Bunge lichunguze mkataba wa Tsh bilioni 65 ilioingia Tanesco na kampuni ya Wahindi kuna harufu ya wizi

Kwa nini uongozi wote wa Tanesco ulifutwa kazi kuanzia Waziri Kalemani na Bodi yote na Mkurugenzi wake mkuu?!

Kwanini wakuu wa Idara wote walihamishiwa utumishi ili wapangiwe kazi zingine?!

Kwanini mara baada ya yote hayo kutendeka Tanesco kupitia safu mpya ya uongozi waliingia mkataba wa bilioni 65 Tsh kwa ghafla na kwa haraka isiyotarajiwa?!

Ni kweli mkataba ule wa mabilioni ya Tshs ulikuwa muhimu mno kuliko hizo pesa zingeelekezwa kwenye matumizi chanya ya kutatua changamoto lukuki zilikabiliao shirika hasa kwa kauli za Waziri husika kudai lipo tatizo la ukarabati wa miundombinu na zile fedha si zingeelekezwa kule?!

Kwa nini sasa huo mkataba na wahindi uingiwe ghafla namna ile na je Baraza la mawaziri lilitoa baraka za uingiwaji wake?!

Tunaomba Bunge letu liunde kamati maalum ya wabunge mahili kwenye kada hiyo ili iweze kuchunguza kwanza uhalali wa mkataba ule na nini faida zake.

Pia endapo ikabainika mkataba ule haukuwa na umuhimu wowote basi Bunge liiwajibishe Serikali kwalo.

Ndugai, kupitia uchunguzi wa Bunge kuhusu huo mkataba angalau kwa uchache wa imani wananchi wataanza kukuamini tena.
Uchunguzi Tena! Wa Nini sasa? Ulishaona supika inaichunguza redio? Mmm sasa Italians? Acha utani bwana😆😆😆
 
Tanzania ni shamba la Bibi hata magufuli na watu wake walipiga so acheni na awamu hii wapige hela za kujiandaa na uchaguzi
 
Hawa ndiyo aina ya mawaziri wanaopendwa na "watu wale", full comedians, badala ya kutatua tatizo la maji wanaleta maigizo...Eti wanaenda kuchota maji na wananchi...

1637424716898.jpeg
 
It's not about kufuta bodi hapa, it's all about that money.
Tanesco chini ya Waziri aliyepita walitangaza tender na kampuni zikaomba , Waziri wa Sasa amekuja kushuhudia utiaji sain na kazi ianze.Pesa imetoka Kwa ajili ya kuweka Sawa mifumo ya Tanesco so mlitaka naye aanze kutudanganya kama last phase? Sasa hapo mnamlaumu Kwa lipi?
 
Mtu alikuwa Magufuli tu katika hii nchi. Pamoja na mapungufu yake yote,lakini alikuwa na uchungu. Usingeweza kukuta vitu vya ajabu ajabu namna hiyo. Ghafla nchi imebadirika upigaji umekuwa live live sasa
Huyo ndio alikuwa fisadi kuu, midege amenunua fedha hazijaizinishwa na bunge, hili tu wapige ten percent, hakuna mkataba hata mmoja kipindi Cha mwendazake ambao ulikuwa wazi au vinginevyo,Tena ukijitia kuhoji umekwisha,

Kipindi Cha Samia mambo mengi anaweka wazi, akikopa fedha nje anatueleza wananchi, mwendazake yeye alikuwa anakopa fedha kwa aliowaita mabeberu,halafu misukule yake anaidanganya kuwa anatumia fedha za ndani,

Mwendazake Kama angefankiwa kumaliza vipindi vyote viwili, Nchi ingekuwa na Deni hata la trillion 200,

SAMIA Ni best president ,na ataifikisha Nchi mbali Sana kimaendeleo, nyie misukule ya mwendazake dawa yenu ipo jikoni!!
 
Watanzania tunapenda sana kudanganyana......

Ndugai aanze lipi sasa?!!

Kwani yuko mbunge naye ameibua kutaka uchunguzi wa manunuzi (value for money) yaliyofanywa na serikali kuanzia 2015 mpaka 2021.......
 
Tanesco chini ya Waziri aliyepita walitangaza tender na kampuni zikaomba , Waziri wa Sasa amekuja kushuhudia utiaji sain na kazi ianze.Pesa imetoka Kwa ajili ya kuweka Sawa mifumo ya Tanesco so mlitaka naye aanze kutudanganya kama last phase? Sasa hapo mnamlaumu Kwa lipi?
Unamaanisha Tanesco wakati wa Magufuli iliingia tender ya ku-monitor kwa satellite jinsi umeme unavyokatika? hebu tuwekee hiyo tender hapa.
 
Unamaanisha Tanesco wakati wa Magufuli iliingia tender ya kumonitor kwa satellite jinsi umeme unavyokatika? hebu tuwekee hiyo tender hapa.
Tender Kwa ajili ya kupata huo mfumo ilitangazwa wakat Kaleman akiwa Waziri chini ya JPM na wala sio Serikal hii ya Sasa.
 
Kwa nini uongozi wote wa Tanesco ulifutwa kazi kuanzia Waziri Kalemani na Bodi yote na Mkurugenzi wake mkuu?!

Kwanini wakuu wa Idara wote walihamishiwa utumishi ili wapangiwe kazi zingine?!

Kwanini mara baada ya yote hayo kutendeka Tanesco kupitia safu mpya ya uongozi waliingia mkataba wa bilioni 65 Tsh kwa ghafla na kwa haraka isiyotarajiwa?!

Ni kweli mkataba ule wa mabilioni ya Tshs ulikuwa muhimu mno kuliko hizo pesa zingeelekezwa kwenye matumizi chanya ya kutatua changamoto lukuki zilikabiliao shirika hasa kwa kauli za Waziri husika kudai lipo tatizo la ukarabati wa miundombinu na zile fedha si zingeelekezwa kule?!

Kwa nini sasa huo mkataba na wahindi uingiwe ghafla namna ile na je Baraza la mawaziri lilitoa baraka za uingiwaji wake?!

Tunaomba Bunge letu liunde kamati maalum ya wabunge mahili kwenye kada hiyo ili iweze kuchunguza kwanza uhalali wa mkataba ule na nini faida zake.

Pia endapo ikabainika mkataba ule haukuwa na umuhimu wowote basi Bunge liiwajibishe Serikali kwalo.

Ndugai, kupitia uchunguzi wa Bunge kuhusu huo mkataba angalau kwa uchache wa imani wananchi wataanza kukuamini tena.
Yes ndugai bunge lichunguze huu mkataba na wahindi. Hawa wamefikia kiasi kwamba lazima watupige iwe mvua iwe pakavu. Saa hivi wapigaji wamo kwenye steering. Tusikubali lazima kuwang'oa.
A luta continua. Viva Magufuli
 
Back
Top Bottom