Bunge limeitaka serikali kutoa taarifa kupotea kwa Mdude Nyagali

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, ameitaka Serikali kufuatilia na kutoa taarifa za kutekwa kwa kijana na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali ambaye anadaiwa kutekwa.

Mdude anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwenye ofisi yake Mbozi, mkoani Songwe juzi, Mei 4 wakiwa na silaha za moto.

Chenge ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma Jumatatu Mei 6, wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyetoa hoja ya kuahirisha Bunge kwa kutumia kanuni ya 64 kuhusu kujadili jambo la dharura.

Katika hoja yake, Msigwa alisema hivi karibuni kumekuwapo na matukio ya watu kutekwa, kupotea na hata kuuawa, huku akitolea mfano madai ya kutekwa kwa kada wa chama hicho, Mdude.

Akitoa maelezo ya hoja hiyo, Chenge ameitaka Serikali kutolea ufafanuzi jambo hilo.

“Ni kweli suala lolote linalohusu uhai wa binadamu, itakuwa vizuri Serikali itoe maelezo ili wananchi wajue hali ilivyo,” amesema Chenge.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusufu Masauni amesema Jeshi la Polisi limeanza kufanyia uchunguzi tangu, Mei 5, na wameongeza nguvu kutoka makao makuu ya jeshi hilo.

Aidha Masauni ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kuhusu utata wa tukio hilo.

Source: Kutoka bungeni.

MY TAKE:

Kwa hili Chenge mwana CCM kaonyesha ukomavu wa kisiasa, kaonyesha tofauti ya CCM asilia na CCM academia ya kina Polepole, hakupindisha maneno hongera sana.
 
Uvumilivu wa nini? Huyo anayetukana matusi machafu kwa Mh. Rais? Ni kweli serikali imemvumilia sana tu mkuu!
Ni kweli jamaa haiheshimu serikali ule si ukosoaji bali matusi endapo hizo post ni zake. Ila tuna utaratibu wa kudeal na wahalifu. Kama ni kweli hizi post ni zake huo ni ushahidi wa kutosha kumshtaki na kuhukumiwa. Apatikane kwanza halafu taratibu zifatwe.
 
Ukipewa shamba ulime, utavuna ulichopanda. Huyo Mdudu, sijui Mdude ana umuhimu kuliko marehemu Mzee Mengi? Hebu tuachane kwanza tumalize msiba!
 
Uvumilivu wa nini? Huyo anayetukana matusi machafu kwa Mh. Rais? Ni kweli serikali imemvumilia sana tu mkuu!
Hakuna sheria?? Hayo matusi kwa huyo raisi wako ni yapi?? Mahakama hazipo???

Kwa statement yako huyo raisi wako inaonesha amemteka siku si nyingi mtatafutana na I'd yako fekeche
 
Masauni awe makini sana na hili sakata la mdude, one day anaweza kuja kubebeshwa zigo, au akijichumia dhambi na kuishi kwa wasi wasi
 
Mengi ni marehemu yake yameisha hapa duniani na kifo chake sio cha kutekwa. Mdude yuko hai ila katekwa kwa amri ya watawala. Kama huna hoja kaa kimya.
Twende msibani. Umuhimu wa marehemu Mzee Mengi utaendelea kuwepo leo mpaka kesho, tena kwa miaka mingi. Huyo Mdude wenu umuhimu wake unaonekana kwa watu wachache tu waliokuwa wakimtumia. Ngoja tumalize kwanza msiba, acheni kutupigia kelele!
 
Uvumilivu wa nini? Huyo anayetukana matusi machafu kwa Mh. Rais? Ni kweli serikali imemvumilia sana tu mkuu!
Mahakama zimewekwa za nini wewe Lumumba boy km unadhani Mdude amekosea? Kwanini mtumie njia za kihuni za kuteka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom