Bunge linapokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara kuna jambo sijalielewa naomba mnijuzuze | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge linapokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara kuna jambo sijalielewa naomba mnijuzuze

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rumishaeli, Jul 26, 2012.

 1. Rumishaeli

  Rumishaeli JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 225
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wakuu wa JF kila wizara inapohitimisha bajeti yake bungeni, bunge hukaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara husika na wabunge huuliza maswali spesifiki kwa kila kipengele kwa wizara husika. Je nini kinachotoke pale waziri husika anapotoa majibu ambayo either ni general au hayajibu swali husika kutoka kwa mbunge. Maana mara nyingi nimeona yanapotokea hayo mwenyekiti huendelea kumwita mbunge mwingine kama vile waziri husika amejibu sawia. Wanajamii wenzangu nijuzeni maana majibu ya mawaziri wetu naona hayana mshiko kwa maswali hayo wakati wa bunge kukaa kama kamati.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hicho ndiyo kipindi muhimu sana katika mjadala wa bajeti. Wakati bunge likiendelea na mijadala mara nyingi ni michango ya wabunge kutoa maoni yao na ushauri kuhusu miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyopo majimboni kwao inayohusiana na wizara husika. Pia mijadala na michango huzungukia masuala ya sera. Bunge linapokaa kama kamati ndipo hasa mafungu ya pesa zilizoombwa na wizara yanapojadiliwa kwa kina. Waziri anatakiwa kujibu hoja na maswali mbalimbali yanayoulizwa na wabunge juu ya vifungu hivyo kwa ufasaha ili bunge liidhinishe pesa katika kifungu husika. Waziri akishindwa kutetea sawasawa kifungu hicho anaweza kujikuta bunge likiamuru pesa zipunguzwe au ziongezwe katika kifungu husika.
  NAWASILISHA
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mkuu nawe ni mtu wa mjengoni nini? usifiche vua anonimity tukutambue kama wenzio akina mwigulu, mnyika na zitto. Thanks umenielewesha!
   
 4. Stanley.

  Stanley. JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Majibu ya kisima ni sahihi. Niongeze pia kama waziri akitoa majibu yakiridhisha au la mwisho mwenyekiti anawahoji kwa kifungu husika. Hapo sasa ndio uamuzi unafanyika kupitisha kifungu au la. Inatakiwa wabunge waliowengi wakubali ndipo kipite. Ukiona imeungwa mkono hata kama kuna mbunge mwingine hakujibiwa vizuri ni kwasababu wenzake hawakumuunga mkono na kusema HAPANA.
   
Loading...