Bunge litunge sheria ya kukabiliana na watumishi hewa!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Wengi wetu tumefurahia sana baada ya Mh Rais Magufuli kulikomalia suala la watumishi hewa.

Pia tumemsikia mh Rais akiliongelea kwa undani sakata hili kwa kutupa takwimu za watumishi hewa na athari zake kiuchumi na kimaendeleo.

Suala la watumishi hewa liliwahi kuvaliwa njuga na aliyekuwa waziri wa maswala ya watumishi matehemu bi Celina O Kombani kiasi cha kutengeneza mfumo wa kieletroniki wa usajili wa watumishi unaoitwa Lowson.

Mwaka huu tumeona mafanikio makubwa na jitihada za dhati za kupambana na watumishi hewa.

Juhudi za mwaka huu ni lazima ziwekewe mfumo wa kisheria ili tatizo hili lisiweze kujirudia siku za usoni.

Ni vizuri ikatungwa sheria maalum ya kuhakikisha tatizo la watumishi hewa linaondoka kabisa.

RWANDA ina sheria maalum inayopambana na watumishi hewa na wahusika wanaosababisha hali hii(source mchangiaji wa mada BBC)

WABUNGE wetu watusaidie kutunga sheria hii kwani hili ni janga la kitaifa.
 
Nakubakiana nawe mkuu, itungwe sheria yenye adhabu kali kwa wahusika watakaofanikisha uwepo wafanyakazi hewa.
 
Back
Top Bottom