Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,269
- 33,872
Kila sakata linaloibuliwa na Rais Magufuli linaacha maswali nyuma kama kweli Bunge letu limekuwa linatimiza wajibu wake sawa sawa kama ulivyotajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Ibara ya 63 kifungu kidogo cha Pili.
Hivi kweli kama Bunge letu lingekuwa linaisimamia serikali kisawasawa kama inavyotakiwa haya mambo ya Airtel yangekuwepo kweli? Ama tuseme waliokuwa wanafaidika na madudu haya yanayoibuliwa sasa ndiyo wenye ushawishi ndani ya Bunge letu?
Ukiangalia mikataba ambayo imekuwa inalalamikiwa na watanzania mingi yake sheria zake zilitungwa bungeni na wabunge walizipitisha kwa nderemo kubwa sana. Inakuwaje ni serikali yenyewe imekuwa inajifanyia upekuzi badala ya upekuzi huo kufanywa na bunge?
Hivi mpaka leo Kamati ya Kisekta imeshaihoji bodi ya Bandari kuhusu yale magari na Vichwa vya treni vilivyokuwa vimetelekezwa Bandarini Dar es salaam. Kamati za kisekta kazi yake ni kutembelea miradi tu lakini hazioni kama kuna umuhimu wa kuihoji serikali zikiwa zimemakinika?
Sijui bunge letu limekumbwa na nini?