Bunge letu na Tuhuma za mke wa Kaisari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu na Tuhuma za mke wa Kaisari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 9, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  JULIUS Kaisari alipata kutamka; " My wife ought not even to be under suspicion"- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.

  Kaisari alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume na mienendo mema ya ndoa.

  Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari kumwacha mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa kutenda yalo maovu.

  Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ilivyo sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba kwa Waziri mwenye dhamana kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa ni kashfa kubwa.

  Si tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa nchi nzima. Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hiyo isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake kwa Bunge na umma.

  Maana, hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari wameshajiuzulu.

  Lakini, likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, Waziri mwenye dhamana aliyetoa tuhuma hizo hadharani na watendaji wenzake wakuu wenye kuhusika na taarifa ya Waziri wanapaswa wajiuzulu mara moja. Ni kwa vile, watakuwa wamesema uongo.

  Na hilo ndilo Neno la Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Raia Mwema juma hili)

  Maggid Mjengwa,
  Bagamoyo.
   
 2. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ukweli mtupu
   
 3. peri

  peri JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  umenena vyema mkuu
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kama EL alijiuzulu kwa kashfa za Dowans, na baadae kusafishwa na boss wake kuwa alisingiziwa (na yeye akaridhia kujiuzulu kwake)! I gave up on this govt long time ago!

  Kaisari alimtaliki mkewe, lakini hakuwahi kuona wala kufikiria umuhimu wa kumrudia. Waswahili vigeugeu ndo maana hata ukiitwa kusuluhisha ndoa una-tread carefully! Manake wakipatana utakuwa ndo mchawi!
   
 5. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Let it be so! Lakini nina wasiwasi kama wataweza ku resign, siyo utamaduni wa viongozi wa Tz.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Very Good!
   
 7. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Hili linawezekana kwa wale wote wanaotumia vichwa vyao kufikiria zaidi ya kufugia nywele! Viongozi wanatumia vichwa kuendeleza ujinga. Sasa ndo waje wajiuzulu, wanakichaa!?
   
 8. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu haya yamekuwa yakitokea muda mrefu, halafu ukumbuke haya yote yamewezekana tu kwa sababu ya changamoto za kambi ya upinzani. lakini ukiyaangalia haya mambo kwa undani utagundua kuwa ndani ya ccm haya mambo yamo kwa muda mrefu na wanayajua vizuri sana ndo maana yakiibuka huwa hawatetemeki, sanasana wanachofanya ni kuyafunika. (rejea ishu ya jairo, na yaliyoibuka hapo). ilionekana wazi kuwa ule mtindo wa wizara kuja kupitisha bajeti kwa kuwapa mlungula wabunge ulikuwa ni kawaida na ccm wengi walikuwa wanaujua. Mwenyezi Mungu alitusaidia nguo zikawavuka waTZ tukaona maumbile yao ya siri.

  Cha muhimu hapa tuhangaikeni kuwaelimisha watu namna rasilimali za nchi zinavyoporwa na hii serikali ya ccm na washirika wao wawekezaji, ili sasa, wananchi kwa ujumla wetu tuwaondoe hawa madarakani.

  Tukiwaondoa hawa, nina uhakika tutakuwa na wasaa mzuri kabisa kama taifa wa kurejesha mfumo wa uadilifu. hata hawa baadhi ya wapinzani wanaotuhumiwa, mi naamini wanashawishiwa sana na hawa vinara na wazoefu wa huu mchezo wa rushwa ccm, sawa ni lazima tuwapigie mayowe, lakini saratani hapa ni huyu mzazi na mlezi wa huu mfumo, ccm, hasa hizi awamu za 2,3 na hii ya 4 ambayo ndo mbovu kabisa funga kazi.
   
Loading...