Bunge Limehairishwa... Ni kipi cha maana kilichofanyika?

Unadhani watazifanyia nini? Wao na wengine wote linapokuwa ni suala maslahi na hasa pesa, hawana tofauti.

hebu tusubiri hizo millini 90 watazifanyia nini... kama watananunua magari ya kiheshimiwa kama ya wale green party hapo tuna haki ya kuwahukumu sio sasa hivi tunapiga bla bla.. tukiona wana magari ya kifahari tutajua nao ni walewale hawana jipya...
 
Total wastage of time and our money! Kumekuwa na tofauti gani katika maisha yetu kabla hawajakaa na baada ya kukukaa
Tumekuwa masikini zaidi baada ya kodi zetu kutumiwa ndivyo sivyo..., bora hawa mabwana wangekaa kwao na hizo pesa kutumika kununua pembejeo.., hakuna faida na hili Bunge la CCM... Ni bora waanze kutumia technology kuwasiliana sababu vikao vyao vinatutia machungu wananchi..., hakuna cha maana kinachofanyika haya yote wangeweza kuyafanya kwa SMS... kwani kumpongeza raisi mpaka na sisi tuone ??

oohh Tumefanya hiki... na Tutafanya Kile ..., while in actual sense hakuna kinachofanyika
 
Ninapatwa na uchungu hii serikali haipo kwa manufaa ya wananchi bali kulindana! katika ku-neutralize mounting pressure towards Dr. Mwinyi and Gen. Mwamunyange to resign wenye nchi hii wameamua kuahirisha bunge! Pia katika kuepuka mijadala ya mauaji ya Arusha, Dowans, Wizara ya Fedha na mengineo mengi...! wameamua kuvunja mkutano wa Bunge! Tunahitaji katiba mpya! hawa wahuni watatuendesha mpaka kufa!
 
..Wana JF pamoja na kuwa mgeni humu ndani, lakini lipo jambo/mambo ambayo binafsi yananikosesha usingizi hususan yaliyojiri katika bunge lililopita. Yamejadiliwa mengi ikiwemo hotuba ya Rais, matatizo ya Umeme, Elimu, pamoja na Afya na katika hayo yote sijaona azimio lolote la msingi lililolenga kutusaidia wananchi maskini wa Tanzania..swali langu kwa bunge hasa na Mh. Spika..
  • vikao vya Bunge ni kwa faida ya nani?
  • mbona katika mambo yote yaliyozungumza sikusikia timelines/deadline walizowekeana.
  • Baadhi ya Wabunge wa Upinzani walihoji nje ya Bunge kuhusu 90mil za mkopo kwao mbona hakuna taarifa zaidi kama huo mkopo umeanza mwaka huu tu au ulikuwa miaka yote iliyopita? nani amepokea?
My take: Tunahitaji katiba mpya haraka ili tuweze kuwawajibisha kwanza hawa tunaowachagua waeze kukidhi mahitaji yetu kwa wakati
 
..Wana JF pamoja na kuwa mgeni humu ndani, lakini lipo jambo/mambo ambayo binafsi yananikosesha usingizi hususan yaliyojiri katika bunge lililopita. Yamejadiliwa mengi ikiwemo hotuba ya Rais, matatizo ya Umeme, Elimu, pamoja na Afya na katika hayo yote sijaona azimio lolote la msingi lililolenga kutusaidia wananchi maskini wa Tanzania..swali langu kwa bunge hasa na Mh. Spika..
  • vikao vya Bunge ni kwa faida ya nani?
  • mbona katika mambo yote yaliyozungumza sikusikia timelines/deadline walizowekeana.
  • Baadhi ya Wabunge wa Upinzani walihoji nje ya Bunge kuhusu 90mil za mkopo kwao mbona hakuna taarifa zaidi kama huo mkopo umeanza mwaka huu tu au ulikuwa miaka yote iliyopita? nani amepokea?
My take: Tunahitaji katiba mpya haraka ili tuweze kuwawajibisha kwanza hawa tunaowachagua waeze kukidhi mahitaji yetu kwa wakati

Bunge haliwajibiki kwa wenye bunge (sisi wananchi) bunge limeonyesha dhahiri kwa kupitia ana makindra linawajibika kwa serikali. Nahisi wakiendelea kuwajibika kwa serikali tukawaondoe bungeni kwa nguvu ya umma, kwani serikali inatuibia, kutuua, bunge badala ya kuibana serikali bunge nalo limejiunga na serikali kutuibia
 
..Wana JF pamoja na kuwa mgeni humu ndani, lakini lipo jambo/mambo ambayo binafsi yananikosesha usingizi hususan yaliyojiri katika bunge lililopita. Yamejadiliwa mengi ikiwemo hotuba ya Rais, matatizo ya Umeme, Elimu, pamoja na Afya na katika hayo yote sijaona azimio lolote la msingi lililolenga kutusaidia wananchi maskini wa Tanzania..swali langu kwa bunge hasa na Mh. Spika..
  • vikao vya Bunge ni kwa faida ya nani?
  • mbona katika mambo yote yaliyozungumza sikusikia timelines/deadline walizowekeana.
  • Baadhi ya Wabunge wa Upinzani walihoji nje ya Bunge kuhusu 90mil za mkopo kwao mbona hakuna taarifa zaidi kama huo mkopo umeanza mwaka huu tu au ulikuwa miaka yote iliyopita? nani amepokea?
My take: Tunahitaji katiba mpya haraka ili tuweze kuwawajibisha kwanza hawa tunaowachagua waeze kukidhi mahitaji yetu kwa wakati

Bunge haliwajibiki kwa wenye bunge (sisi wananchi) bunge limeonyesha dhahiri kwa kupitia ana makindra linawajibika kwa serikali. Nahisi wakiendelea kuwajibika kwa serikali tukawaondoe bungeni kwa nguvu ya umma, kwani serikali inatuibia, kutuua, bunge badala ya kuibana serikali bunge nalo limejiunga na serikali kutuibia
 
Badala ya kulalamika tutoe mapendekezo. Tunataka Bunge letu liwe na sura ya aina gani?
 
ujue huu ni wizi wa dhahiri hakuna asiyejua sasa hata vijijiini, kiachosubiriwa ni hamasa tu kwani ni mithili ya nyumba kumwagwa petroli kinachosubiriwa ni mwenye moto kujipitisha kulipua,tumechoka kila siku afadhali jana nani tena anataka kuwa mtumwa wa mtu wakati tuliukataa wajamaa weupe walikwisha tuachia nchi yetu?
 
Sura tunayotaka ni ya kila mwenye dhamana aliyopewa a wananchi itimize,wewe kama kiongozi wa serikalijibu kinachotakiwa na sio kuonyeshana makucha nai zaidi,pia Spika anatakiwa hata kama katiokea CCM aache Uccm awe katikati kusiwe na mtoto wa mgogongi na watumboni, hapa inaonekana kuwa upizai ni kama sio sehemu ya watanzania wanaopigania haki9 yao...
 
Mkutano wa pili wa bunge la kumi umemalizika kwa vioja vingi vya hatari kubwa,Hamadi Rashid na Kafulila jinsi walivyo shirikiana na CCM kufinyanga sheria juu ya Upinzani bungeni, kilichofanyika ndicho CDM ilichokuwa inakataa kushirikiana na chama chenye ndoa na serikali,Kafulila hakumuelewa Hamadi sasa atakuwa amemuelewa,kupewa uenyekiti Mzee mapesa na Mzee wa kukamata Dhahabu airport natafsiri ni msaada kwa Serikali ya CCM.Mzee Mapesa yeye anachohitaji ni mapesa tu ku-compromise na kuficha uchafu wa serikali ni kitu rahisi sana kwake ni bora akapata mapesa,mimi simuamini kabisa huyu jamaa.Mzee wa kukamata Dhahabu airport nae anamatatizo,ana uswahiba wa kiana, yuko tayari aendelee kudumu kwa njia ya KUHURUMIWA HURUMIWA ili maisha yaende lakini asiiumbue serikali ya CCM kwa utendaji wake,Kafulila angeelewa kilichopo ndani yake baada ya CCM kuingilia hoja na kutoa maneno ya kasfa sana baada ya marekebisho kupitishwa na ninaona jinsi sasa anavyokuna kichwa na mwili kumlegea kabisa na kukosa kampani.Hamadi hana wasiwasi anakampani ya CCM.
Vile vile tumeona kuna ukuta mkubwa wa Spika kwa hoja mbalimbali zinazotaka kutoelewa na wabunge wa upinzani,juu ya utendaji wa serikali lakini spika wetu kaamua kutekeleza matakwa ya viongozi wake japo anasema yeye ni spika wa wote na bunge ni kitu kimoja, sawa kinazaria, kivitendo sio,wabunge wa CCM wamepigwa stop kubwa sana juu ya wao kuisema serikali sasa wamerudi katika ile karne 19 ya sawa boss,nasema hivi kwa kuwangalia tu wameogopa kabisa kuonyesha ushujaa wao wa karne ya 20 dalili ya mvua ni mawingu.Upinzani bungeni ni pamoja na kuibua hoja mbalimbali ambazo bunge lingejadili na kufikia maamuzi ambayo ni ya msingi kwa watanzania na maendeleo yake.mwisho maamuzi yangepelekwa serikalini kwa utekelezaji.Spika asione ni dhambi kukubali hoja za wapinzani kwani ndio mahala ambapo watanzania wamechagua pakusemea,kuongeza wapinzani bungeni ni kuongeza sauti nyingi kwa serikali juu ya utendaji wake.Je spika anavyokataa hizo hoja anataka nini haoni kuwa anazidi kuingamiza CCM 2015.Ajue msukumo wa watanzania kupeleka wawakilishi wengi ndio njia bora zaidi kuliko kuwaacha CCM peke yao na kuanza kuandamana kama Misri na Tunisia?kitendo cha watanzania kupeleka wawakilishi wengi ni njia mbadala wa angalau kupunguza dhuluma ya haki zao,Spika kumbuka huku mtaani mambo sio mazuri,kunatatizo, youth boom +shaky economy =explosive unrest,vijana hawapati elimu nzuri,huduma nzuri za afya na hakuna kazi(watoto wa wakulima na masikini) na ndio wengi,lakini wao wanaona watoto wa wakubwa serikalini na chama wanapata elimu nzuri(mikopo ya elimu pia),huduma nzuri za afya na kazi kubwa kubwa maana wanaonekana na kusikika katika vyombo vya habari na kadharika.Tena wanaanza kuchukua nafasi za baba zao katika uongozi wa nchi hii, hii ni mbaya sana vijana (watoto wa masikini na wakulima )wakilipuka hawatazuilika hata kidogo.Ni bora spika akaangalia ni namna gani anaweza kutumia bunge na wabunge wake kurekebisha hali halisa ya Tanzania maana bunge ndio linalosimamia utendaji kazi wa serikali na pale mjengoni ndio mahala pake pa kuibua mijadala ya hoja mbalimbali.Spika kumbuka watanzania wa sasa sio wale wa wakati wa uhuru, dunia iko wazi,hivyo wanajua mengi ikiwa ni mabaya na mazuri yanayofanywa na serikali maana yake watanzania wamekuwa weledi wa mambo,ukifanyakazi ya kuilinda serikali ya chama chako kama unavyofanya ni hatari sana,watanzania wanatafsiri wewe ulipendekezwa kwa kazi maalumu ambayo umeonekana kuifanya.
BORA KINGA KULIKO TIBA,
 
Wakati naendelea kusikia hoja mbalimbali za Wabunge,kuna neno wanatumia Wabunge kwamba Mheshimiwa Spika na Bunge lako Tukufu.Sasa hoja inakuja kwamba Utukufu wa Bunge nini? Wakati Bunge Limejaa maovu yanayolalamikiwa kila kukicha yakiwemo,DOWANS,RICHMOND,KAGODA,MEREMETA,MAUAJI YA ARUSHA,MABOMU YA MBAGALA NA GONGO LA MBOTO,MASUALA YA RADA,BODI YA MIKOPO,hapo naomba nifanye hoouuuuuf,je Utukufu wa bunge uko wapi
 
Serikali imeanza kufurahia matunda ya semina elekezi waliyofanyiwa wabunge wa ccm chini ya wenyekiti wa chama chao; katika semina hiyo wabunge wa ccm ikiwa ni pamoja na spika walipewa jukumu la kulinda kwa hali na mali serikali yao, hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamekiuka matakwa ya katiba yanayowataka wabunge hao pamoja na mambo mengine kusimamia utendaji wa serikali.
 
Bunge letu limejaa,mafisadi manyangau. wanyanganyi wa rasilimali zetu na wapambe wao.Mungu awasaidie wabunge wenye kujua wajibu wao kwa wananchi.kwani wengine wanawajibika kwa mafisadi.Heshima ya Bunge letu haipo tena.UTUKUFU ANASTAHILI MUNGU.
 
Hii inatoka Tahariri ya Tanzania Daima ya tar 20.02.2011

TUMEFUATILIA kwa makini mwenendo wa Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Ijumaa na tumesikitishwa jinsi chombo hicho cha kuwawakilisha wananchi kilivyoshindwa kuutumia vizuri muda wake katika kuwatumikia wananchi.

Mkutano huo wa Bunge ulifanyika wakati taifa likiwa linakabiliwa na matatizo na madai mbalimbali kama tatizo mgawo wa umeme, suala la fidia ya Dowans, kupanda kwa gharama za maisha (nauli za daladala na mabasi kupanda, bei za vyakula, mafuta, gesi na nishati yenyewe ya umeme kuwa juu), tatizo la mikopo ya vyuo vya elimu ya juu kutopatiwa ufumbuzi na madai ya katiba mpya, bila kusahau janga la kitaifa la milipuko ya mabomu iliyotokea Mbagala na hivi juzi Gongo la Mboto.

