Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
BUNGE limebaini dosari katika utungaji wa sheria ndogo nchini, ikiwamo sheria inayoweka zuio kwa Mwananchi kuwa na laini ya simu zaidi ya moja
Akiwasilisha bungeni jijini hapa jana, taarifa ya Kamati ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa katika mikutano ya 18 na 19 ya Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Ngeleja, alisema miongoni mwa dosari hizo ni sheria ndogo kwenda kinyume cha sheria mama na sheria nyingine za nchi.
Alizitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni pamoja na The Water Supply, Regulations 2019 ambayo inakwenda kinyume cha Sheria ya The Water Supply and Sanitation, 2019 na Sheria Ndogo (Ada na Ushuru) za Halmashauri za Mkinga 2019 inayokwenda kinyume cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290.
Ngeleja alisema dosari ya pili ni sheria ndogo kutozingatia misingi ya uandishi wa sheria, akiwakumbusha waandishi wa sheria kuzingatia kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria kinachowataka kuzingatia majedwali kuwa sehemu ya sheria.
Mbunge huyo wa Sengerema (CCM) aliitaja dosari ya tatu kuwa ni sheria ndogo kuwa na makosa katika majedwali kwa kurejea kanuni ambazo si sahihi au kurejea kanuni ambazo hazipo.
Alisema dosari ya nne ni sheria ndogo kutoendana na uhalisia wa mambo ukiwamo urahisi katika utekelezwji wake, hali ya uchumi wa walengwa na viwango vya adhabu na faini.
Alisema Sheria ya The Electronic and Postal Communication, Regulations 2020, imeweka masharti yasiyo na uhalisia yenye zuio la mtu kumiliki zaidi ya laini moja ya simu kutoka kampuni moja ya simu.
Vilevile, alisema wamebaini sheria ndogo kukiuka haki za binadamu, akiitolea mfano Sheria ya The Transport Licensing Act (Sura 317) ambayo mtu anaweza kufutiwa leseni bila hata kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Alisema kuwa katika mikutano hiyo miwili, kamati yao ilipitia na kuchambua sheria ndogo 2,601.