Bunge linaogopa kumshughulikia Kikwete na badala yake linatoa kafara mawaziri tu !

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Habari wakuu,

Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya spika Makinda,kwa muda mrefu sasa, limeonyesha udhaifu mkubwa na pengine limekuwa na nidhamu ya woga kwa mh.Raisi.

Nasema hivi kwasababu Bunge limekuwa likipitisha maazimio mengi tu lakini serikali ya JK haietekelezi na wabunge wanaonekana kunywea kabisa kwani hawaonyeshi dhamira ya kweli ya kuhakikisha serikali inatekeleza.

Nitataja maazimio machache tu ambayo serikali ya JK haijatekeleza mpaka leo na wabunge wamenywea.Maazimio hayo ni kama vile:-

1.Maazimio ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa Richmond

2.Maazimio ya Bunge kuhusu Jairo

3.Mabilioni ya Uswis

4.Mikataba kupelekwa Bungeni kabla ya kusainiwa

5.Maazimio ya Bunge kuhusu uchunguzi wa kashifa za Meremeta,Kagoda na Deep green finance.

Hiyo ni mifano michache tu na wewe unaweza kuongeza katika hiyo orodha.

Wabunge wamekuwa waoga kuhoji kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo ambayo Raisi wa nchi ana nafasi kubwa katika kuyatekeleza na kuyasimamia.Kwa mfano kuhusu Jairo,waziri mkuu alitamka bungeni kuwa anasubiri Raisi atue South Afrika na kisha atoe maamuzi lakini mpaka leo kimya na hakuna mbunge anaehoji.

Hata maelezo ya aliekuwa waziri wa mifugo,ndugu Mathayo David, kuwa bajeti inayopitishwa bungeni na kiasi kidogo(pungufu) ambacho wizara yake imekuwa ikipewa kila mwaka ambapo bila shaka alikuwa akimanisha ni matokeo ya udhaifu wa mwenyekiti wa baraza la mawaziri lakini hakuna mbunge alieitafakari kwa makini maelezo yale ya aliekuwa waziri wa mifugo.

Ukiachilia mbali maazimio hayo,pia Raisi akiwa anahutubia Bunge alivunja katiba kwa kuwataka wezi wa EPA warudishe fedha walizoiba ndani ya miezi mitatu vinginevyo wangeshughulikiwa.Pamoja na ukweli kuwa Raisi hana mamlaka ys kusamehe mtujumiwa ambae bado hajahukumiwa na mahakama,wabunge walikaa kimya badala ya kuhoji na kujadili kauli hiyo bungeni na pengine kumtaka Raisi awajibike.

Kwa ujumla,mambo ni mengi ambayo Raisi kayapuuza ila wabunge wetu hawana habari kazi yao ni kukomaa na mawaziri na waziri mkuu tu.Kila siku utasikia kusudio la kupiga kura ya kumuondoa waziri mkuu lakini kura ya kutokuwa na imani na Raisi ni jambo haramu!

In short,Bunge letu ni dhaifu sana mbele ya Raisi na ataendelea kufanya atakavyo.
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
mkuu tanzania hakuna wabunge bali kuna wabunge njaa. ukitaka kujua hilo angalia wanavyotumia mihela mingi kupigania huo ubunge. kwa kifupi ni kama wanawekeza. sasa wakifanya impeachment na ubunge wao unaota mbawa. utafikiri wako tayari kwenda kuwekeza tena? wakati wamewekeza kwa muda wa miaka 5? think, chukua hatua.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
mkuu tanzania hakuna wabunge bali kuna wabunge njaa. ukitaka kujua hilo angalia wanavyotumia mihela mingi kupigania huo ubunge. kwa kifupi ni kama wanawekeza. sasa wakifanya impeachment na ubunge wao unaota mbawa. utafikiri wako tayari kwenda kuwekeza tena? wakati wamewekeza kwa muda wa miaka 5? think, chukua hatua.

Ni taasisi ya kinafiki sana.

Hawako serious hawa watu.Wanachotaka wengi wao ni huo uwaziri tu!
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,036
2,000
Wameonewa sana na wamedhalilishwa sana ila wale watendaji wakuu awataguswa ata kidogo IGP,CDF,DIRECTOR WA TISS. POLENI SANA WATZ WALIOFANYIWA UNYAMA NA HAO MAKAFIRI WA CCM MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,831
2,000
Wameonewa sana na wamedhalilishwa sana ila wale watendaji wakuu awataguswa ata kidogo IGP,CDF,DIRECTOR WA TISS. POLENI SANA WATZ WALIOFANYIWA UNYAMA NA HAO MAKAFIRI WA CCM MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.

Watanzania tuna kila sababu ya kuandamana kutaka JK aondoke madarakani!
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,826
2,000
JK ni janga la Taifa, Wabunge wetu wengi ni walamba viatu wa JK hakuna wa kumnyooshea kidole..

Huwa nashangaa kusikia Mibunge minafiki ikilalamika eti Rais anakwamishwa na watendaji aliowateua halafu sijawahi kusikia Rais kilalamika kukwamishwa na wateule wake......
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,870
2,000
Mimi ninachoona hapa ni tatzo la kutokuwa na elimu juu ya mambo mengi,hivyo tunakuwa watu wa kuyumbishwa na wabunge uchwarwa hawa,hususa wa ccm maana ndiyo wengi. Na isitoshe kufanya mapinduzi ya kiuwanaharakati yanarudishwa nyuma na mapoliccm wanaotumika vibaya na wakubwa wao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom