Bunge lisilo na uwezo kuirekebisha serikali ni haki kuwepo?

gkutta

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
273
168
Hakuna kitu cha KIBAYA na CHA KINAFIKI katika nchi yoyote duniani, hasa ya ulimwengu wa tatu kimaendeleo, kama kutumia pesa za walipakodi kuendesha gharama za Biunge lisilokuwa na uwezo wa kuirekebisha sereikali na kudhibiti utwala mbovu usio wa kisheria na kikatiba huku Sereikali ikilitumia Bunge husika kwa wingi wa wabiunge wake uchwara kupitisha hoja zake na bajeti zake bila kuzingatia pingamizi za wabunge wa upinzani juu ya makosa yaliyopo kisheria.

Hii ni hoja ya ujumla bila kujikita kwa nchi yoyote; usiingie ovyo ukafikiri umesemwa wewe!!
 
Hakuna kitu cha KIBAYA na CHA KINAFIKI katika nchi yoyote duniani, hasa ya ulimwengu wa tatu kimaendeleo, kama kutumia pesa za walipakodi kuendesha gharama za Biunge lisilokuwa na uwezo wa kuirekebisha sereikali na kudhibiti utwala mbovu usio wa kisheria na kikatiba huku Sereikali ikilitumia Biunge husika kwa wingi wa wabiunge wake uchwara kupitisha hoja zake na bajeti zake bila kuzingatia pingamizi za wabunge wa upinzani juu ya makosa yaliyopo kisheria,...Hii ni hoja ya ujumla bila kujikita kwa nchi yoyote; usiingie ovyo ukafikiri umesemwa wewe!!

Usiwe mjinga, Bunge lolote Duniani hutokana na Vyama vya Siasa, na Chama kinachoshinda Uchaguzi ndicho kinachoongoza Serikali maana yake ni kwamba kinakuwa upande wa Serikali yake, hivyo badala ya kulaumu Bunge letu ambalo linaoongozwa na CCM, ulipaswa ulaumu Wabunge wa Vyama vya Upinzani kwa Vyama vyao kushindwa kuaminiwa na Watanzania kwa kupewa Wabunge wengi na siyo kulaumu Bunge letu!
 
Hakuna kitu cha KIBAYA na CHA KINAFIKI katika nchi yoyote duniani, hasa ya ulimwengu wa tatu kimaendeleo, kama kutumia pesa za walipakodi kuendesha gharama za Biunge lisilokuwa na uwezo wa kuirekebisha sereikali na kudhibiti utwala mbovu usio wa kisheria na kikatiba huku Sereikali ikilitumia Bunge husika kwa wingi wa wabiunge wake uchwara kupitisha hoja zake na bajeti zake bila kuzingatia pingamizi za wabunge wa upinzani juu ya makosa yaliyopo kisheria.

Hii ni hoja ya ujumla bila kujikita kwa nchi yoyote; usiingie ovyo ukafikiri umesemwa wewe!!
hivi kwa mapanki kuna bunge
 
Watanzania tunataka kuona thamani ya bunge letu sio tu kupitisha miswada ya serikali bali pia kuirekebisha serikali kuzuia mambo mengine mengi yasiyo na weledi wa kikatiba na kiutawala wa sheria!!..Laa sivyo tunajiuliza ni halali pesa za walipa kodi kutumika bungeni bila mlishonyuma wa bunge kuwatetea katika hoja zao dhidi ya serikali?
 
Kuna wabunge au vikatuni vya jengo la bunge!!? Maana siion faida yao hakika hasa katika kuiwajibisha serikali wamejaa unafiki tu.
 
Mi najiuliza ile bajeti iliyopangwa ndo itatumika?Je bajeti iliyopita walisrma wataajiri? Wameajiri? Kama hawajaajiri hela ya kuajiri imeenda wapi? Je tulipitisha hela ya chato airport na tra chato, je tulipitisha hela ya reli na ndege?
 
Usiwe mjinga, Bunge lolote Duniani hutokana na Vyama vya Siasa, na Chama kinachoshinda Uchaguzi ndicho kinachoongoza Serikali maana yake ni kwamba kinakuwa upande wa Serikali yake, hivyo badala ya kulaumu Bunge letu ambalo linaoongozwa na CCM, ulipaswa ulaumu Wabunge wa Vyama vya Upinzani kwa Vyama vyao kushindwa kuaminiwa na Watanzania kwa kupewa Wabunge wengi na siyo kulaumu Bunge letu!
Ujinga ni kudhani ushindi wa vyama hutokana na idadi ya waliopiga kura!!..Pia ujinga mkubwa ni kufikiria kuwa wabunge wa chama tawala wana kazi ya NDIYOOOOO bungeni badala ya kuisaidia serikali kufanya yaipasayo nchini!!
 
Labda haujaelewa maana ya mfumo wa vyama vingi, hivyo ndivyo ilivyo, Chama kinachoshinda Uchaguzi ndicho kinachoongoza Serikali na Chama chenye Wabunge wengi kina haki na uwezo wa kushinikiza matakwa ya Serikali yake, hakuna mahali inapofanyika kinyume chake Dunia hii ukiondoa nchi zenye Chama kimoja kama Uchina au Korea Kaskazini!

Hivyo badala ya kupoteza muda kulaumu Bunge letu, ulipaswa uwekeze muda kwenye kuwashawishi Watanzania ili wachague Wabunge wengi wa Vyama vya upinzani ili waweze nao kupinga matakwa ya Chama tawala au pia kushinikiza matakwa yao!
 
Nahisi una mgando wa fikra hasi kuhusu mfumo wa vyama vingi!!...Tanzania sio nchi ya pekee yenye mfumo huo na zipo nchi zenye mfumo huo ambazo mabunge yake sio kwa maslahi ya serikali ya chama chao bali ni kwa maslahi ya nchi na wapiga kura!!
 
Ni hasra kuona tunagharamia wabunge na bunge bila kupata mlishonyuma maridhawa value for money kwa kazi zao kubaki kuwa ni vilio vya NDIYOOOO kwa kila mswada hata uwe na mapungufu na athari kwa wapiga kura na wa;lipakodi nchini!
 
Hakika rafiki!!.. Ni hasra kuona tunagharamia wabunge na bunge bila kupata mlishonyuma maridhawa value for money kwa kazi zao kubaki kuwa ni vilio vya NDIYOOOO kwa kila mswada hata uwe na mapungufu na athari kwa wapiga kura na wa;lipakodi nchini!
 
Nahisi una mgando wa fikra hasi kuhusu mfumo wa vyama vingi!!...Tanzania sio nchi ya pekee yenye mfumo huo na zipo nchi zenye mfumo huo ambazo mabunge yake sio kwa maslahi ya serikali ya chama chao bali ni kwa maslahi ya nchi na wapiga kura!!

Nitajie nchi moja ambayo chama chenye Wawakilishi wengi Bungeni klk vyote na ambacho kimeunda Serikali ambayo kinaipinga!
 
Hakuna kitu cha KIBAYA na CHA KINAFIKI katika nchi yoyote duniani, hasa ya ulimwengu wa tatu kimaendeleo, kama kutumia pesa za walipakodi kuendesha gharama za Biunge lisilokuwa na uwezo wa kuirekebisha sereikali na kudhibiti utwala mbovu usio wa kisheria na kikatiba huku Sereikali ikilitumia Bunge husika kwa wingi wa wabiunge wake uchwara kupitisha hoja zake na bajeti zake bila kuzingatia pingamizi za wabunge wa upinzani juu ya makosa yaliyopo kisheria.

Hii ni hoja ya ujumla bila kujikita kwa nchi yoyote; usiingie ovyo ukafikiri umesemwa wewe!!

