Bunge na Spika Ndugai kukataa kufanya kazi na CAG ni dharau kwa Rais Magufuli

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Haijapata kutokea tangu Tanzania ijitawale kuwa na Spika mbabe, jeuri na mkorofi kama Supukali Job Ndugai. Kitendo cha kumkataa CAG Assad ni dharau, matusi na kejeli kwa mamlaka za Uteuzi wa CAG ambaye ni Rais wa JMT Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Spika Job na Nduagi na Bunge lote wameonesha dharau ya hali ya juu kwa Mhe. Rais kwa kumkataa Prof. Assad kisa ati alisema Bunge ni dhaifu. Ukitazama hili sakata lililoanzishwa na Spika Nduagi kwa jicho la tatu unaweza kubaini kwamba hapa kuna agenda imejificha.

Agenda hiyo yawezekana ikawa ni kutokana na CAG kuibua madudu ya matumizi ya hovyo ya Fedha za Watanzania kama vile matibanu ya Spika Ndugai lakini pia taarifa ya upotevu wa Fedha au kukosa maelezo ya kina jinsi Tshs. 1,5T zilivyo yeyuka na Serikali kushindwa kutoa ufafanuzi wa kina.

Kama Rais hataingilia kati kuhusu sakata hili ili kunusuru Heshima ya Bunge la Tanzania basi tunaweza kusema anachofanya Spika Job Ndugai ni maelekezo toka Juu. Ni wakti wa Prof. Assad kufungasha virago na kutafuta maisha mengine. Hii itakuwa ni udhihirisho mwingine wa Tanzania kupoteza Utawala wa Sheria.

Inasikitisha.
 
Tuko busy na waziri kuvutishwa bangi

"Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko, ukalisimamie hilo, kwa sababu nina matatizo sana na baadhi ya miradi ya maji, na ndio maana nimekuwa nikifanya mabadiliko kwenye miradi ya maji, kwa sababu haileti impact. Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa, mradi umetumika milioni 400, zilikuwa milioni 800 lakini maji hayapo, sasa nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavute bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta, ili ukienda kwenye mradi hawa mainjia wa maji wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.
 
Back
Top Bottom