Bunge lisijadili Mitaala ya Elimu, Wabunge wengi wana upeo mdogo

Kama hili genge la wabunge likishirikishwa kwa namna yoyote ile kutengeneza mtaala wa elimu itakuwa ni janga kwa Taifa.

Bungeni kumejaa vilaza wa ajabu, elimu za kuungaunga, wale wenye elimu inayoeleweka nao ni watu wanafiki, wenye hila na waongo. Watu wa namna hiyo watatengeneza mtaala gani?

Kama tunataka kuwa na mtaala mzuri, tutafute wataalamu kutoka mataifa ya nje, hasa yale yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye elimu.
Point kubwa.
 
Tena iwe marufuku kwa Bunge hili kujadili mitala ya Elimu. Hivi Ndungai anadhani hili Bunge ni Wataalamu wa kila kitu?

Hembu waache utani kabisa, kuna vitu hawaviwezi, labda wanatafuta siku za posho tu.
Alitaka kila siku wanavyoingia kipindi cha bunge watenge muda maalumu kujadili mabadiliko ya mitaala ya Elimu Tanzania.
Hatari sana!
 
Leo Bungeni wakati wa maswali na Majibu, Kuna swali lililohusu mabadiliko ya mitaala ya Elimu ili kuendana na hali ilivyo.

Naibu waziri wa elimu alikiri kuwa mfumo wetu wa Elimu uliopo haumsaidii Mhitimu kuweza kujiajiri hivyo wapo kwenye mchakato wa kubadilisha Mitaala inayotumika kukidhi soko.

Waziri alisema wanashirikiana na wadau mbalimbali kwenye kufanya mabadiliko hayo, bunge pia litashirikishwa kutoa mapendekezo yao.

Spika Ndugai akamwambia Waziri bunge lishiriki kwenye mchakato huo na siyo kuhusishwa kupitia makongamano.

Spika Ndugai anataka kila siku bungeni kutengwe muda maalumu kwa ajili ya wabunge kujadili na kupitisha marekebisho hayo ya Mtaala wa Elimu.

Ndugu Watanzania kwa aina ya Bunge hili lililopo kujadili na kupitisha mabadiliko ya Mitaala ya Elimu ni kuingiza majanga mengine makubwa kwenye Elimu ya Tanzania, Waziri wa Elimu na Wadau wengine pendeni watoto na wanafunzi wa Tanzania hii.

Kwa aina ya Bunge tulilo nalo sasa litajadili nini kuhusu Elimu?
Mfano, Mbunge anataka wafungwa na mahabusu waende na magodoro yao huko jela, huyu atachangia nini kwenye Mtaala wa Elimu?
kubadili mtaala kunawahusu, curriculum specialist au Educationist.

Sio akina BABU NA KIBAJAJI🙄🙄🙄🙄
 
Back
Top Bottom