Wabunge wa Chama Cha Mauaji wanajali matumbo yao,si ulimsikia Lucy Mayenga yeye akikaa bungeni anafikiria Biashara zake
 
Aiseeeh, asante Kwa kutoa angalizo, mimi najikita kwa bunge la hapo Tanzania.

Namnukuu RC wa dar, "wabunge wanalala tu"

Kwa hiyo mimi binafsi, naona lifutwe tu hakuna linachofanya zaidi nikiliangalia bunge la Tanzania naona lina bomoa mshikamano wa kitaifa na upendo wa wananchi unadhoofishwa na yale wanayoyatenda badala ya kuisimamia serikali.

Nimechanganya, maoni ya watu wengine na yangu Kwa hiyo naomba, mtu asitoe povu.
 
Usiwe mjinga, Bunge lolote Duniani hutokana na Vyama vya Siasa, na Chama kinachoshinda Uchaguzi ndicho kinachoongoza Serikali maana yake ni kwamba kinakuwa upande wa Serikali yake, hivyo badala ya kulaumu Bunge letu ambalo linaoongozwa na CCM, ulipaswa ulaumu Wabunge wa Vyama vya Upinzani kwa Vyama vyao kushindwa kuaminiwa na Watanzania kwa kupewa Wabunge wengi na siyo kulaumu Bunge letu!
KWA HIYO IKIAMINIWA NDO UNA FANYA UJINGA SIO!!,
 
Hakuna kitu cha KIBAYA na CHA KINAFIKI katika nchi yoyote duniani, hasa ya ulimwengu wa tatu kimaendeleo, kama kutumia pesa za walipakodi kuendesha gharama za Biunge lisilokuwa na uwezo wa kuirekebisha sereikali na kudhibiti utwala mbovu usio wa kisheria na kikatiba huku Sereikali ikilitumia Bunge husika kwa wingi wa wabiunge wake uchwara kupitisha hoja zake na bajeti zake bila kuzingatia pingamizi za wabunge wa upinzani juu ya makosa yaliyopo kisheria.

Hii ni hoja ya ujumla bila kujikita kwa nchi yoyote; usiingie ovyo ukafikiri umesemwa wewe!!
Bunge la tanzania lilisha jitengenezea lenyewe mazingira ya kudharauliwa kwa sababu ya mambo na maamuzi yao yakipuuzu wawapo bungeni na kuto kuwa na misimamo kama wabunge bali kuwa kama makada wa vyama ndani ya bunge na kusimamia misimamo yao ya vyama , wabunge hawa hawana maana yeyote kwa taifa hili wafutiliwe mbali ,

maana ukiwa na 50,000/=yes namaanisha elfu hamsini, unaweza wabadilisha wote wakakufuata wewe unacho taka, hovyo kabisa hawa watu, hata kama kitaliangamiza taifa kwa siku za usoni , nililidharau bunhe hili kwa kuikataa rasimu ya warioba iliyo kuwa na lengo la kulinyoosha taifa na pengine haya wanayo yalalamikia leo yangekuwa ndani ya uwezo wao lakin ndio hivyo tuna wabunge vipofu.
 
Aiseeeh, asante Kwa kutoa angalizo, mimi najikita kwa bunge la hapo Tanzania.

Namnukuu RC wa dar, "wabunge wanalala tu"

Kwa hiyo mimi binafsi, naona lifutwe tu hakuna linachofanya zaidi nikiliangalia bunge la Tanzania naona lina bomoa mshikamano wa kitaifa na upendo wa wananchi unadhoofishwa na yale wanayoyatenda badala ya kuisimamia serikali.

Nimechanganya, maoni ya watu wengine na yangu Kwa hiyo naomba, mtu asitoe povu.
Kwa sehemu naona akili ila hili la kujikita kwa bashite nahisi umepotea njia!!...haikutumika akili pale zaidi ya huka binafsi za kutaka kujizolea sifa rafiki!
 
Back
Top Bottom