Sisi tunaamini kama Bunge lingejipanga vizuri katika kutimiza wajibu wake wa kuwawakilisha wananchi, masuala hayo ndiyo yaliyopaswa kujadiliwa kwa masilahi ya wananchi kwa kipindi hiki, kama si masuala yote basi angalau machache katika hayo tuliyoorodhesha yalipaswa kujadiliwa na kutolewa maamuzi ya kiutekelezaji ili kunusuru wananchi.

Hata hivyo, kinyume na matarajio ya wengi, taifa lilishuhudia Spika mpya wa Bunge, Anne Makinda, akizima mijadala nyeti ya Bunge kuhusiana na masuala hayo hata pale ilipoibuliwa na wabunge kwa masilahi ya taifa.

Mathalani, Bunge lilizuia hoja binafsi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, ambayo ilikusudiwa ipendekeze Bunge kujadili na kutoa mwongozo wa mchakato ambao utafanikisha kupatikana kwa katiba mpya lakini kwa masikitiko ya wengi hoja hiyo ilizuiwa kuwasilishwa kwa madai kuwa serikali italeta muswada wake kuhusu suala hilo bungeni.

Katika hilo tunaona kuwa mbunge huyo hakutendewa haki na kusudio la hoja yake ambalo linagusa matakwa ya umma pia halikutendewa haki kwani kinachokusudiwa kuletwa na serikali katika muswada wake wa katiba kwa mujibu wa taarifa yao bungeni ni muswada utakaohusu uanzishwaji wa tume ya kuratibu mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambayo itatokana na kurekebishwa kwa hii ya sasa na si kuandikwa upya kwa katiba kama hoja ya Mnyika na wananchi wengi wanavyotaka.

Ikumbukwe kuwa aina ya tume inayokusudiwa kuundwa na rais ilishawahi kuundwa huko nyuma na kuongozwa na Jaji Francis Nyalali, lakini kwa kuwa tume hiyo iliundwa na serikali na ilipaswa kuwajibika kwa serikali, mapendekezo yake mengi ya kimsingi likiwemo pendekezo la Katiba, yalitupiliwa mbali.

Tunasisitiza haikuwa haki kwa Bunge kukataa hoja maana kinachotaka kuletwa bungeni na serikali kupitia muswada wake huo ndicho kinachopingwa na kusudio la hoja ya Mnyika, kwa maneno mengine kuzuiwa kwa hoja hiyo kulilenga kumzuia mbunge kupinga mwenendo wa serikali katika kushughulikia suala hilo la katiba.

Haikuwa halali pia kwa Bunge chini ya spika huyo kukataa hoja ya mgawo wa umeme usijadiliwe bungeni kama suala la dharura kwani pamoja na kuwepo kamati ambayo analifanyia utafiti na kulitafutia ufumbuzi suala hilo bado mjadala wa dharura ulikuwa ni muhimu katika kutoa mwongozo wa kina kwa kamati hiyo.

Haikuwa halali pia kwa Bunge kuzuia hoja nyingine ya dharura iliyotolewa na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyetaka tatizo la milipuko ya mabomu lijadiliwe, kwani pamoja na kuundwa kwa tume inayolichunguza suala hilo bado mjadala wa dharura ulihitajika ili kutoa mwelekeo na hadidu rejea kuhusu majukumu ya tume hiyo.

Haikuwa halali pia kwa Spika kuongozwa na jazba na upendeleo kwa chama chake cha siasa (CCM) badala ya misingi ya kanuni aliyosisitiza kuifuata katika kuendesha vikao, mfano mzuri ni pale alipoombwa muongozo na mbunge wa Arusha Mjini kuhusu hatua za kuchukua ikiwa kiongozi mkubwa serikalini kama waziri mkuu amelidanganya bunge; badala ya kutoa mwongozo alioombwa yeye alipandwa na jazba na kumtaka mbunge huyo alete maelezo kwa kumwita waziri mkuu muongo lakini hata mbunge huyo alipokuwa tayari kutoa maelezo yake bungeni Makinda alimkataza asiyatoe kwa mdomo –ayatoe kwa maandishi maamuzi ambayo yalionekana dhahiri kulenga kumuokoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Kwa ujumla, mwenendo wa Spika Anne Makinda katika kuendesha mkutano huo hususani alipoliongoza Bunge kubadilisha kanuni kwa kisingizio cha “kuweka tafsiri ya neno kambi rasmi” haukuwa mzuri kwani ulionekana kutawaliwa zaidi na upendeleo wa kisiasa kwa manufaa ya chama chake (CCM) kuliko matakwa na masilahi ya wananchi​
 
Back
Top Bottom