Bunge lina udhaifu mkubwa katika kuisimamia Serikali. Taifa linahitaji maombi

Habarini ndugu,jamaa,waheshmiwa na wanajf wenzangu.kheri ya mwaka mpya 2022.

Kumekua na sakata kubwa la mvutano wa mkuu wa serikali na wa aliyekua spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,sakata ambalo wengi wamelichukulia kisiasa na kishabiki tu bila ya kutazama athari na faida yake.

Kimsingi napongeza uamuzi wa spika job ndugai kujiuzuru kwani kafanya uungwana kuepusha shali na kwa maslahi mapana ya nchi.kuishauri serikali kwamba ipunguze kukopa au iwe makini na mwenendo wa ukopaji wa deni la taifa ni uzalendo mkubwa mno.pia,kufanya hivyo sio tu amefanya kitu Cha uzalendo Bali pia,ametekeleza majukumu ya bunge ya kuisimamia na kuishauri serikali.

Rais Samia anajitahidi kuusimamisha uchumi wetu,na njia moja wapo ni kwa kukopa kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.Na ndio maana kupitia mkopo wa imf wa1.3trilioni ,amefanya mambo makubwa ya kiuzalendo ya ujenzi wa shule,hospitali na vifaa tiba.pia kwa tukio hilo tu,ameongeza mzunguko wa pesa katika uchumi .tatizo lake kubwa ni mikopo mingi ya kibiashara isiyo na riba nafuu ambayo anataka kuikopa ijapokuwa tayari mikopo hiyo ni mikubwa tayari.

Kitabia rais Samia ni mtu ambaye yupo makini sana na taarifa ndogondogo,hapendi kukurupuka na smart sana.lakini shida yake kubwa hapendi kukosolewa pale ambapo anakosea.mfano halisi ni kitendo chake Cha kumfananisha mh ndugai na mtu mnafiki/anayemkwamisha katika juhudi zake.

Spika ndugai alikua mkuu wa mhimili wa bunge,hivyo anapoishauri au kuisimamia serikali kwa kukosoa na kutoa tahadhari kwa baadhi ya mambo bado anakua yuko sahihi kikatiba.rais Samia kaonyesha kwamba bunge likiwa imara basi serikali yake itafanya chochote kulidhoofidha.huu ni mwenendo mbaya sana kwa taifa.

Hiyo inapelekea rais kuonesha nguvu na mabavu kupitia chama chake na kuendelea kutoheshimu sheria na katiba.Na ndio maana nchi inahitaji maombi mengi sana ili utulivu upatikane na rais aheshimu sheria na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania
Mambo matatu ambayo yaliyomgarimu Ndugai:

1. Kulalamika kwamba shughuli za Serikali zimehamia Dar Kinyemela
2. Kulalamika kwamba hakuna haja ya kujitambulisha kila mara" Mimi ni Mwanamke" - jambo hili linaeleweka na kila mtu
3. Kulalamiakia mkopo wa 1.3 tril wakati tumeshapitisha tozo
4. Kujaribu kuaminisha umma kuwa mihimili yote judiciary, executive, na legislature ni sawa
 
Huenda tuendako mihimili yote mitatu ya Tanzania itaongozwa na kina mama na wanaume kuwa wasaidizi

Serikali - Mheshimiwa Raisi Samia S.H; Bunge Mheshimiwa Tulia A. na Mahakama .. Jaji .......
 
Habarini ndugu,jamaa,waheshmiwa na wanajf wenzangu.kheri ya mwaka mpya 2022.

Kumekua na sakata kubwa la mvutano wa mkuu wa serikali na wa aliyekua spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania,sakata ambalo wengi wamelichukulia kisiasa na kishabiki tu bila ya kutazama athari na faida yake.

Kimsingi napongeza uamuzi wa spika job ndugai kujiuzuru kwani kafanya uungwana kuepusha shali na kwa maslahi mapana ya nchi.kuishauri serikali kwamba ipunguze kukopa au iwe makini na mwenendo wa ukopaji wa deni la taifa ni uzalendo mkubwa mno.pia,kufanya hivyo sio tu amefanya kitu Cha uzalendo Bali pia,ametekeleza majukumu ya bunge ya kuisimamia na kuishauri serikali.

Rais Samia anajitahidi kuusimamisha uchumi wetu,na njia moja wapo ni kwa kukopa kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.Na ndio maana kupitia mkopo wa imf wa1.3trilioni ,amefanya mambo makubwa ya kiuzalendo ya ujenzi wa shule,hospitali na vifaa tiba.pia kwa tukio hilo tu,ameongeza mzunguko wa pesa katika uchumi .tatizo lake kubwa ni mikopo mingi ya kibiashara isiyo na riba nafuu ambayo anataka kuikopa ijapokuwa tayari mikopo hiyo ni mikubwa tayari.

Kitabia rais Samia ni mtu ambaye yupo makini sana na taarifa ndogondogo,hapendi kukurupuka na smart sana.lakini shida yake kubwa hapendi kukosolewa pale ambapo anakosea.mfano halisi ni kitendo chake Cha kumfananisha mh ndugai na mtu mnafiki/anayemkwamisha katika juhudi zake.

Spika ndugai alikua mkuu wa mhimili wa bunge,hivyo anapoishauri au kuisimamia serikali kwa kukosoa na kutoa tahadhari kwa baadhi ya mambo bado anakua yuko sahihi kikatiba.rais Samia kaonyesha kwamba bunge likiwa imara basi serikali yake itafanya chochote kulidhoofidha.huu ni mwenendo mbaya sana kwa taifa.

Hiyo inapelekea rais kuonesha nguvu na mabavu kupitia chama chake na kuendelea kutoheshimu sheria na katiba.Na ndio maana nchi inahitaji maombi mengi sana ili utulivu upatikane na rais aheshimu sheria na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania
Tz na nchi nyingine za Afrika mhimili ni mmoja tu. Mwingine ni wa jeshi la ulinzi na usalama. Nje ya hapo ni geresha tu.
 
Back
Top Bottom