Bunge nje ya bunge 2008-2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge nje ya bunge 2008-2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by waziri kalala, Sep 2, 2008.

 1. w

  waziri kalala Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI MHUSIKA KALALA- AU ANAMNGOJEA RAIS AMWAMBIE?

  KWA KUWA hii ni wiki ya Nenda kwa Usalama Bunge nje ya Bunge limeamua kuanza kuuliza maswali ya msingi ambayo yanakusudiwa kwamba yakipatiwa majibu basi yanaweza kubadilisha maisha ya Mtanzania katika muda mfupi kiasi msomaji wako usichokiwazia. Kwa hiyo mada yetu ya leo ni kama hapo chini na maswali yetu ndio kama hayo na tunawangojea wabunge wa jamiiforums watachangia hili ili ndugu waziri aweze kupata chemchemi ya hekima yeye ashindwe kuyanywa maji yake tu.

  POLISI WA USALAMA BARABARANI: Hivi Waziri anamngojea Rais afanye haya

  1. Watoto na wazee wetu kulindwa wanapotembea njiani au kuvuka barabara?
  2. Magari mabovu ikiwemo na daladala kuwepo barabarani?
  3. Madereva kusimama ovyo barabarani?
  4. Madereva kutowaheshimu waendao kwa mguu na kudharau 'zebra crossing' kiasi cha kugonga watu hapo na kutochukuliwa hatua zozote?
  5. Madereva kutochukuliwa hatua yoyote wanapokwenda kasi sana kati ya mji?
  6. Daladala kujaa kiasi cha watu kuambukizana TB ndani ya mabasi?
  7. Daladala kuwachaji watu nauli mara kama mbili abiria kwa wale wanaogeuza karibu na mwisho wa ruti?
  8. Madereva na makondakta kwenye daladala kuvaa matambara badala ya sare rasmi zinazopendeza machoni kwa abiria?
  9. Makonda na madereva wanaoendeleza ubabe kwa wanafunzi?
  10. Abiria kukanyagana [wanaopata shida ni watoto na wazee] wakati wa kukimbilia kupanda kwenye gari. Je, waziri haoni ni jukumu lake kulinda wazee, watoto na wanyonge au walemavu katika jamii?
  11. Mitaa inayostahili kuwa na taa za usalama barabarani inapata taa hizo. Si tumesikia kuna Watanzania wanaozitengeneza? Au waziri hajui?
  12. Hivi njia tatu zina faida au madhara? Kuna aliyetafiti hili? Au waziri hana kasma ya utafiti?
  13. Magari yanayopita kwenye njia za watembea kwa mguu sasa imekuwa ruhusa nchi nzima?
  14. Faini ya papo kwa hapo kwanini waziri haijaomba bungeni. Itasaidia Usalama barabarani kuwa na mfuko wa ziada kuwalipa posho askari wake ili waache kudai rushwa njiani.
  15. Trafiki polisi wanaosimamisha magari ovyo ovyo majiani na kusababisha hatari waziri amewahi kuwaona au kuwasikia. Anawachukulia hatua gani.
  16. Hivi ndugu waziri hiki kisa cha magari kimekuwa ni: 'If mountain cannot go to the Mohammed, then Mohammed must go to the mountain? ' Kwa maana kwamba wenye daladala na magari ya uchukuzi idara imeshindwa kuwaita mahala fulani katika vipindi vinavyoeleweka mpaka inalazimika kuyakamata magari ovyo ovyo barabarani.

  Na kwa kuwa makonda wanajua basi utakuta njia ya Buguruni hadi kwa Nyerere siku za Jumatatu na Mnazi Mmoja Ubungo na Tabata hadi Posta siku fulani hawatoki kwa kuwa wanajua jamaa wamekaa mkao wa kula kwenye ruti zao?

  Na kwanini Usalama barabarani wanapenda njia ambazo wakubwa hawazitumii au hawapiti kabisa?

  Mheshimiwa Spika,

  Naomba kutoa hoja!
   
Loading...