifa
  3. Yanayostahili kuwa Bunge la Washika Dau wote

  KAMA ingelikuwa kwenye Bunge langu hoja iliyopoteza muda na fedha za serikali kuhusu Jimbo la Mheshimiwa Laiser ingelirudishwa kwenye Bunge la Mkoa. Sababu kubwa: Wizara haina uchungu na jimbo moja tu! Na hawakuwa na muda wa kushughulikia kikamilfu.

  Hoja ya kuomba Umeme ilikuwa ni ya mkoa lakini ikaletwa kimakosa kwenye Bunge la Taifa. Yote hii ni kuonesha bado tuna safari ndefu ya kupangiana majukumu na kuelewa lipi linastahili kuzungumzwa wapi, wakati gani, nani na nini hasara au faida ya kulizungumza jambo mahala lisipostahili. Mahala amabapo halitakaa lishughulikiwe hadi muda wa mbunge bunge la taifa uishe!

  Masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii sisi tunayaweka kwenye kategori ya bunge la mkoa.

  Masuala yanayohusu ushirikiano kati ya mikoa au yanayogusa nchi nzima tunayaweka kwenye bunge la taifa.

  Yanayohusu wazee, watoto, walimu, wanamichezo na kadhalika tunayaweka kwenye bunge la uwakilishi maalum baada ya kuwaondoa wabunge wote wa kuteuliwa na kuwaweka huko pamoja na wawakilishi wa kila kikundi katika jamii kuanzia watoto, wanafunzi, walimu, mashehe, mapadri, wafanyakazi, wakulima, wavuvi, madaktari, manesi yaaani watu wote ambao wanafanya kundi moja leneye hoja na maslahi yanayosthaili kuzungumziwa tutakuwa nao.

  Utaona basi mabunge yetu yatakuwa yanafanya kazi kwa muda mfupi; hakuna anayesinzia bungeni; hoja zinakuwa fupi na zinazofanyiwa kazi papo hapo; na hakuna majibu ya kibabaishaji kutoka kwa yeyote yule saa zote, wakati wote!

  TAARIFA: BUNGE NJE YA BUNGE
  Kwa taarifa muhimu bunge LETU NJE YA BUNGE la taifa wakati huu lilikuwa na hoja hizi muhimu kuzungumzia:

  . peteroli na dizeli imeshuka bei nje lakini sio Tanzania kwanini?
  . tumefikia wapi kuhusu mrahaba wa migodi ya dhahabu?
  . tutajihami vipi na mtafaruku wa mikopo na masuala ya kifedha duniani? Ni ni tufanye tunufaike badala ya kuhasirika?
  . je, tutafaidika kwa kuwa karibu na nchi za Mashariki au Magharibi?
  . je, tuisaidiaje Kongo maana mashariki ya nchi imeanza kupata mafua ya Kongo
  . nafuu ya usafiri wa umma inakuja au la?
  . tunajiandaaje kumalaiza matatizo ya wanafunzi, walimu, madaktari na makundi mengine ya jamii yenye matatizo kama vile wazee wa EAC?
  . tuna mipango gani ya kiuchumi na kifedha kwa mwaka 2009 baada ya hali ya dunia kuchafuka ghafla?
   
Loading...