Bunge letu na kura za mayowe 'NDIYO' 'SIYO' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu na kura za mayowe 'NDIYO' 'SIYO'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duduwasha, Apr 16, 2011.

 1. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,157
  Trophy Points: 280
  Ndugu Wananchi!!! Nadhani tumefikia mwisho wa kiwango chetu cha matumizi ya Bunge!! Huu upigaji wa kura za Midomo uwe mwisho Tuweke mwingine...

  Kila mbunge mwenye nia Njema ya Kuchangia Muswada ajulikane na awekwe wazi Watanzania wote Wamjue kama ni Mcheleweshaa maendeleo au lah! Kwani imefikia Wazi Bunge Letu sio Tukufu tena. Na hatuliamini tena Majibu ya aliyochangia yachapishwe na kuwekwa kwenye Jimbo lake ajione ukilaza wake, kwa mwananchi yeyete anapotizama Bunge la sasa, Lazima apatwe na kichefuchefu..!! puuu!!

  Hoja na miswada inapitishwa au kukataliwa kwangu mimi naona ni kizembe.., kwani hata kile cha maana kinaweza kataliwa bila sababu za msingi au ikatolewa sababu isiyohusiana na hoja ali mradi ionekane mpinga hoja au mtoa hoja kapotoka au kupotosha nini maana yake... Ukweli huwa haujifichi na mnafiki anaonekana wazi.

  Inafaa sasa kuwe na kuapa unapopitishwa muswada wenye maslai ya wananchi, ukada wa vyama uwekwe kando.. Bunge lishakuwa la kichama sio la wananchi tena.

  Na ikifika muda wa kupiga kura waliopinga wapewe pepa waeleze sababu zao maalum za kupinga ua kukubari muswada au marekebisho ya sheria. Wananchi waliomtuma wamuelewe ndicho walichomtuma.. kwani imekuwa tabia mbunge analala kwa kuwa ni wa chama fulani anakurupuka na kusema Ndiyooooo au Siyoooo kama zuzu..

  Na ningependekeza kuwe na faini kwa wabunge waropokaji manake mashangingi yashavamia Bunge, kwa kuwekwa na wapenda mashangingi ,utasikia fujo sana bungeni kana kwamba Wabunge hawana Adabu vigelegele kama wapo kitchen party. Namhurumia Spika anawatuliza bila mafanikio sababu ni wa chama chake hana la kuwafanya.

  Wananchi Tungeomba tukemee wajapo Majimboni mwetu, tatizo ni wale waliopewa hawana majimbo..Viti maalum..

  Ndiyoooooo.... Siyooooooo.. whats is this... Tuvue Magamba Kila Sehemu 50 years kwa system hii imesha fail tuige za wenzetu walioendelea... mambo ya kupeana 90 days siyo mwake mfilisi kwanza..

  Bunge limefikia kiwango chao cha mwisho wapige simu kwa wananchi wawasaidie
   
 2. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Labda hujamwelewa,anasema wasioafiki,halafu anamalizia,wanafiki waseme ndiyo,ndipo wabunge wa Ccm wanajibu ndiyo,
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wanafiki----siyooooooooooooooooo
  Wakweli-----Ndiyooooooooooooooo:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Wananchi tuwaelimishe kupitia CDM kinachofanywa na vilaza wao wa CCM wawapo mjengoni, ili 2015 tuchukue viti vya kutosha ikiwezekana 2je kubadili kanuni kwa manufaa ya taifa letu. Mashangingi wavua chupi siku hizi ndo wamejazana mjengoni, wanashangilia ndiyoooo ili kulipa fadhila za mabasha wao, lakini hoja hawana, inatia kichefu chefu wallah!
   
 5. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hivi ndugu zangu wenye taaluma IT hakuna electronic device ambayo zinaweza kufungwa kwenye kila meza ya Mbunge kwa ajili ya kupiga kura pale inapohitajika? kama zipo nafikiri huu ndio muda muafaka wa kufunga device za namna hiyo na kama hakuna inabidi watu wafikirie ni njia gani iwe rasmi kwa ajili kupiga kura bungeni ambayo ni confidential kwasababu tulichokishuhudia bungeni leo ni aibu. wabunge wengi wa CCM ni waoga kuonesha misimamo yao mbele ya viongozi wao.
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Very sad:alien:
   
 7. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo utashangaa mijitu mingine inasema eti tunatetea cdm,mmeona leo vilaza wa ccm?hawana akili kabisa uliwahi kuona wapi kura zinpigwa kwa mdomo?eti semeni siyooooooooo!au ndiyoooooooooo! Huu ni upumbavu mpaka zito kawarekebisha,that's ******* Spik.
   
 8. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati Samwel Sitta anahitimisha Bunge kuingia kwenye uchaguzi wa 2010, alisema Bunge lijalo (hili tunalolishuhudia sasa) litatumia teknolojia ya elektroniki, yaani kila Mbunge atafungiwa kifaa maalumu ambacho kitamfanya 'abofye' kitufe cha 'NDIYO' au 'SIYO' na kura zitajumulishwa automatically, pia kitakuwa na mambo mengine ya msingi.

  Hii imefikia wapi wakuu? Au kwa sababu speed and standard sasa siyo spika? Unakumbuka kikao kilichopita kuhusu hoja ya Mh Lissu ilibidi spika aanze kuita majina moja baada ya jingine na kusema ndio au hapa hii ni baada ya sauti za ndiyo na hapana kukaribiana.

  Matokeo yake wabunge wa CCM waliufyata (waliogopa kuhojiwa kwenye vikao baadaye kuwa why umesema Ndiyo?) na kusema siyo na wale wa ndiyo wakashindwa.

  KUMBE NJIA HII INGEONDOA KURA ZA MKUMBO,Vipi swala hili limefikia wapi?

  Tumuulize nani?

  Makinda? Kashilila? Au nani?

   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  utadhania ni muhadhara wa manzese
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inafanywa makusudi kuwadhibiti wabunge wa CCM. Maana wakishawekwa kwenye kamati, wakitoka huko hawna tana hamu na maslahiya taifa bali kulinda magamba.:confused2:
   
 11. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  Pendekezo: tuandike e-mail kwa ofisi ya bunge kuuliza hii kitu iliishia wapi? zijae ili wajue watu bado tunikumbuka hiyo ahadi. nimeshaituma. e-mail ni tanzparl@parliament.go.tz
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,580
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM ni wachumia tumbo hawana akili kabisa ndiyo maana viongozi wao wanawafanya kama mbuzi wa shughuli, hovyo kabisa hawa wabunge magamba
   
 13. M

  MPG JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wabunge wa magamba a.k.a CCM wanatusumbua sana kila kitu ndiyoooooo..ANGUKO LA CCM LIMETIMIA.
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hela zinapiga mjengo hapa dar hado brbr imefungwa.
   
 15. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,211
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  Kwenu Wabunge (Waheshiwa wa kambi ya upinzani).

  Napenda kuwapa moyo kwa kusema hongereni kwa Kazi nzuri mnayofanya pamoja na Uchache wenu Bungeni. Niseme kuwa asiyejua nini Maana ya Haki na Amani ndiye tu mwenye kuweza kukejeli kazi kubwa mnayofanya kutuepusha na janga la vurugu huko mbeleni na kwamba bila haki amani hutoweka.

  Waheshimiwa Wabunge naelewa kuwa mnafahamu vizuri Kanuni za Bunge Letu,Hivyo basi ningependa tuirejee Kanuni Za Kudumu ya Bunge ya 2007 kipengele namba 34;1,2,3 na 4,kama inavyosomeka hapa.

  34.
  (1) Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni maombi
  kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo, na ombi hilo halitawasilishwa Bungeni mpaka kwanza taarifa ya ombi hilo iwe imetolewa kwa maandishi na kupokelewa na Katibu si chini ya siku mbili za kazi kabla ya Mkutano ambapo ombi hilo linakusudiwa kuwasilishwa.
  (2) Ombi lolote linaweza kuwasilishwa Bungeni na Mbunge, likionesha jina la Mbunge anayeliwasilisha.
  (3) Mbunge anayewasilisha ombi atatoa maelezo mafupi ya kutambulisha watu wanaotoa ombi hilo, idadi yao, saini zilizoambatanishwa kwenye ombi hilo, madai ya msingi yaliyomo, na madhumuni ya ombi hilo.
  (4) Baada ya kutimiza masharti ya fasili ya (3) ya Kanuni hii, Mbunge anayewasilisha ombi anaweza kutoa hoja kwamba, Bunge lijadili ombi hilo, isipokuwa kwamba hoja hiyo haitahitaji kutolewa taarifa na inaweza kuamuliwa bila mjadala wowote.

