Mzee Msemakweli
Senior Member
- Oct 12, 2010
- 159
- 34
Jamani nchi hii sasa ina ombwe la uongozi limezidi mipaka. Priority katika mambo ya msingi hakuna tena. Tunapo ambiwa suala la madaktari liko mahakamani nani asiyejua utendaji wa shughuli za mahakama unavyo chukua muda kufikia hukumu zake? Serikali kwa sababu haina nia ya kutatua mgogoro huu waliamua kulikimbizia mahakamani wakijua fika mahakama haiwezi kushurutishwa kutenda shughuli zake na hivyo kupunguza nguvu ya mgomo.
Hivyo basi naomba wananchi wote, vyama vya siasa, wanaharakati wa haki za binadamu, dini zilizo na uchungu na nchi hii zisizo tumiwa na wanasiasa tuipe serikali siku chache kama siyo masaa serikali kutatua mgogoro huu ama sivyo tuiwajibishe. Upole wetu unatuponza, wanautumia kutufanya wanavyotaka kama mafisadi wanavyomtumia DHAIFU kufanya wanavyotaka.
Haya ndo matatizo ya kuongozwa na Serikali ya kishikaji na dhaifu. Hakuna uwajibikaji zaidi ya kuitafuna Nchi yetu. Kuwaondoa ndo ufumbuzi ni kuwaondoa kwa mfumo wanaoutumia wenzetu wa Syria. Kinyume ya hapo hawawezi kuondoka madarakani.