Bunge linapokosa sauti ya pamoja

hittler

Member
Jul 18, 2011
55
10
Napenda kuwapongeza wabunge wote walio na moyo thabiti wa kutetea na kupigania maslai ya Taifa. Ingekuwa vizuri kama wabunge wote wangefikia mahali wakawa na sauti moja na kupiga kura ya kutokumuamini mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali na katibu mkuu kiongozi ili kumshinikiza rais kuwaondoa kama yeye kaona bado anawataka. Ni adha isiyo kifani kwa mtu kama katibu mkuu kiongozi kuwa na power zaidi ya waziri mkuu.
Wabunge mnadhamana kubwa sana ya kulitetea taifa katika nyanja tofauti tofauti tatizo lenu mnakosa umoja, mnataka kuonyeshana umwamba Bungeni, hapo mnakosea lazima muwe wamoja kama kuna jambo nyeti linalogusa taifa, siyo kila kitu lazima mpokee order kutoka kwa mwenyekiti au katibu wa chama, wananchi wamewachagua wakiwa na imani kuwa mnaweza, onyesheni uwezo wenu wa kujenga hoja kwa umoja na ifikie mahali tuwasikie mkitumia madaraka yenu kuwaondoa watu wabovu kwenye ngazi zao, ata kama kateuliwa na rais. Nyie ndiyo mnaotunga sheria lakini mmekuwa mstari wa mbele kuzipindisha, utawala wa kisheria ni hadithi tu, badilisheni sheria, badilisheni mfumo wa ujima wa kutetea maslai ya chama na badala yake tuwe na maslai zaidi kitaifa. Kukosa kwenu sauti ya pamoja ndiko kunakolipeleka taifa letu kaburini, mkiwa na umoja ata rais atakuwa makini katika maamuzi yake na ata uteuzi na utetezi wa watu wasiofaa kuliongoza taifa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom