Bunge Limehairishwa... Ni kipi cha maana kilichofanyika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge Limehairishwa... Ni kipi cha maana kilichofanyika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WildCard, Feb 18, 2011.

 1. W

  WildCard JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  -Anawashukuru wamechangia posho ya siku moja kwa wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto.
  -Anasema wamekufa 20 kutokana na mabomu hayo hadi jana jioni

  ==============
  Hotuba kamili ya Waziri mkuu ni hii hapa chini
  ==============

  HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WAKATI WA KUAHIRISHA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DODOMA – TAREHE 18 FEBRUARI 2011

  UTANGULIZI

  Mheshimiwa Spika,

  Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema kwa kutupa uhai hadi leo na kutuwezesha kuhitimisha Mkutano huu wa pili salama.

  Mheshimiwa Spika,
  Kama nilivyotoa Taarifa jana, Taifa letu liko kwenye majonzi na masikitiko makubwa kufuatia Maafa yaliyosababishwa na milipuko ya Mabomu kwenye Maghala ya Kambi la Jeshi eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana hadi jana jioni zinaonyesha kuwa, jumla ya Watu waliopoteza maisha ni 20, Majeruhini 315, na ambao bado wamelazwa hospitalini ni 135. Mbali na Maafa ya Vifo na Majeruhi, milipuko hiyo imesababisha hasara kubwa ya mali kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Mheshimiwa Rais jana tarehe 17 Februari 2011, alitembelea eneo la maafa na kujionea uharibifu mkubwa uliotokea. Baada ya kutembelea eneo hilo, Mheshimiwa Rais aliitisha Kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Taifa ili kutathmini hasara iliyotokea na kubainisha njia za haraka za kuchukuliwa ili kuwasaidia Wananchi wote walioathirika na Maafa hayo. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais, tunaomba Wananchi wote wawe watulivu na warejee kwenye maeneo yao wakati Serikali inashughulikia tatizo hilo. Maafa haya yamesababisha mihangaiko miongoni mwa Watanzania. Maafa haya ni yetu sote Watanzania. Waliopoteza maisha na mali zao ni Ndugu zetu. Hivyo, nawaomba Watanzania wote ndani na nje ya Nchi popote walipo na Washirika wetu wa maendeleo kuisaidia Serikali kukabiliana na tatizo hili. Nawasihi tushirikiane kuwafariji Waathirika kwa kuwapa misaada mbalimbali ya hali na mali ili waweze kurudia maisha yao ya kawaida mapema iwezekanavyo. Napenda kwa mara nyingine tena, kuwapa Pole wote waliokumbwa na maafa haya. Kwa majeruhi wote, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie nafuu na kupona haraka na kwa wale waliopoteza maisha, tuungane sote kumlilia Mwenyezi Mungu ili azipokee roho zao peponi na kuzilaza Mahala Pema. Amina.

  Mheshimiwa Spika,
  Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge lako Tukufu ambao ulianza tarehe 8 Februari 2011. Mkutano huu ndio Mkutano wa Kwanza wa Kazi wa Bunge hili baada ya kukamilisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu ambao ndio umetupatia kibali cha kuwa Wabunge wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, Mkutano huu umefanyika baada ya Semina Elekezi kuhusu Wajibu wetu kama Wabunge iliyofanyika Dar es Salaam kwa muda wa siku kumi na kufungwa tarehe 3 Februari 2011.Wote tuliobahatika kuhudhuria Semina ile, tunakubaliana kwamba Semina Elekezi ilitujengea uelewa mpana wa masuala ya utendaji, yakiwemo masuala yanayogusa Mihimili mitatu, yaani Mahakama, Bunge na Serikali.

  Napenda nitumie fursa hii, kwanza, kuishukuru tena Ofisi yako Mheshimiwa Spika kwa kuandaa Semina hiyo. Pili, kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote ambao walishiriki kikamilifu kwa muda wote. Ni dhahiri kwamba, Semina ile imekuwa chachu katika kujipanga kutekeleza majukumu yetu kama Wabunge. Tumepewa fursa, tumejua wajibu wetu, tumebaini changamoto na tumeweka mikakati ya kuzikabili changamoto hizo. Kilichobaki sasa ni kufanya kazi kwa misingi ya maelekezo tuliyoyapata kwa bidii zaidi ili kuongeza tija na ufanisi katika kuwatumikia Wananchi waliotuchagua.

  Hoja ya Rais

  Mheshimiwa Spika,
  Katika Mkutano huu, Agenda iliyochukua nafasi kubwa ni Hoja ya Serikali ya kujadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais. Hoja hiyo tumeihitimisha vizuri na kwa mafanikio makubwa. Napenda kuwapongeza tena Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki katika mjadala wa hotuba hiyo vizuri.

  Chaguzi Mbalimbali

  Vilevile, katika Mkutano huu, tumeweza kufanya Chaguzi za Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge. Vilevile, tulifanya chaguzi za Wajumbe wa kutuwakilisha katika Kamati na Taasisi mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa. Kwa vile orodha ni ndefu, napenda nitumie nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa na kwa ujumla wao wote waliogombea nafasi hizo na kushinda. Ni matarajio yangu kwamba tutatumia nafasi hizo vizuri katika kuleta ushirikiano, mshikamano na kufanya kazi kwa pamoja kama Wawakilishi wa Wananchi wa Tanzania na kutekeleza majukumu yetu kama Wabunge ndani ya Bunge hili.

  Maswali

  Mheshimiwa Spika,
  Katika Mkutano huu wa Pili wa Bunge jumla ya Maswali 95 ya Msingi na Maswali 187 ya Nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge. Vilevile, utaratibu wa Maswali kwa Waziri Mkuu kila Alhamisi uliendelea kwa Waheshimiwa Wabunge kuuliza Maswali 54 ya Nyongeza. ya Msingi na

  Miswada

  Mheshimiwa Spika,
  Katika Mkutano huu pia Miswada ya Serikali ifuatayo ilisomwa kwa mara ya kwanza:
  i) Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma wa Mwaka 2010 [The Public Procurement Bill, 2010];

  ii) Muswada wa Sheria ya Famasia wa Mwaka 2010 [The Pharmacy Bill, 2010];

  iii) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2011 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2011]; na

  iv) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Maeneo ya Maendeleo ya Kiuchumi wa Mwaka 2011 [The Economic Zones Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2011].

  Kauli za Serikali

  Mheshimiwa Spika,
  Bunge lako Tukufu lilipokea Kauli ya Serikali kuhusu Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, inayohusu Kuanzisha Mchakato wa Kuitazama Upya Katiba ya Nchi kwa Lengo la Kuihuisha ili Kuendana na Mabadiliko na Matakwa na Hali ya Sasa na Baadaye. Aidha, Bunge lako Tukufu lilipokea Kauli za Serikali Kuhusu Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini; na ile ya Hali ya Umeme Nchini na Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Katika Kipindi Kifupi na cha Kati.

  Kuhitimisha Mjadala wa Hotuba ya Rais

  Mheshimiwa Spika,
  Siku mbili zilizopita, tarehe 15 Februari 2011, nilisimama hapa kutoa maelezo na ufafanuzi wa hoja na masuala mbalimbali yaliyotokana na majadiliano ya Hotuba ya Mheshimiwa Rais ya kuzindua Bunge la Kumi. Kwenye maelezo yangu, nilizungumzia mambo mbalimbali yakiwemo marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, Masuala ya Muungano, Umoja wa Kitaifa, Sekta za Kijamii, hali ya Uchumi na Migomo na Maandamano kwenye Vyuo Vikuu.

  Kabla ya kutoa maelezo na ufafanuzi wangu, nilitanguliwa na Mawaziri Tisa waliojibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kwenye Sekta zao. Aidha, kabla ya Waheshimiwa Mawaziri kujibu hoja hizo, Serikali ilikuwa imeshatoa Kauli kwenye Masuala ya Kurekebisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maji na Nishati. Ninaamini, kwa maoni yangu, maelezo na ufafanuzi wangu, Kauli za Serikali na majibu ya Waheshimiwa Mawaziri, yalionesha dhahiri wapi tunatoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Safari bado ni ndefu, lakini kwa kushirikiana na kuweka Itikadi zetu za Kisiasa pembeni na kutanguliza mbele mahitaji na matatizo ya waliotuchagua na kutuleta ndani ya Jengo hili tutafika, tena tutafika salama.

  HALI YA CHAKULA

  Mheshimiwa Spika,
  Kabla ya kuhitimisha maelezo yangu napenda kuwaeleza Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwamba, hali ya Chakula imeendelea kuwa nzuri katika maeneo mengi Nchini kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 kufuatia mavuno mazuri ya mwaka 2009/2010. Tathmini iliyofanyika mwezi Desemba 2010 ilionesha kwamba uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa 2009/2010 ulifikia Tani Milioni 12.3 zikiwemo Tani Milioni 7.4 za mazao ya nafaka na Tani Milioni 4.9 za mazao yasiyo nafaka. Mahitaji ya Chakula kwa mwaka 2010/2011 ni Tani Milioni 11.1 hivyo uzalishaji huu utatosheleza mahitaji ya Chakula kwa Asilimia 111, sawa na ziada ya takriban Tani Milioni 1.2. Baadhi ya maeneo ya Nchi yalipata mavuno ya ziada na mengine kujitosheleza. Kufuatia hali hiyo, upatikanaji wa Chakula katika maeneo mengi ya Nchi, hususan katika Masoko ya Vijijini na Mijini bado umekuwa ni wa kuridhisha.

  Hadi tarehe 14 Februari 2011, Akiba ya Chakula katika Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ilikuwa jumla ya Tani 216,030.653 za mahindi ambazo ziko katika Kanda mbalimbali za Hifadhi ya Chakula ya Taifa. Aidha, kiasi cha Tani 176,083 ya mazao ya nafaka zilikuwa kwa Wafanyabiashara Binafsi.

  Hata hivyo, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu yako baadhi ya maeneo ambayo yameonesha dalili ya kuwa na upungufu wa chakula kati ya mwezi Januari na mwezi Machi 2011. Maeneo hayo ni yale yanayopata mvua za vuli na ambako mvua hizo hazikunyesha vizuri. Tayari Serikali imeanza kuchukua hatua kwa kutenga jumla ya Tani 13,760 za Chakula kutoka Hifadhi ya Taifa kwa ajili ya Watu 423,530 ambao wameainishwa kwamba wanakabiliwa na Upungufu wa Chakula.

  Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Wananchi wote kutumia chakula kilichopo kwa uangalifu kama njia mojawapo ya kujihami na Janga la Njaa linaloweza kutokea. Aidha, kila mmoja wetu anao wajibu wa kuchukua tahadhari mapema. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, tunaporudi Majimboni mwetu tutumie muda huo kuwaasa Wananchi, hasa wale wenye mavuno machache umuhimu wa kutunza chakula. Vilevile, Wakulima wahimizwe kutumia mvua zinazonyesha kupanda mazao yanayoendana na hali ya hewa ya maeneo yao.

  HITIMISHO

  Mheshimiwa Spika,
  Katika muda mfupi tuliokaa pamoja hapa Bungeni, nimegundua kuwa tuna Waheshimiwa Wabunge mahiri waliobobea katika nyanja mbalimbali. Wapo wasomi wa ngazi zote – Wazee kwa Vijana ambao wana uzoefu na Utaalam mkubwa. Ni imani yangu kuwa tutatumia Utaalam, Umahiri na Uwezo wetu mkubwa tulionao katika kuijenga Nchi yetu na kuwasaidia Watanzania kutoka hapa tulipo hadi hatua ya mbele katika kuleta maendeleo ya Nchi yetu. Wananchi waliotuchagua wanatutegemea. Nawaomba tutangulize Uzalendo katika kila jambo tufanyalo kwa manufaa ya Taifa letu na Watu wake, badala ya ushabiki wa Kisiasa.

  Mheshimiwa Spika,
  Napenda kuhitimisha Hotuba yangu kwa kurejea tena kusema kwamba, baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu kwa mafanikio makubwa, kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kuijenga Nchi yetu kwa Umoja na Mshikamano mkubwa. Nawaomba tuweke maslahi ya Watanzania na Taifa mbele. Tudumishe Amani na Utulivu. Tupuuze Sera zozote za kudhoofisha Utaifa wetu kama Watanzania na kutugawa kwa misingi yoyote ile, iwe ya Kikabila, Imani za Dini, Rangi au kwa Itikadi za Kisiasa. Dhamira yetu sote iwe ni kukuza uchumi wa Nchi yetu na kuondoa umaskini ili kuwaletea Wananchi wetu maendeleo na maisha mazuri. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua mbele. Tufanye kazi kwa bidii, juhudi, maarifa na ubunifu zaidi. Mimi naamini kuwa kwa ushirikiano wa Bunge hili na Wananchi kwa ujumla tutaweza kutimiza matarajio ya Wananchi waliotuchagua na matarajio ya Watanzania wote.

