Bunge: Mbunge akifa hatutatangaza kafa kwa ugonjwa gani kuanzia sasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
#NipasheHabari Bunge limesema kuwa halitatangaza ugonjwa wa mbunge yeyote kwa kuwa ni siri ya mgonjwa na hiari iko kwa familia yake kutangaza.
:
Akihitimisha kikao cha Bunge juzi jijini Dodoma, Naibu Spika, Tulia Akson, alitoa kauli hiyo baada ya kuwapo kwa hoja ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema kuwa hakuna ushahidi kuwa kuna mbunge amekufa kwa corona.

=====

Magonjwa yanayoua wabunge kutotajwa

BUNGE limesema kuwa halitatangaza ugonjwa wa mbunge yeyote kwa kuwa ni siri ya mgonjwa na hiari iko kwa familia yake kutangaza.

Akihitimisha kikao cha Bunge juzi jijini Dodoma, Naibu Spika, Tulia Akson, alitoa kauli hiyo baada ya kuwapo kwa hoja ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema kuwa hakuna ushahidi kuwa kuna mbunge amekufa kwa corona.

Aprili 20, mwaka huu, Naibu Spika alilijulisha bunge kuwa mbunge mmoja (jina limehifadhiwa) amepata maambukizo ya corona na anaendelea na matibabu.

“Waheshimiwa wabunge sisi sote ni viongozi tunafahamu ugonjwa wa mtu ni siri yake yeye peke yake, akitaka sana yeye na daktari, sasa hatuwezi kufika mahali tukalazimishana kwamba mtu aseme ugonjwa wake ni nini ama mtu mwingine amsemee mtu mwingine kwamba amekufa na ugonjwa gani,” alisema.

Alifafanua kuwa wale walioumwa Covid-19 wametangaza wao wenyewe na hakuna mahali serikali inasema nani amekufa na ugonjwa gani kwa sababu kila mtu ana ugonjwa wake na ugonjwa ni siri ya mtu.

“Kama ameamua kusema hilo ni suala lake kama hakusema mkakuta mauti imemchukua ameondoka nayo siri yake yeye na daktari, haimhusu mtu mwingine,” alisema.

Kwa mujibu wa Naibu Spika huyo, hakuna mahali Bunge litafika kutangazia wabunge kuwa mtu amekufa na kifo fulani hilo halitowezekana na libaki hivyo.

“Nadhani tutakuwa tumefuata miongozo yote ambayo inawataka wenzetu kwenye eneo la afya kufanya hivyo nasi tusingetaka kuingia kwenye eneo hilo,” alifafanua.

Wabunge waliofariki tangu kuanza kwa vikao vya Bunge ni Mbunge wa Newala Vijijini (CCM), Rashid Akibar, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Getrude Rwakatare, Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Dk. Elly Macha, Mbunge wa Dimani (CCM), Hafidh Ally Tahir, Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama, Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago, Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Augustine Mahiga.
 
Kwahiyo vifo vya Corona havitaongezeka tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ndo habari ya mjini! kwetu kujaza takwimu ya vifo hakuna faida zaidi ya kuharibu moods zetu tu na kutishia watu nao wakajifungia ndani kufa njaa kwa kushindwa kwenda hata shamba, kuvua samaki au kubangaiza machinga mitaani!! elimu za wengi darasa la nne!
 
Dah kwelii tumewapoteza weng ba ni katika uongozi wa Ndugai ndio tmeoba mtu akiwa mbunge ktoka vyama viwil tofaut

Its not over until its over...
 
Hahaha futuhi hii ni futuhi iv kwanza hakuna data KUTOLEWA kama zamani hakuna ongezeko la wagonjwa au walio kufa au waliopona hii nchi bhana acha tu
 
Back
Top Bottom