  Baada ya kujiridhisha na Kanuni natumai kama mpiga Kura halali na ambaye kama wengine tumewapa nyinyi waheshimiwa nafasi ya kutuwakilisha sasa naomba kipengele hii itumike kufikisha hoja au maombi ya Kubadilisha/batilisha mfumo unaotumika kupitisha hoja ya Serikali (Ndiyo na Siyo) badala yake hoja ipite kwa kila Mbunge kusimama na kutamka kuunga au kutokunga hoja.Maana Kura zetu lazima ifike mahali ithaminiwe na Kodi zetu itumike kwa minajili iliyokusudiwa ya uwakilishi wa wananchi ambao tunaweza kuupima kwa Kauli na Vitendo.

  Mheshimiwa Zito naelewa kuwa hoja hii uliiguzia kwenye Kikao hiki kinachoendelea cha Bajeti lakini sikumbuki ni mjadala upi na kama sikosei ni ule wa Wizara ya Fedha (Marekebisho yanakaribishwa.)

  Naelewa wazi kuwa wenzetu wa Ndiyo imepita watatumia uwingi wao lakini hii isiwakatishea tamaa .

  Sasa naomba kuwasilisha Ombi lenyewe.

  Kwamba Wabunge wote waupinzani kwa ujumla wenu mtaomba kwa niaba ya wapiga kura wenu pamoja na wasiowapiga kura wenu kuwa Mfumo unaotumika sasa wa kupitisha hoja kwa Kauli ya Ndiyo na Siyo ikimaliziwa na Spika, Naibu wake au Mwenyeviti kwa Kibwagizo cha Nadhani waliosema Ndiyo wameshinda imepitwa na wakati na ni Matumizi mabovu ya Muda na Rasilimali za Watanzania.

  Kwamba Mtapita majimboni Kwenu na Nchi Nzima Kukusanya Majina na Saini ya wanaowaunga Mkono kwa hoja hii kama Masharti yanavyotaka.

  Nakwamba mtakusanya kwa pamoja na kuwasilisha kama hoja ya pamoja (Upinzani) Bungeni kubatilisha au kufuta mfumo huu (Ndiyo na Siyo)

  Naomba Kuwasilisha.
   
 16. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,211
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  Msomaji na Wana Jf wengine tunaweza kupanua mtazamo kwa Nyongeza hii na kwamba vita hii ni yetu wote bila kujali mtazamo tofauti wa kisiasa.

  Copied from Raia Mwema as shown below.

  Kona ya Karugendo

  Kwa nini tupoteze fedha nyingi kujadili "ndiyo" bungeni?

   
 17. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani waliosema NDIOO, wameshinda.....

  Ndivyo tunavyotegemea bajeti ya CCM, ikipitishwa kwa mwangwi wa sauti za ndiyooo kutoka kwa wabunge wa CCM.

  Source: Mnyika NJE YA UKUMBI WA BUNGE
   
 18. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kila kati ya wabunge watano watakao simama wanaponda na kuilaumu.. Serikali tena sana... Lakini wanamaliza kwa kuunga mkono hoja.. Mmoja tu kati yao haungi mkono hoja.. ndo.. Watazomeana hapo watachekana hapo bungeni.. Watapina meza zao.. WATASEMA NDIYOOO Mama mwenye nyumba makinda atawasapoti.. My take SIASA ZIMEHAMIA BUNGENI..! NIDHAMU {F" UCHAPAKAZI ZERO.. AHADI LUNDO UTEKELEZAJI {F}.. WATANZANIA TUJIKOMBOE WENYEWE TUSIDANGANYIKE .. !Wabunge nao wanatafuta hela na maslahi kama sisi.. Wanakula kodi zetu.. Wanajichana madini yetu wanatufisadi.. MWADAMU HANA WEMA USIMWONE KUCHEKA MULE BUNGENI
   
 19. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  haya ndo madhara ya kuwa tunapitisha sheria kwa ushabiki wa wengi wape, leo watu wanalalamikia sheri ya mafao ya miaka 55 hadi 60, hata wale waliokuwa wakiishabikia kwa kutoa sauti ya ndiyooooooo wanalalamika,
   
 20. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  True !
   
Loading...