Bunge letu kwa sasa halina faida yoyote kwa Wananchi

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
784
1,260
Wabunge walitakiwa ndio wawe wa kwanza kupinga mambo ambayo yataumiza wanchi lakini Kwa sasa imekuwa kinyume wao ndio wa kwanza kupitisha mambo yanayokuja kuumiza wananchi.

Vifurushi vya simu vilipanda na wao waliunga mkono.

Wapangaji wanalipishwa kodi za majengo waliyopanga kupitia Luku wabunge wamekubali na wamepitisha.

Serikali imeweka tozo katika miamala ya simu iliyasababisha ghalama ya kutoa million Moja kupanda kutoka tshs 8000 hadi tshs 17400 wabunge wamekubali na wamepitisha.

Mawakala wa M-pesa, tigopesa na Airtel money hawa ni wananchi wa kawaida na ndio waliowapigia kura katika haya mabadiriko wabunge hawahitaji kujua Wala kufuatilia ili kuona hawa mawakala wanafaidika vipi maana inasemekana katika haya mabadiriko na wao kamisheni zao zimeshuka.

Hapo nyuma ilikuwa mteja akitoa laki 2 wakala anapata kamisheni ya tshs 1200 ila kuanzia Jana Wana pata tshs 400 mana yake hapa ajira ya uwakala imeshakufa.

Kwa hiyo hili bunge halina faida yoyote Kwa Watanzania sana sana ni mzigo tu Kwa wananchi ikiangalia uwingi wao na kiasi cha mishahara pamoja na marupurupu wanayolipwa.

Lakini pia nahisi Watanzania tumefanya makosa kuchagua wabunge wa chama kimoja na hili litatugalimu miaka yote 5 hi iliyobaki
 
Viti maalum waondolewe kabisa,

Tuwe na senate yenye wabunge wasiozidi 45.

Hawa watakua wanapitia maamuzi ya bunge la kawaida kabla ya kuwa Sheria.
 
Hilo ndio bunge lililochongwa na Mwendazake!!! Sisi wenye akili tulijua tuuu nini kitafuata!??
Marehemu alikichonga hili bunge ili limuongezee muda wa kukaa madarakani.
Hizo ndio zilikua ndoto zake ila watu hawakijua sasa mbunge aliye pendelewa na magufuli ataikosoaje serikali!?? Haiwezekani!!!
Hivi dunia ya leo una mwacha zito kabwe ,john mnyika ,sugu ,nk unamweka babu tale!?? Hapo unategemea nn!??
 
Back
Top Bottom