Bunge litengue sheria ya polisi kuarifiwa na kulinda mikutano ya vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge litengue sheria ya polisi kuarifiwa na kulinda mikutano ya vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Sep 9, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Baada ya polisi kuwa ndio wauwaji wa wananchi wasio na hatia kwenye mikutano ya vyama vya siasa, nashauri bunge litengue sheria ya polisi kuarifiwa na kutoa ulinzi kwenye mikutano yote ya vyama vya siasa. Kila chama cha siasa kiwe na wajibu wa kujilinda chenyewe kwa kutumia walinzi binafsi, walinzi wa vyama nk ili kila chama kiwajibike chenyewe badala ya sasa polisi kutumiwa na chama tawala kuleta fujo na kuuwa raia wasio na hatia kwa manufaa ya CCM.

  Na bunge lazima lijadili jinsi ya kufumua jeshi la polisi na kuwajibika kwa wananchi, kuangalia upya mfumo wa jeshi la polisi na IGP kuwajibika kwa bunge badala ya Raisi. Kuvunja mfumo wa Jeshi la polisi liwe na mikoa badala la kitaifa. Ajira mafunzo ya polisi yasimamiwe kimkoa ili kutoa amri za ajabu ajabu ambazo zinatolewa na watawala ili kulinda maslahi yao.

  Ninapoandika makala hii tayari makundi yote ya kijamii yamesha athirika na matumizi mabovu ya jeshi la polisi. Kifo cha ajabu polisi morogoro, kupigwa na kuuwawa kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na msingi na jeshi la polisi pale walipokuwa wakidai haki zao. Madaktari kupigwa mabomu na kunyanyaswa huku wengine wakiteswa, Kupigwa mabomu waalimu na wengine wakidhalilishwa, kupigwa wazee wa iliyokuwa east africa comm, kuuwawa raia wasio na hatia, kuvuruga kupiga mabomu na kuuwawa wafuasi wa vyama vya siasa wasio na hatia. Kukamata wananchi wasio na hatia na kuwafungulia kesi za kutengeneza, kula rushwa , kusaidia wafanya baishara haramu, kulinda wahalifu nk kuuwa waandishi wa habari na kuwatengenezea kesi za uwongo.

  Matukio ni mengi sana imefika wakati tukubali Jeshi la polisi halilindi tena usalama wa raia bali limekuwa linahatarisha usalama wa raia. leo raia wa TZ wanaogopa sana wakikutana na polisi kuliko na vibaka au majambazi kwani uwezekano wa kutoka salama ukiwa umeibiwa kwa jambazi ni mkubwa kuliko kutoka salama mikononi mwa polisi.

  Chief Mkwawa Wa kalenga
  Nchi yangua inaharibiwa kwa viongozi wake kukosa hekima na busara
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hao viongozi uliokiri kuiharibu nchi yako usiwatarajie kuitengeneza kwa kuweka hiyo sheria unayoitaka kwani kuwepo kwake ndiko kuna kamilisha huo uharibifu.
  Umepoteza muda kuandika bandiko reeeeeefu na mwishowe umejijibu mwenyewe.
  Kwaheri.
   
Loading...