BUNGE limechagua kiingereza... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BUNGE limechagua kiingereza...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Apr 18, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,733
  Likes Received: 5,100
  Trophy Points: 280
  Kila aliyenyooosha kiingereza kwenye uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki jana alichaguliwa.Wabunge wakiongozwa na Spika walihama kwenye hoja na kuhamia kwenye kiingereza.Imedhihirika jana.Waliojikwaa kwenye lugha hii,wamejikwaa pia kwenye kura. Wamedhalilishwa.Ni kweli kigezo pekee ni kujua kiingereza? Wangapi walikuwa Bunge hilo wakijua kiingereza lakini hawakufanya chochote?

  Ni muda wa kubadilika.Ni muda wa kusema hata Kiswahili chapaswa kutumiwa. Tukisimamie Kiswahili chetu popote.Tutaeleweka na kutetea maslahi yetu vyema.Kiingereza si lugha yetu jamani..

  Mzee Tupatupa
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,667
  Likes Received: 2,734
  Trophy Points: 280
  na huyo bibi mkubwa kiingilishi kinapanda kweli.
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,733
  Likes Received: 5,100
  Trophy Points: 280
  Hana lolote,mikwaruzo kibao.
   
 4. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mmh kama ni kidhungu tu ata MC wa mpambano bibi kiroboto nae alikwama yani pamoja na exposure yote aliyonayo ndo kizungu chake kile.
   
 5. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ma dia membas of paliament zey!! zey!! Bunge la Afrika mashariki zey want kiinglish.
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,907
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Kilengesa ni hataree arifu ugonjwa wa taifa huu bora hata interview makazini ziwe za kiswahili.
   
 7. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Ina maana hata Baharia wetu hajui kidhungu???
   
 8. B

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,216
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tupende tusipende kwa Tanzania Kiingereza kinaleta hadhi. Ukiongea Kiingereza kizuri basi utaonekana wewe ni "kichwa", utaonekana umesoma na kustaarabika, n.k.

  Na ukiongea Kiingereza kibaya basi utaonekana hamnazo, hujasoma, hujastaarabika, na mambo mengine kama hayo.

  Si sahihi kabisa ila hivyo ni ndivyo ilivyo.
   
 9. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,119
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo sana haka kalugha kanachanganya kidogo.
   
 10. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,710
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Wivu tu watanganyika!
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 4,949
  Likes Received: 813
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tunapaswa kukipenda Kiswahili lakini tuna vikwazo vingi.Uchumi wetu bado mchanga,tunategemea bidhaa nyingi kutoka nje sababu viwanda vyetu vilishauzwa/kubinafsishwa siku nyingi.Mfano Mdogo simu/kompyuta uliyoitumia kuwafikishia watu hii habari maelekezo yake yapo kwa kiswahili?isitoshe Bunge la EA haliendeshwi kwa Kiswahili ktk jambo lolote.Mikataba inayoingiwa na viongozi wetu Wa kiserikali imeandaliwa kwa kiingereza sbb ya utegemezi(wawekezaji)tunaoutaka kutoka nje.Kiswahili tunakipenda lakini asilimia kubwa ya wananchi Wa Tanzania hawajui kuzungumza Kiswahili fasaha.
   
 12. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi niliskia Kiswahili ndio lugha ya EA sasa hii habari ya kuwapima kwenye ki English ilitoka wapi?
   
 13. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Umesema kweli. Nguvi wa thiongo aliwahi kusema, "Si vizuri lugha moja ikakua katika kaburi la lugha nyingine," kwani lugha inapokufa kila kitu katika lugha ile kinakufa. Yaani namna ya kufikiri, ugunduzi, falsafa, mtazamo nk. Hapa kwetu Kiingereza kinataka kukua katika kaburi la Kiswahili. Kimsingi tunapoteza fedha na mda kujifunza Kiingereza. Nimewahi kufanya utafiti nikagundua kwamba tunahitaji 1% ya uwekezaji kama taifa katika lugha ya Kiingereza. Yaani kwa ajili ya watu watakaofanya kazi ya mipakani, uhamiaji, viwanja vya ndege na wageni wa ikulu. Mashuleni tufundishe Kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Hii itasaidia sana kutengeneza utamaduni wetu pia tutakuwa na siri za taifa na namna ya kuwasiliana kama watu wa familia moja.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kiingereza ndio lugha rasmi ya Jumuiya. Kinachonishangaza ni kuwa kwa nini wawakilishi watu hadi leo hawajapambana kuhakikisha kuwa Kiswahili ndiyo inakuwa lugha rasmi ya jumuiya.
   
 15. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi nilifikiri kwamba kwa vile watz wengi tunaongea Kiswahili na wakati mwingine lugha za makabila.Nilijua kwamba wagombea wote watawapeleka kozi ya kuongea Kiingereza kwanza halafu waombe kura kwenye bunge baada ya kufuzu Inglishi kozi.Ningekuwa mimi ningeomba mwongozo kwa spika ili niongee kiswahili.
   
 16. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2017
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,733
  Likes Received: 5,100
  Trophy Points: 280
  Filamu hii yaweza kujirudia mwaka huu

  Mzee Tupatupa
   
Loading...