Bunge limeahirishwa kutoka na ajali ya Mv Skagit

Hizi ni habari za kweli meli ni ya abiria na mizigo na inauwezo wa kubeba watu 250. Tumwombe Mungu ili watu waokolewe kwa usalama.
 
ccm wanatoa kafara hapo
Sasa kati ya CCM na CHADEMA nani wana operation Sangara. Na sangara tunajua ni samaki kama usemayo ni kweli basi sisi Chadema tunatumia njia ya maji kuwafanya wananchi wawe chakula cha wanyama waishio majini. Acha kutuhaibisha wenzako bwana Episodes
 
Wadau kuna yeyete mwenyetaarifa za chanzo halisi cha ajali hiyo na je nini kinaendelea mpaka sasa!

Tunawapa pole sana wale wote waliofika na ajali na wale wote waliopoteza wapendwa wao.
 
Uongozi dhaifu hakuna wakaguzi kabla chombo hakiondoka kazi ya ccm hiyo .

Jamani Kabla ya kulaumu pande yoyote tujaribu kuwa na habari kamili. Kwenye weather forecast wametoa angalizo la strong winds for three consecutive days starting today, na watu pia wameshauriwa kukaa mbali na fukwe
 
Jamani naangalia TBC1 sasa hivi baadhi ya watu wamefika bandarini Dar iLife kujua idadi ya abiria, Imagine hata ofisi hawana hao wenye meli sasa abiria sijui walikuwa wanakatia ticket wapi.
 
Hivi hata aibu hawana na nchimbi anaongea kinafiki kweli kweli, mbaya zaidi hoja ya Rashidi wameijata, walivyotoka nje wameijata kuna nini?
 
eeeh kweli hata mie tbccm wamenipotosha mie nikadhani bi kiroboto amekubali hoja ya nchimbi kuhairisha bunge kutokana na kuzama kwa meli kumbe alishaikataa hoja hiyo baada ya kutolewa na Rashidi?aisee
 
Hadi aibu,bunge walionyesha wenyewe Live, kwenye habari wamekwepa kabisa kuonyesha kipande cha mama akichemka.
 
Bado mnatazama TV ya chama chenye rangi kama ya haya maandishi??? ungetazama ITV mwanzo mwisho wameonesha ukweli wa hoja ya Mohaed Rashid....hao ccm hawana kitu...
 
jaman haya mamlaka ya udhibiti mji mbona wanajisahau hivyo au wanataka zanzabar pia twende kwa gari maana kila siku meli zinazama sababu ni uchakavu na wingi wa abilia jaman watanzania tutaisha
 
Uzuri ni kwamba siku hizi habari hazitolewi na chombo kimoja kama enzi za chama kushika hatamu,wakidanganya,upande wa pili unatoa ukweli.Bado itaendelea kula kwa magamba mpaka wamrudie Mungu maana haya wanayotufanyia hayampendezi Mungu kabisa.
 
Wanakula tu PAYE zetu halafu wanapendelea habari za CCM, ipo siku tutagawana hiyo mitambo kila mtu atajua auze km scrapper au vipi ili arudishe PAYE yake
 
kwani uongo,chanzo cha bunge kuahirishwa ni kuzama kwa meli,nikuulize singezama bunge lingeahirishwa ?
 
Tbc ilikuwa ni ya kipindi cha Tido Mhando, lakin ya sa hiv haina tofaut na gazeti la uhuru.
 
Back
Top Bottom