'Bunge Live' yatinga mahakama ya Afrika Mashariki

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,672
2,000
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeazimia kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kudai mambo 7 yanayohusiana na haki za binadamu ikiwemo sakata la matangazo mubashara ya vikao vya bunge (Bunge LIVE)

Kikao cha Bunge la Tanzania

Akitoa taarifa hiyo ambayo ni yaazimio ya mkutano wa wa siku mbili uliohusisha watetezi wa haki za binadamu, wadau pamoja na asasi mbalimbali za kiraia Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mtandao huo bwana Onesmo Ole Ngurumwa amesema kesi hizo zitafunguliwa hivi karibuni.

Ameyataja mambo mengine ambayo wameazimia kuyafikisha katika mahakama hiyo kuwa ni kupinga sheria ya huduma za habari iliyopitishwa hivi karibuni pamoja na suala la uchaguzi wa Zanzibar.

"Kuna wenzetu kutoka Zanzibar wamekuja na hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, tumewasikiliza tukaona wana hoja, kwahiyo nalo tumelipitisha na tutalifiksha katika mahakama hiyo"Onesmo Olengurumwa - Mkurugenzi THRDC

Jambo lingine litakalofikishwa katika mahakama hiyo ni migogoro ya ardhi hususani mgogoro wa Loliondo, na lingine ni kuiomba mahakama iwaamuru mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka na kutekeleza mkataba wa haki za binadamu kama ilivyo kwenye makubaliano ya kuundwa kwa jumuiya.

Amesema watetezi hao wamefikia maamuzi ya kuyapeleka kwenye ngazi hiyo ya mahakama baada ya kushindwa kupata haki katika mahakama za ndani ya Tanzania

Chanzo: IPP Media
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,825
2,000
Na niwaombe kabisa nyie watetezi, kama munaishtaki serikali sijui CCM.....basi muhakikishe nao wanawekwa ndani, tena muhakikishe hawapati dhamana kama wanavyowanyima dhamana wapendwa wetu..........hata kama ni kuhonga mhonge, lkn dhamana no...........
 
Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,772
2,000
Kumbe ni maazimio basi ni tofauti na kichwa cha habari.
Ingekuwa hivi .....THRDC waazimia kupeleka hoja ya "Bunge Live' kwenye mahakama ya Afrika Mashariki.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Pelekeni na suala la mita mia mbili wakati wa kupiga kura maana tunaibiwa sana na kuporwa ushindi kirahisi
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,953
2,000
Tunawatakia mafanikio mema katika harakati hizi za utetezi wa uhuru wa kupata habari.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeazimia kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kudai mambo 7 yanayohusiana na haki za binadamu ikiwemo sakata la matangazo mubashara ya vikao vya bunge (Bunge LIVE)

Kikao cha Bunge la Tanzania

Akitoa taarifa hiyo ambayo ni yaazimio ya mkutano wa wa siku mbili uliohusisha watetezi wa haki za binadamu, wadau pamoja na asasi mbalimbali za kiraia Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mtandao huo bwana Onesmo Ole Ngurumwa amesema kesi hizo zitafunguliwa hivi karibuni.

Ameyataja mambo mengine ambayo wameazimia kuyafikisha katika mahakama hiyo kuwa ni kupinga sheria ya huduma za habari iliyopitishwa hivi karibuni pamoja na suala la uchaguzi wa Zanzibar.

"Kuna wenzetu kutoka Zanzibar wamekuja na hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, tumewasikiliza tukaona wana hoja, kwahiyo nalo tumelipitisha na tutalifiksha katika mahakama hiyo"Onesmo Olengurumwa - Mkurugenzi THRDC

Jambo lingine litakalofikishwa katika mahakama hiyo ni migogoro ya ardhi hususani mgogoro wa Loliondo, na lingine ni kuiomba mahakama iwaamuru mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka na kutekeleza mkataba wa haki za binadamu kama ilivyo kwenye makubaliano ya kuundwa kwa jumuiya.

Amesema watetezi hao wamefikia maamuzi ya kuyapeleka kwenye ngazi hiyo ya mahakama baada ya kushindwa kupata haki katika mahakama za ndani ya Tanzania

Chanzo: IPP Media
Well done THRDC

Haiwezekani serikali ipige marufuku kwa sababu za 'kipuuzi' kuwa muda wa kuangalia Bunge Live ni muda wa kazi kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuwepo makazini badala ya kuangalia Bunge Live.....

Lakini serikali hiyo hiyo inakilazimisha chombo chetu hiko hiko cha Umma TBC kutangaza ziara za kampeni za CCM kila Mkulu anapofanya ziara zake akizivalisha kilemba kuwa ni ziara za kiserikali!
 
Wamabere

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
939
500
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeazimia kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kudai mambo 7 yanayohusiana na haki za binadamu ikiwemo sakata la matangazo mubashara ya vikao vya bunge (Bunge LIVE)

Kikao cha Bunge la Tanzania

Akitoa taarifa hiyo ambayo ni yaazimio ya mkutano wa wa siku mbili uliohusisha watetezi wa haki za binadamu, wadau pamoja na asasi mbalimbali za kiraia Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mtandao huo bwana Onesmo Ole Ngurumwa amesema kesi hizo zitafunguliwa hivi karibuni.

Ameyataja mambo mengine ambayo wameazimia kuyafikisha katika mahakama hiyo kuwa ni kupinga sheria ya huduma za habari iliyopitishwa hivi karibuni pamoja na suala la uchaguzi wa Zanzibar.

"Kuna wenzetu kutoka Zanzibar wamekuja na hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, tumewasikiliza tukaona wana hoja, kwahiyo nalo tumelipitisha na tutalifiksha katika mahakama hiyo"Onesmo Olengurumwa - Mkurugenzi THRDC

Jambo lingine litakalofikishwa katika mahakama hiyo ni migogoro ya ardhi hususani mgogoro wa Loliondo, na lingine ni kuiomba mahakama iwaamuru mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka na kutekeleza mkataba wa haki za binadamu kama ilivyo kwenye makubaliano ya kuundwa kwa jumuiya.

Amesema watetezi hao wamefikia maamuzi ya kuyapeleka kwenye ngazi hiyo ya mahakama baada ya kushindwa kupata haki katika mahakama za ndani ya Tanzania

Chanzo: IPP Media
Naona atakayelipia matangazo ndiyo atakayeamua kama yawepo au la. Kama mahakama ya ya afrika mashariki italipia matangazo basi itakuwa mubashara
 
Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,633
2,000
Mahakama ya Africa Mashariki ipo wapi vile?, Nairobi,Kampala au Kigali?,. THRDC inaishtaki serikali?,.Awamu hii tutaona na kusikia mengi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom