Bunge linaweza kusema lilikosea kumuunga mkono Rais baada ya habari hii?

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Regional
Monday, June 24, 2002
--------------------------------------------------------------------------------

Dar Officials Accused of
Abetting Arms Racket
By RICHARD MGAMBA
SPECIAL CORRESPONDENT
Top Tanzania security officials have been accused of complicity in an illicit trade involving arms smuggled in by Russian-made aircraft that fly fresh Nile perch fish fillet from Mwanza to Europe.

Commenting on the allegation, the Mwanza Regional Commissioner, Stephen Mashishanga confirmed to The EastAfrican last week in Mwanza that in October 2001: "We received the information from our security officers at Mwanza airport about cargo planes being used to bring in arms in the country and we informed top-level security organs for action."

He said that during the same period, his officers detained a cargo plane from Ukraine which was loaded with arms, but a day later "we received instructions from top-level security organs instructing us to release the plane."

He, however, declined to reveal the names of the officials who gave the instructions to release the aircraft.

On October 2 last year, security officers in Mwanza airport detained a cargo plane believed to be carrying arms on a flight supposedly originating from Israel to Angola.

The Antonov 12 plane, belonging to Ukraine Cargo Airways, with a capacity of 35 tonnes of cargo, was however released the next day.

A government source told The EastAfrican in Mwanza recently that the weapons enter the country through Mwanza airport, which has been described as the conduit for arms smuggled into countries affected by civil strife by arm dealers from Europe, Asia and the Middle East.

Government sources told The EastAfrican that security at Mwanza airport was poor, making it a popular route through which arm dealers smuggle their wares into the Great Lakes region.

The Member of Parliament for Shinyanga, Leonard Derefa, criticised Minister for Home Affairs Seif Khatib for not taking measures to control the situation.

The MP attributed the increased incidence of arms smuggling to security laxity at places such as Mwanza airport.

Mr Derefa told parliament in Dodoma last week, "I asked the Minister for Home Affairs what steps he was taking to curb the situation and he said he was 'thinking' of taking measures. How can one be still 'thinking' about something as serious as this instead of stopping the racket?"

He challenged the minister to resign "for being irresponsible on this matter."
 
Mugishagwe.. that is not even enough.. when I post my piece (which I'll do tomorrow) you'll be suprised to know that even JK himself new that arms trafficking was going on through Tanzania. It is a ten pages in depth research on Tanzania's role in arms trafficking since 1997 to 2006!!!
 
MAPANKI….MAPANKI; Wanahabari kateni mzizi wa fitina!!!

Nakiri kuwa mmoja kati ya wengi ambao hawakuwa wameiona filamu ya Darwins Night Mare kipindi ambacho Rais aliishambulia. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuusikia mjadala huu kutoka kwa mheshmiwa Rais Jakaya kikwete.Yaliyozungu mzwa na Jakaya pamoja na mengi yaliyopata kuzungumzwa baadaye yananisukuma nami kutupa shilingi yangu.Hoja zilizotolewa ni nyingi na nyingine zenye kudiriki kutishia uhuru wa mtu wa kushiriki na kutoa maoni yake.Nilistushwa na mmoja wa wachambuzi aliyetoa hoja ya kumshitaki mmoja kati ya watu waliohojiwa ndani ya filamu hiyo.Nilitatanishwa na kauli ya Rais kwamba filamu hii ni ya kutungwa na wananchi waliohojiwa mule ni waigizaji kama walivyo wasanii wengine.Nikajiuliza kama kweli yupo mtanzania ambaye bila kujali itikadi yake angeweza kuigaragaza hadhi ya nchi yake namna ile.Binafsi nikajijibu hakuna,ingawa wapo ambao kwa hoja watasema kuna watu wa namna hii kama alivyotanabaisha mheshmiwa Raisi.


