Bunge Linapojadili Maoni ya Kambi ya Upinzani Badala ya Budget ya Serikali: Inaashiria nini?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,794
71,214
Wakuu jamvini, Nimekuwa nafuatilia mijadala ya Bunge letu la Budget kwa muda sasa ila sasa nimechoka kabisa.
Kilicho nichosha ni hii tabia ya baadhi ya wabunge wengi (hasa wa CCM) kutumia muda wao wote kujadili mstari kwa mstari wa maoni ya Upinzani katika kila Budget iletwayo na Wizara.

Nijuavyo mimi maoni ya kambi ya upinzani sio lazima yafuatwe na serikali iliyoko madarakani hivyo kama yana makosa serikali inayaweka pembeni na bado inakuwa haijavunja sheria yeyote.

Sasa najiuliza kwa nini wabunge wa CCM na baadhi wa CUF wanatunisha Misuli na kutumia nguvu nyingi ku crash maoni ya Chadema na watoa maoni hayo wakati siyo yatakayo endesha serikali 2012/2013?

Wanapoteza muda wao kisha wanaishia na kusema "Mhe Spika naona waziri asilisahau jimbo langu linakabiliwa na umasikini"
Najiuliza tena Hili Linaashiria nini?
 
Bajeti yao dhaifu,
sasa wafanye nini?
Ni kweli yaweza kuwa hivyo, sasa kwa nini wasijadili katika kuifanyia marekebisho ili iwe imara? kujadili(kupingana) maoni ya upinzani kunawasaidiaje maana hayakuletwa kujadiliwa.
 
Chadema wanachonga barabara then wengine wote wanapita huko
 
bunge la sasa halina tofauti na katuni za tom & jerry!!

bunge lina vituko kila kukisha afadhali ya jana wanapoteza muda bure na kutunyonya wananchi kwa kukaana kubwatukiana pasipo sababu za msingi ushabiki wa kisiasa badala ya maslai ya wananchi
 
Ni kweli yaweza kuwa hivyo, sasa kwa nini wasijadili katika kuifanyia marekebisho ili iwe imara? kujadili(kupingana) maoni ya upinzani kunawasaidiaje maana hayakuletwa kujadiliwa.
Akili zao dhaifu.
Haioni bajeti dhaifu.
Wanadhani bajeti kivuli ya CDM ndo itakuwa implemented.
Once DHAIFU always DHAIFU.
 
Soma katuni ya masoud Kipanya leo tarehe 4 julai kwenye mwananchi ndo utapata picha ya BUNGE
 
Wakuu jamvini, Nimekuwa nafuatilia mijadala ya Bunge letu la Budget kwa muda sasa ila sasa nimechoka kabisa.
Kilicho nichosha ni hii tabia ya baadhi ya wabunge wengi (hasa wa CCM) kutumia muda wao wote kujadili mstari kwa mstari wa maoni ya Upinzani katika kila Budget iletwayo na Wizara.

Nijuavyo mimi maoni ya kambi ya upinzani sio lazima yafuatwe na serikali iliyoko madarakani hivyo kama yana makosa serikali inayaweka pembeni na bado inakuwa haijavunja sheria yeyote.

Sasa najiuliza kwa nini wabunge wa CCM na baadhi wa CUF wanatunisha Misuli na kutumia nguvu nyingi ku crash maoni ya Chadema na watoa maoni hayo wakati siyo yatakayo endesha serikali 2012/2013?

Wanapoteza muda wao kisha wanaishia na kusema "Mhe Spika naona waziri asilisahau jimbo langu linakabiliwa na umasikini"
Najiuliza tena Hili Linaashiria nini?
Yangekuwa siyo ya kujadiliwa na wabunge yasingewasilishwa.
 
ukiwauliza wabunge wa ccm wanakwambia eti tunajibu mapigo ndiyo maana wanaacha hoja iliyoko mezani wanaparamia maoni ya kambi ya upinzani,kwa wabunge wa cuf ni chuki binafsi tu ambazo wameshindwa kuzificha na sasa wamekuwa wakizionyesha waziwazi lakini niseme tu majibu ya haya yote mh. mnyika alishayatoa kuwa "huu ni uzembe wa bunge na wabunge na upuuzi wa wabunge wa ccm" only that
 
Unategemea nini kwa wabunge wanaotumia masaburi kufikiri na kuongozwa na mwenyekiti dhaifu?
 
CHADEMA imewafanya Ccm waweweseke hasa hii M4C wabunge wake pamoja na mawaziri wanahofia sana uchaguzi wa 2015.Endelea kufuatilia bunge utabaini.
 
images
 
suluhisho katiba mpya jamani

tuondoe makambi bungeni. bunge tulifanye moja kusimamia seriakali. na kuishairi.

bunge lisifanywe sehemu ya kufanyia ubishi wa kisiasa bali ni chombo muhimu kwa kusimamia serikali. utashangaa waziri anaenda kusaini mkataba wa madini uingereza wanaelezwa wananyamaza lakini aliyeleta mawazo ya kuboresha bajeti anabishiwa.

wabunge walio wengi wanafikiri bungeni ni mahali pa kufanyia debate kama za sekondari za upande unaosapoti na upande unaopinga huku rasilimali zikiporwa wao wako kwenye mchezo tu. kuna uozo mwingi tu katika utendaji waserikali wao ni ubishi wa kivyama tu

kitabu cha "katiba mpya na mwelekeo wa uchumi" kinachambua udhaifu wa bunge na kuonyesha jinsi vyama vya siasa vilivyopora bunge kutoka kwa wananchi na kulifanya sehemu yao ya kubishania jiandae kupata nakala
 
Wanajaribu kuhalalisha bajeti za magamba zinazopita kwa rushwa.....ccm na wabunge wake kupitisha bajeti kwa njia ya rushwa ndicho kilichotufikisha hapa baada ya miaka 50 ya uhuru.....wanahalalisha uhuni wao....2015 is too close
 
Back
Top Bottom