Bunge letu kuyumba tatizo ni elimu ndogo ya wabunge, kuwa la kichama zaidi au uongozi mbovu?

Vyote ila unaposema kichama uangalie pande zote!

View attachment 519540
Hizi ni bangi, muone mdee hapo juu.
Kwa mdee kupinga uhuni ndio bangi ila waliosababisha uhuni sio bangi??? Tuache ushabiki mkuu...... kosa lilianza kwa spika iwaje uone impact ya kosa lake ukaacha kuoma chanzo cha kosa??? Ni sawa na mtu umpige kofi yye akurushie ngumi afu useme ni mvuta bangi

Lets get real
 
Vyote. Binafsi sioni faida yao zaidi ya kutafuna pesa yetu ya kodi wana gharama sana halafu mchango wa kwa taifa ni mdogo sana. Kama mikataba mibovu inapitishwa wao wanazidi kuongeza vitambi. Hawana umuhimu wowote. Tuwapunguze mkoa mmoja mmbunge mmoja inatosha.
 
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Nionavyo mimi tatizo lililopo kwasasa ni UNAFIQ.Kunakundi la wabunge wanaojifanya wanasifia mdomoni wakati moyoni wanakashfu. Wala elimu ndogo sio sababu kwa sasa,kwa sababu tunaona hata madokta na maprofesa wanajifanya hawana uelewa wawanayo zungumzia.
UNAFIQ ndio kikwazo cha maelewano bungeni kwa sasa.
 
La kichama zaidi. Tena ccm wanajiona wao Ndio wao kwa sababu tu wana spika na naibu wake wanaowa favour. Ipo siku mnayowatendea wenzenu mtatendewa nyinyi,na itakuwa chungu zaidi ya shubiri
 
Kwa mdee kupinga uhuni ndio bangi ila waliosababisha uhuni sio bangi??? Tuache ushabiki mkuu...... kosa lilianza kwa spika iwaje uone impact ya kosa lake ukaacha kuoma chanzo cha kosa??? Ni sawa na mtu umpige kofi yye akurushie ngumi afu useme ni mvuta bangi

Lets get real
Ni vizuri kubishana kwa maneno, alichofanya mdee ni kuvuka mipaka.
Na pia nimesema bunge lote upuuzi wake wote unaletwa na sababu tajwa za mleta uzi.
 
Kwanza Kutanguliza Uchama Kuliko Maslahi Ya Taifa Kwa Ujumla Ni Tatizo. Na Hii Inatokana Na Ujinga Wa Kushindwa Kujifunza Maana Hasa Ya Siasa Ya Vyama Vingi.

Lakini Pia Maslahi Na Sifa Binafsi. Mbunge Anaingia Bungeni Mawazo Yake Yote Ni Posho Na Kuwafurahisha Wakubwa Wa Chama Chake, Ni Lazima Awe Mnafki Hata Kama Anaujua Ukweli.

Na Mwisho Kabisa Sheria Irekebishwe Ili Kutupa Nguvu Wananchi Juu Ya Wale Tunaowachagua. Unakuta Mwakilishi Anapwaya Kabisa Kuwasilisha Matatizo Na Maoni Ya Wananchi Bungeni, Lakini Wananchi Hawana Cha Kumfanya Mpaka Amalize Muda Wake.
 
Ni vizuri kubishana kwa maneno, alichofanya mdee ni kuvuka mipaka.
Na pia nimesema bunge lote upuuzi wake wote unaletwa na sababu tajwa za mleta uzi.
Hakuna asiyejua mdee alikosea na bulaya pia ila ni muhim kuangalia circumstances kma alivyosema mtolea..... mnyika katukanwa, akaomba maelezo akapuuzwa zaidi akaishia kutimuliwa ni psychology ndogo tu ssa kuwa lazima wapinzani wapandishe hasira baada ya MTU WAO kuonewa ssa badala ya kubalance game yye anaenda kuwatimua na waliomback mnyika..... hivi ndio nini hiki mnafanya??? Mnagain nni kuwakomoa wapinzani?? Afu watu wazima kma nyie mnashabikia kabisa???

Dah unanishangaza mkuu..... mwaka mzima wako nje??? And its fine with u
 
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.

Unaweza kuwa na elimu lakini ukawa na mawazo madogo, yaani haujawa exposed na dunia. Na unaweza kuwa na elimu ndogo lakini ukawa exposed, na elimu ya dunia, you are well informed. Wabunge wetu wengi hawana elimu ya dunia, hawajui kitu gani kinachoendekea duniani zaidi ya Tanzania. Kisha wanaleta mawazo yao ya jadi na ya kidini na kuyaingiza kwenye sheria za nchi. Kwa mfano No. 1. Mwalim alisisitiza Tanzania as a country haina dini, bali kila mtu ana dini yake, lakini kuna wanasiasa wanataka kuleta sheria za dini kwa nguvu kurudisha maisha ya Watanzania nyuma.

kwa mfano, Mbunge wa kuteuliwa Mama Kikwete, anapinga watoto wa kike wenye kupata mimba wakiwa wadogo waruhusiwe kuendelea na elimu ati kwa kuwa dini hairuhusu, dini gani hii isiyokuwa na msamaha? Zaidi ya ubinafsi na chuki? Na HUYU ndiye mbunge anayejisifu anapigania haki za wanakina mama na watoto, Sasa HUYU mama tunategemea maendeleo gani anaweza kuleta na mawazo yake ya kizamani? Anajuwa wazi watoto wa masikini ndiyo watakuwa affected, Na kama ni binti yake atampeleka shule za binafsi.

