Bunge letu letu si lazima kuiga lakini tunaweza kujifunza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu letu si lazima kuiga lakini tunaweza kujifunza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Jul 21, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa (breaking news) sasa kuwa yapata watu 12 wameuwawa Colorado wakiwa katika ukumbi wa sinema nadhani 16 Century. Haya ni maafa yasiyotarajiwa kama yaliyotukuta ya wenzetu Watanzania waliofariki katika ajali ya meli visiwani juzi.

  Rais Obama na mpinzani wake wamesimamisha shughuli zote za kisiasa kwa ajili ya hili tukio.

  Ukweli ni kwamba baada ya kuwa ma- Rais wetu wametangaza maombolezo ya tatu isingekuwa vibaya kuendelea kuahirisha shughuli za Bunge au hata ku-dedicate muda wa Bunge kujadili tu namna ya kujikinga na kujiandaa na majanga au matatizo ya ajali za vyombo vya usafiri kwa undani. Hapa naona kuwa Tundu Lissu alikuwa sahihi kuomba ruhusa ili awasilishe hoja.

  Wana CCM wenzangu tafadhali sana wakati mwingine tusiwe watu wa kuwahukumu au kudharau kila hoja eti kwa sababu tu zimeletwa na watu wa upinzani. Si lazima tuige wanachofanya USA na kwingineko lakini tunaweza kujifunza somo fulani hapa.
   
Loading...