Bunge likivunjwa kuna wabunge watapishana kuhama vyama

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,795
Yaani kwa jinsi upepo unavyooenda kuna wabunge wa ccm watahamia vyama vingine vya upinzani na bado kuna wabunge wa upinzani watarudi ccm hii ni baada ya bunge kuvunjwa maana inaonyesha kabisa kuna ambao waliweka msimamo hadi bunge livunjwe.

Uchanguzi unaonyesha huko chama kuu kuna kundi kubwa sana mpaka sasa wameshakata tamaa ni vile tuu wako huko ila ikifika mwisho wa muda wao kila mmoja anachukua mbao yake kwenye boti pote la mbali huyu mwendeshaji atajua mwenyewe.

Kutokana na baadhi ya vijana wapya wanaomkubali na kumsifia watakao ingizwa majimboni kuwania ubunge mara baada ya uchaguzi kuisha bunge lijalo sheria/katiba itachezewa maana wale wazoefu watakuwa hawapo na hapa ndipo fursa itatumiwa ya ndiooo mswada kupitishwa hata kama hauna maslahi kwa nchi,na hili lisipoangaliwa kwa ukaribu hata muda wa ukomo wa urais kuna wasiwasi ukabadilishwa na hapo ndio itakapojilikana kuwa kile kinachosemwa kimetimia maana ile nguvu ya bunge itakuwa imeshashikwa na mtu mmoja ambae hakuna tena mwenye uwezo wa kuongea/kumkemea.

Je!kama hili litafanikiwa nini hatma ya nchi yetu na watanzania kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom