Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Habari wakuu,
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya spika Makinda,kwa muda mrefu sasa, limeonyesha udhaifu mkubwa na pengine limekuwa na nidhamu ya woga kwa mh.Raisi.
Nasema hivi kwasababu Bunge limekuwa likipitisha maazimio mengi tu lakini serikali ya JK haietekelezi na wabunge wanaonekana kunywea kabisa kwani hawaonyeshi dhamira ya kweli ya kuhakikisha serikali inatekeleza.
Nitataja maazimio machache tu ambayo serikali ya JK haijatekeleza mpaka leo na wabunge wamenywea.Maazimio hayo ni kama vile:-
1.Maazimio ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa Richmond
2.Maazimio ya Bunge kuhusu Jairo
3.Mabilioni ya Uswis
4.Mikataba kupelekwa Bungeni kabla ya kusainiwa
5.Maazimio ya Bunge kuhusu uchunguzi wa kashifa za Meremeta,Kagoda na Deep green finance.
Hiyo ni mifano michache tu na wewe unaweza kuongeza katika hiyo orodha.
Wabunge wamekuwa waoga kuhoji kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo ambayo Raisi wa nchi ana nafasi kubwa katika kuyatekeleza na kuyasimamia.Kwa mfano kuhusu Jairo,waziri mkuu alitamka bungeni kuwa anasubiri Raisi atue South Afrika na kisha atoe maamuzi lakini mpaka leo kimya na hakuna mbunge anaehoji.
Hata maelezo ya aliekuwa waziri wa mifugo,ndugu Mathayo David, kuwa bajeti inayopitishwa bungeni na kiasi kidogo(pungufu) ambacho wizara yake imekuwa ikipewa kila mwaka ambapo bila shaka alikuwa akimanisha ni matokeo ya udhaifu wa mwenyekiti wa baraza la mawaziri lakini hakuna mbunge alieitafakari kwa makini maelezo yale ya aliekuwa waziri wa mifugo.
Ukiachilia mbali maazimio hayo,pia Raisi akiwa anahutubia Bunge alivunja katiba kwa kuwataka wezi wa EPA warudishe fedha walizoiba ndani ya miezi mitatu vinginevyo wangeshughulikiwa.Pamoja na ukweli kuwa Raisi hana mamlaka ys kusamehe mtujumiwa ambae bado hajahukumiwa na mahakama,wabunge walikaa kimya badala ya kuhoji na kujadili kauli hiyo bungeni na pengine kumtaka Raisi awajibike.
Kwa ujumla,mambo ni mengi ambayo Raisi kayapuuza ila wabunge wetu hawana habari kazi yao ni kukomaa na mawaziri na waziri mkuu tu.Kila siku utasikia kusudio la kupiga kura ya kumuondoa waziri mkuu lakini kura ya kutokuwa na imani na Raisi ni jambo haramu!
In short,Bunge letu ni dhaifu sana mbele ya Raisi na ataendelea kufanya atakavyo.