Sasa tuache yote nyuma na tuanze kujadili mustakabali wa Taifa.Ni kweli kabisa wote tunapaswa kukubaliana na ukweli mchungu kwamba taswira ya Tanzania imechafuka.Si dhumuni la makala hii kuanza kutoa mhadhara mrefu na mpana juu ya athari za kijamii na kiuchumi ambazo Tanzania kama nchi yeyote ulimwenguni na Tanzania kama jirani mwema wa nchi za maziwa makuu inaweza kuzipata.Nikiangali a kwa undani karibu wachambuzi wote walishabihiana katika eneo hili na tofauti ilikuwepo tu katika namna ya kukabiliana na hili zimwi lililopo mbele yetu.Ilipatwa kusemwa na mwanaharakati Martin Luther King kwamba busara ya binadamu haipimwi wakati hali ni shwari na mambo yamenyooka,bali wakati mambo si shwari ama kuna mvutano(Tafsiri isiyo rasmi).Utakubaliana na usemi huu pamoja na kuniunga mkono kwamba busara zetu Watanzania pamoja na kiongozi wetu sasa zipo katika mizani.Ni mizani hii pekee itakayongamua uwezo na uthabiti wetu katika kutetea hadhi,haki na utu wetu.Ni mizani hii pekee itakayo engua chuki na mgawanyiko ulio hatarini kutokea sababu ya yaliyooneshwa katika filamu hii baina ya Tanzania na majirani zake wa maziwa makuu walio katika vita.Tukumbuke pia mizani hii itatabiri mustakabali wa hali ya kiuchumi na mahusiano ya kibiashara baina ya nchi yetu na zile za magharibi.


Ni dhahiri kuwa filamu hii mbali ya kupigwa vijembe na baadhi ya watu, ina asilimia kadhaa za ukweli ndani yake.Sidhani kama mtunzi aliamua kuwa gaidi wa ki-namna yake na kuamua kuichafua Tanzania.Kama ni hivyo hatua ya serikali kuishambulia filamu katika mtindo wa mashairi ya taarabu sio sahihi.Kama ni hivyo basi serikali ingemtangaza kuwa adui namba moja na gaidi la kimataifa na msako kuanza mara moja.Iko wazi kwa watu wote kuwa Osama Bin Laden mbali ya kujitangaza kuhusika na milipuko ya septemba 11 hakuna aliyemuona akifanya hivyo.Lakini hii haikuizuia Marekani kumtangaza kama gaidi na kuanza mashambulizi kwa lengo la kumtafuta.Si lengo langu kuchambua uhalali wa Marekani kufanya hivyo ila najaribu kuonyesha ni jinsi gani hatua kali zinaweza kuchukuliwa kwa maadui wa Taifa na kimataifa ili kuweka kikomo katika uhalifu.Swali la kujiuliza Watanzania hapa ni kwa jinsi gani Marekani inashwawishika kuamini kuwa Osama Bin Laden kwanza ni mtu aliye hai na kweli kuwa na tishio kwa usalama wa Taifa la Marekani.Binafsi nashawishika kuamini hivyo kwa uzito na uthabiti wa hoja zitolewazo kuthibitisha malalamiko hayo.Hapa tunaona kuwa kumbe ni Nguvu ya hoja ndiyo inayoweza kuishi milele katika mjadala.Mtunzi wa Darwins Nightmare kwa upande wake ametoa hoja na kuithibitisha kwa njia ya picha za video.Mtunzi anakwenda mbali zaidi ya hapo tena kwa uhakika na kujiamini anaeleza namna gani alifanikiwa kupiga picha za filamu yake.Katika moja ya mahojiano aliyofanya mara baada ya hotuba ya Raisi anazungumzia bila kificho namna gani alilazimika kubadili utambulisho wake ili kuweza kupenya katika madege ya kirusi yanayosemekana kubeba silaha za maangamizi.Katika mantiki ya kawaida kabisa ina maana yeye ameshatoa hoja yake na kuisimamia sasa ni kazi kwetu kutoa hoja zetu.Watafiti husema No research..no right to speak naam!! ni kwa utafiti alioufanya mtunzi ndio akapata haki ya kuzungumza kwa namna aliyoichagua yeye.

Kwa kutambua mambo yote hayo tunaweza kujiuliza iwapo katika kukanusha kwetu tulifanya utafiti??Na kama hatukufanya tumeitoa wapi haki ya kuzungumza?? Na kama tulifanya iweje tushindwe kukanusha kwa hoja na vielelezo badala yake tuishie kushambulia ki-blaa blaa tu hali ya kuwa uchafu katika sura ya Tanzania unaendelea kubaki palepale.Pamoja na yote yaliyotokea naamini bado tunayo nafasi ya kulinda thamani na utu wetu.Ni katika fikara hizo ambapo nakwazika na namna ambavyo watu wenye uwezo wa kuiokoa Tanzania katika hili wanaposhindwa kufanya hivyo.Siamini kama huu ni wakati wa kufanya neno Mapanki kama la kutaniana mitaani na kunakshia vichwa vya habari katika magazeti yetu. Nasikitishwa na uhodari wa baadhi ya wachambuzi makini ninao waamini nchini kwa kuibua mjadala uliochacha kama huu.Nalazimika kusema ni mjadala uliochacha kwa sababu filamu hii haikutoka jana wala leo na kama mlivyosikia ilishwawahi kushinda tuzo.Kwa taarifa yetu tu Filamu haswa za aina ya Documentary moja ya kigezo kinachozifanya zishinde katika tuzo yoyote ya filamu Duniani ni suala la ubora,uasilia na uhalisia wa Dhamira inayozungumziwa. Kwa kutambua hili tunapaswa kabla ya kuushwawishi umma na Jumuiya ya kimataifa tuwe wenyewe tunashawishika na tunachokisema. Ikumbukwe kuwa Dunia haitaki tu kuona ushujaa wetu katika kukana hoja za filamu hii bali pia kuona namna gani wahusika watashughulikiwa iwapo itagundulika kuwa yaliyomo katika filamu hii ni ya kweli.Na iwapo itagundulika kama madai haya si kweli basi dunia igependa kuona ni namna gani Tanzania inawashughulikia.


Tanzania imebarikiwa kuwa na vyombo vya habari vingi tena vingine makao makuu yake ikiwa ni kanda ya ziwa.Kama hii haitoshi bado tunao waandishi binafsi ambao na wao kwa kutumia ujuzi wao wanaweza kufanya uchunguzi ili wapate haki ya kuzungimza.Kulingan a na kipawa na fursa alizonazo mwanahabari ama chombo cha habari tunaweza kuchagua namna gani tuwasiliane na Dunia kwa ujumla wake.Utakubaliana na mimi juu ya dhima mojawapo ya vyombo vya habari mbali ya kuburudisha ni kuhabarisha na Kuelimisha.Nikizung umzia kuhabarisha hapa namaanisha hoja zenye vielelezo vya Habari husika vinavyo wapa wanajamii habari sahihi,makini na hali halisi ya mambo yalivyo katika ukanda huu ulioshambuliwa na Darwins Nightmare.Izingatiw e kuwa kuhabarisha huku kuzingatie maslahi ya nchi kwa kutoa ukweli na ukweli mtupu ili kutoka hapo tujue ni wapi na namna ipi tunakwenda.Uhabaris haji huu usitawaliwe na siasa wala propaganda zenye lengo la kufichana fichana na kulindiana vitumbua vyetu bali tujali ubora wa habari na usahihi wake.Kwa kutumia documentary kwa mfano ioneshwe dhahiri kama Biashara hii haramu ya silaha ipo ama haipo pamoja na mengine mengi yaliyotajwa katika filamu hii.Tena kabla sijasahau napenda kufikisha salamu zangu kwako mjomba mheshmiwa Rais kwamba wazungu husema Two wrongs wont make it right…kwa Tafsiri rahisi makosa mawili hayawezi kuhalalisha kitendo na kukifanya kionekane sahihi..Sikutarajia mheshmiwa uhalalishe Umalaya,uomba omba na kula mapanki eti tu kwa sababu mambo haya hata nchi za magharibi yapo….salamu zangu kwako mjomba!!


Mimi ni mmoja kati ya waumini wazuri wa demokrasia na haki za binadamu.Natambua pia kuwa serikali yangu ni waumini wenzangu katika hayo hivyo itakaa mbali ili kuhakikisha vyombo vya habari husika vitakavyoitikia wito huu vitapewa uhuru wa kufanya hivyo.Kwa wanahabari au mwanahabari atakayetoka na ripoti mbadala ambayo aidha itathibisha ukweli wa Darwins NightMare ama uongo wake amini nakuambia jina lako litabaki katika historia kama mpambanaji wa mustakabali wa taifa letu.Iwapo itathibitika kuwa hoja za filamu hii ni za kweli basi wanahabari waende mbali zaidi na kutuhabarisha kuwa ni namna gani yaliyotokea yamefanikiwa kutokea ndani ya ardhi ya kisiwa cha amani Tanzania.Wanahabari wasikome..tena wasikome kabisa waendelee mbele na kusema ni nani basi wahusika wakuu wanaowezesha hayo madege kupita aidha pasipo kupekuliwa ama kupekuliwa pasipo uangalifu.Hii ni fursa ya aina yake kwa Tanzania pamoja na vyombo vya habari kuidhihirishia dunia ukomavu wake katika kielelezo kikuu cha uhai na utashi wa Taifa katika maisha ya kila siku ya watu wake yaani Demokrasia.Kwa uvumbuzi huu sasa serikali nayo inapaswa kuionyesha dunia jinsi gani italifanyia kazi suala hili.Moja kati ya mengi ambayo serikali inaweza kufanya ni kuunda timu maalum ya kuchunguza ni kwa jinsi gani ubadhirifu huu ulitokea na ni nani alihusika na kwa namna ipi.Kana kwamba hii haitoshi seerikali sit u kwa kusafisha jina letu bali kwa kutambua uzito wa jambo hili iwachukulie hatua wahusika wote katika mchezo huu hatari.