  Mheshimiwa Spika,
  Mwisho niwashukuru wote waliofanikisha Mkutano huu wa Pili wa Bunge. Shukrani za pekee ni kwako wewe Mheshimiwa Spika kwa kudhihirisha kwamba una uwezo mkubwa wa kutuongoza ndani ya Bunge hili. Ni dhahiri umeanza vizuri, tunakupongeza! Nimshukuru vilevile, Naibu Spika kwa umahiri wake wakati wa kuongoza Vikao vya Bunge hili. Niwashukuru pia Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu ambayo japo kwa wengine ilikuwa mara ya kwanza kuchangia hapa Bungeni, wote mmeonekana Wazoefu wa siku nyingi katika kuchangia hoja zilizowasilishwa kwenye Mkutano huu. Namshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilillah na Wasaidizi wake kwa huduma mbalimbali ambazo zilifanikisha Mkutano huu. Nawashukuru Watumishi wa Serikali, Taasisi mbalimbali na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari kwa kutoa taarifa za mambo yote yaliyojadiliwa katika Mkutano huu kwa wakati. Wote kwa ujumla wao nawashukuru sana!

  Mheshimiwa Spika,
  Baada ya kusema hayo, nawatakia wote safari njema. Naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liahirishwe hadi siku ya Jumanne tarehe 5 Aprili, 2011 Saa Tatu Asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa Tatu hapa Mjini Dodoma.

  Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  HIvi kwa nini huyu jamaa asijiuzulu??
   
 3. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  bunge la safari hii halikuwa na jipya bara limeisha lilikuwa linaleta kichefu chefu kama mjamzito ukilisikilioza mimba inaweza ikatoka
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hoja ya Lema haipo tena.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bao la kisigino


  Asnte Pinda:clap2::clap2:
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watakutana tena tarehe 5.4.2011. Bunge la hovyo kabisa tangu uhuru?
   
 7. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Kodi zetu hizoo
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Spika naye anafoka sasa. Anawaambia wabunge wasisemeseme hovyo nje.
   
 9. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ati nini? wawe na adabu sio?
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  whaaaaaaiiiiiiiiii
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wasiseme seme nini mkuu
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  No wonder bado ni ''miss'' at that age...mume gani atataka kufokewa
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hoja zao zote wazisemee ndani ya Bunge. Hata kama ni hasira wazimalizie ndani ya Bunge.
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wasiseme kuwa Milipuko ya Mabomu Katika Basement Store Depot - Gongo la Mboto ni UZEMBE wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi!!
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ha .... huyu mama anauchizi .... yaani amekataa wasizungumzie bungeni sasa anataka wakae kimya ..kwanza mamlaka hiyo anayo .... anyways miaka minne iliyobaki ni kidogo sana
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  bunge kimeo kabisa - halina mvuno na huyu mama ndiyo kalifanya liwe zezeta - Hongera hoja ya Mnyika kuhusu Umeme, Lissu kuhusu Mabomu pamoja na Therathini.

  Hongera pia Lema, wewe ni mshindi umemwangusha Spika na Waziri mkuu kwa Hoja, Hongera Mbowe kwa Hotuba yako kama mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani. Tunawapa tano wapiganaji wetu na msijali kama hoja wakiziweka kapuni sisi wananchi tunaelewa kwani serikali ni yao, bunge wamelifanya kikao cha CCM wakitumia wingi wao kama kigezo, mahakama pia ni zao - tutapigana tu mpaka kieleweke.

  pamoja na kuiteka hoja ya katiba sisi tunajua haikuwa priority yao ila wameona wairukie kwani wamezoea kudandia hoja nyingi tu zetu, mnyika usife moyo.

  Kama mtu anasema suala la abomu si dharura basi mfikirie mara tatu na si mbara mbili - huyu mtu ni wa kuogopa - ni adui wa usalama wa nchi.


  Mapambano bado yanaendelea. Alutaaa.........
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  yaani lisu na wenzake waitishe press conference ..waeleze jinsi walivyonyimwa na spika fursa ya kujadili janga la milipuko ya mabomu bungeni
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu mama analiendesha Bunge hili kama la chama kimoja. Katiba yetu ya JMT haisemi ni nini la kufanya unapokuwa na Spika mbovu kama huyu.
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kazi ya wabunge toka ccm ni nini ndani ya bunge?wapo pale kusubiri posho tuu na dharura waibe basi
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jana waliaarisha...kwa sababu ta Gongo L M ...Shame!!

  ..Leo wanairisha...

  Hayo matukio yamekaa vipi?

  That means ...

  Kwa nini hawakuairisha jana...?
   
Loading...