Bunge letu lina Waganga, wachungaji na Mashehe kwann mambo hayaendiii???

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Nimewaza sana lakini sijapata jibu bunge letu lina aina zote za watu tunaowaita wa Mungu ila ni mungu yupi wanamjua wao na miungu yao.

Najiuliza hawa watu tunaowaita wa mungu wanafanya mambo ya Mungu?

Mungu mimi kwa imani yangu Huwezi kumpenda kama binadamu mwenzio unamchukia au humpendi.

Lakini wachungaji, waganga na mashehe wanajipenda wao kwanza kabla ya wengine sijui ni mungu wao ndo anawafundisha kujipenda zaidi kuliko wengine???

Katika maisha yao wanaamini nini??
 
Mambo hayaendi kwa nchi nzima kwa sababu ya dhuluma! (kubwa yao ni shirki)
Waislamu tunajua waziwazi kutokana na mafundisho ya Quran na Sunnah kuwa ukitaka kuharibikiwa Duniani na Akhera basi jiingize katika dhulma, nikinukuu aya na Hadith kuhusu dhulma nafasi haitatosha hapa! lakini inatosha kuwakumbusha kauli ya Mtume SAW kuwa "Ogopa dua ya mwenye kudhulumiwa kwa sababu hakuna katika yake na Mwenyezi Mungu kizuizi (chochote)"
Ukiangalia Biblia:
(Jeremiah 21:12), "...Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu ye yote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu".
Hata katika nchi za Ulaya wanajaribu sana (kimfumo) kuhakikisha kuwa hakuna anayedhulumiwa ndani ya mipaka ya nchi zao, hii yote ni baada ya kushuhudia historia ikionyesha kuwa kila wakati taifa moja au jingine likijiingiza katika dhulma basi hilo taifa huteketea na kutoweka pamoja na mfumo wake.
Umeona juzijuzi jinsi dhulma ya watoto wa Kiislamu wanavyodhulumiwa elimu ilivyojidhihirisha wazi, wako wapi Maaskofu wakuwaponya waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu?!
Sawa, hawana uwezo basi hata kuukemea uovu wameshindwa?!
 
Back
Top Bottom