Inaendelea .......................
 
Wakati huohuo iwapo vyombo vya habari vitatoka na taarifa inayokanusha kwa hoja na vielelezo filamu ya Darwins Nightmare basi ni hapo ambapo dhima ya kuelimisha itakapokushika mkondo wake.Huu utakuwa wakati wa kuielimisha dunia juu ya ukweli halisi kuhusiana na shutuma hizi zinazoitia doa bendera yetu.Ni kipindi hiki ambapo bila jazba tena kwa uhakika ambapo tunaweza sasa kusimama hadharani na kukanusha kwa hoja na vielelezo kuwa hakuna kitu cha namna hiyo katika nchi yetu hii kisiwa cha amani.Ni katika hili ambapo kwa kushawishika na kile tunachoueleza umma tutakapoweza kupioga hatua mbele zaidi ya kumtangaza mtunzi wa filamu ile kama Adui namba moja wa Tanzania na gaidi mkubwa.Serikali hapa sasa kwa kutambua uovu wa tulichotendewa itakapoamua kum-buruza katika mahakama ya kimataifa Muongozaji wa filamu ya darwins Nightmare na washirika wake.Katika kufanya hivi izingatiwe pia Watanzania waliohusika wachunguzwe kuona kama na wao wanahusika kwa namna moja ama nyingine katika kupika uongo uliomo humo.Hata hivyo hii izingatie uhuru na haki ya mtu ya kujieleza kwa sababu huenda kwa mazingira waliyohojiwa walizungumzia kile wanachokifahamu katika eneo lao husika na wala si ukanda wa maziwa makuu kwa ujumla.

Kama hujui unapotoka,hujui unapokwenda, fikiri kabla ya kutenda.Nalazimika kumaliza na msemo huu kwa kuwa katika hili tunapaswa kuzingatia mengi.Mosi,tujue tunapotoka kwa kumchukulia Mtunzi kama mtafiti lazima alikuwa na hypothesis yake ambayo alikuja kuithibitsha. Lazma tujue nini kilimvutia Mtunzi kuchagua dhima hii ya kutisha katika kufanya utafiti wake na hatimaye filamu hii.Lazma tuukubali ukweli kuwa filamu hii haijaishambulia Tanzania peke yake bali mataifa ya magharibi pia ambayo kwa mujibu wa mtunzi anayaita makatili na yenye kiu ya kujilimbikizia mali.Ukimya wa mataifa haya katika kukanusha madai ya filamu hii unapaswa kutuzindua na kutambua uzito wa hoja na vielelezo vilivyotumika na muandishi.Katika mtazamo huu huu ukimya wa mataifa haya kwa sasa unaonyesha ni jinsi gani wanafanya utafiti kabla ya kutoka kinaga ubaga hadharani kutunisha misuli yao ili kupinga shutuma hizi.Naam!!inatupas a tufikiri kabla ya kutenda na safari hii wanhabari kama ilivyo ada wawe mstari wa mbele kuchimbua mzizi wa fitna na kuukata.

Angalizo kwa wadau wote tu ni kwamba inapaswa isiwepo hali hata ya kushukiwa kuwepo kwa jambo lolote ambalo ni kinyume na jadi yetu.Kama ilivyo kwa askari polisi ambaye anaambiwa aishi katika namna ambayo Raia watamuamini na asiwe na doa wala kushukiwa kuwa na doa basi vivyo hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa Tanzania kama Nchi ambayo ni kisiwa cha amani,mpatanishi wa wagombanao na kimbilio la wanyonge.Naamini hapa ni pazuri kwa kuanzia haswa kwa kuzingatia kuwa tunavyo vyombo habari Makini ,wanahabari jasiri na mahiri katika kuandika na kuandaa habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.Waswahili husema usione kobe kainama,ujue anatunga sheria basi kwa msemo huu nasi tutunge sheria mara baada ya kuinama na kusukuti kwa marefu na mapana yake.Shime mabibi na mabwana mwenye kalamu ashike kalamu na mwenye kamera ashike kamera tujitose kanda ya ziwa kwa utafiti utakaotupa haki ya kuzungumza.Mapanki Mapanki…..wanahabari kateni mzizi wa fitina!!Asalam alleykum
 
Back
Top Bottom