2. Wabunge wengi wako kwenye siasa kwaajili ya power na kujitajirisha wao wenyewe, Watu hawa wengi wao hawaelewi, hawana mawazo ama fikra zaidi ya kufikilia watanyakuwa nini wakati wakiwa wabunge. . Wengi wao wanaonana na wanaowachaguwa wakati wakiomba kula, baada ya hapo, haswa Wakati wa serikali ya nne ni nikufikilia benefits zao allowance na magali makubwa ndizo waliokuwa wakizipigania.

Wabunge wetu wanatakiwa wajielimishe, . Wasome magazeti zaidi ya magazeti ya udaku. Dunia inabadilika tena kwa kasi, wananchi wanaona Wabunge wa Nchi nyingine wanavyowatumikia raia, wengi wao bado wanaishi kwenye dunia ya unyakuwaji. Wanatakiwa waache mazowea ya ubinafsi, watembee dunia kama sio kusafri hata kwa mitandao wajue dunia inaendeleaje. Bado tuko mbali sana, kwa uongozi..
 
watanzania ni wavivu wa kusoma(Elimu halisi haipatikani darasani bali kwenye kusoma/reading vitu sahihi). Sina hakika na wawakilishi wetu kama nao wanatabia kama zetu...
Umenena vyema!

Hata mimi sinahakika kama wanatabia ya kusoma vitabu.
 
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Yote yanachangia.....
kwa mfano...Wabunge wengi elimu yao ni tatizo hasa wakina mama...unaweza ukaona ni hoja gani wanazochangia kwa wingi..leo wamekuwa kidedea katika kuchangia hoja za kuwaadhibu wenzao...
Ungozi mbovu...ili halina shaka toka aondoke Sitta (Marehemu) tatizo linazidi kukuwa...
Ofcourse kuwa kichama hili halipingiki lakini je swali la kujiuliza kwani wakati wa Sitta halikuwa kichama? mbona mambo yalikuwa yanaenda vyema tu...
 
Vyote. Binafsi sioni faida yao zaidi ya kutafuna pesa yetu ya kodi wana gharama sana halafu mchango wa kwa taifa ni mdogo sana. Kama mikataba mibovu inapitishwa wao wanazidi kuongeza vitambi. Hawana umuhimu wowote. Tuwapunguze mkoa mmoja mmbunge mmoja inatosha.

Maana ya ubunge ni kuwawakilisha watu walio kuchaguwa; Wanatakiwa wawe mikowani mwao kusikiliza shida za watu waliowaweka bungeni. Wakiupata ubunge tu, wanapotelea mitaani mpaka siku ya kuomba kula tena. Faida gani ya kuwa na mbunge? Wengi wao hawajui kitu chochote ikiwa na shida zinazowakabili waliowapigia kula. Hawajui hata mambo yanayoendelea duniani n, hawasomi magazeti wala vitabu, tunawakilishwa na watu hawezi hata kuwakilisha familia zao.
 
Mnakwepa kwepa tu. Lakini ukweli ni kwamba asilimia 90 ya wabunge ni vilaza, elimu ndogo. Na wenye elimu kidogo nao ni walihudhuria madarasani lakini hawakuelimika..ndio maana profesa wa bongo hana tofauti na mpiga domo wa kijiweni...eti mwanasheria msomi anaongea utadhani kavuta bangee ...naangalia kwa jicho la tatu tu.
 
Pale Bungeni tatizo ni kwamba tunaleta siasa badala ya kufanya kazi unakuta chama tawala kinameza michango wa vyama vya upinzaji coz hawapebdi kukosolewa ila kama hoja zingekuwa zinachukuliwa na kufanyiwa ufumbuzi mambo yote shwari ila ndio hivo wao wakula Kodi zetu mwishovwa siku tunawalaumu Chadema hili halisaidii!!
 
Wabunge ni majanga mtu unakuta kasoma economics na ni postgraduate lakini hajui tofauti ya 'annual general meeting' inayowakutanisha shareholders and the actual process to how a PLC is managed, the make up of board of directors, the process of decision making, the legal requirement of being open etc.

Kama taifa we need a succession planning sio ya chama kimoja tu bali vijana kwa ujumla hawa jamaa wanapwaya sana.

Yaani tatizo ni kuchagua wabunge wapuuzi ambao kwao maisha yote ni kuwa mbunge, huyu akitishwa atatetea kila kitu. Angalia wabunge wetu hoja za msingi zenye kutetea maslahi ya nchi hawajali wamekalia uchama, ni elimu ndogo na njaa.

CCM ina kundi kubwa la wabunge wa aina hii
 
Kwa kweli tunahitaji katiba mpya tena ile ya Warioba, la si hivyo wapuuzi wachache watatusumbua mpaka mwisho wa dunia. Kuna wajinga wengi wamepewa madaraka hata wao hawaamini nini kimetokea.
 
tatizo baadhi ya wabunge wanavuta ndumu na kunywa viroba then ndo wanaingia mjengoni
 
Back
Top Bottom