Bunge letu kuyumba tatizo ni elimu ndogo ya wabunge, kuwa la kichama zaidi au uongozi mbovu?

Robinhomtoto

JF-Expert Member
May 17, 2017
238
250
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,387
2,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
ELimu ndogo ya siasa ya vyama vingi.Wengi wa Viongozi wa CCM na wabunge wa CCM wanaona vyama vingi nishida na uadui mkubwa.

Ni mpaka pale hawa viongozi waliofilisi Tanzania watakapoondolewa ndipo ndoto ya BUNGE huru inawezekana
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Wabunge ni majanga mtu unakuta kasoma economics na ni postgraduate lakini hajui tofauti ya 'annual general meeting' inayowakutanisha shareholders and the actual process to how a PLC is managed, the make up of board of directors, the process of decision making, the legal requirement of being open etc.

Kama taifa we need a succession planning sio ya chama kimoja tu bali vijana kwa ujumla hawa jamaa wanapwaya sana.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,260
2,000
Vyote vinachangia hasa LA uongozi mbovu Wa spika na naibu wake kisha uccm kwanza badala ya taifa kwanza na mwisho alaumiwe Kairuki kwa kutoa sifa za mbunge yaani Elimu. Hao kina kibajaji na Mzee wa utetezi Wa bangi ni kikwazo cha taifa la viwanda.
Ni wakati muafaka sasa wa bunge kupata spika asiye mbunge.
 

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,694
2,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Binge halijayumba Bali limeshindwa kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya 5.
 

kobokocastory

JF-Expert Member
Aug 30, 2014
1,059
2,000
Tatizo mfumo wa sasa wa siasa za Tanzania ni wa kujikweza na kutaka kuoneka kwa bwana mkubwa (sizonje).

Hilo linapelekea performance ya asilimia kubwa ya wabunge wa ccm kufanya kazi bungeni kishabiki badala ya kufanya kazi kwa weledi.

Wana ccm bungeni wanafanya kazi ili kumridhisha mwenyekiti wao hivyo basi katika mazingira kama hayo bunge letu lazima litaonekana kupwaya.
 

Salih

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
546
500
Nadhani ungefanya marekebisho ya swali liwe sio la upendeleo na hukumu, naona mtoa mada umelenga chama kimoja directly
 

sergio 5

JF-Expert Member
May 22, 2017
8,719
2,000
Elimu ndogo ya kina maji marefu ,na kingu ndyo wanasabisha haya yote
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,553
2,000
Yote, kujua kusoma na kuandika tu... Hili ni tatizo ila uongozi mbovu wa jazba na unao egemea upande mmoja nayo ni shida kubwa.
Tatu ushabiki wa kichama kuliko kujali maslahi mapana ya Taifa
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
28,696
2,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Vyote ila unaposema kichama uangalie pande zote!

image.jpeg

Hizi ni bangi, muone mdee hapo juu.
 

ndugaseli

JF-Expert Member
May 17, 2017
857
1,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
vyote ulivyotaja apo juu ni majbu sahh
 

zinyalulu

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
420
250
vyote vitatu, yaani kuwa na wabunge wengi wenye elimu ndogo ju ya kazi ya mbunge.
2 bunge kubeba ajenda za vyama badala ya ajenda za kitaifa.
3 bunge kuwa na viongozi waliopwaya kwenye nafasi zao
 

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,815
2,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?
Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Tatizo ni upinzani uchwara uliyopo unaoongozwa na mihemko badala ya ukweli. Hawana subira wala uvumilivu. They don't care about procedures. Wako kama vitoto vilivyodekezwa.
 

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,138
2,000
Binafsi nafikiri kinachosumbua ni njaa na kutojitambua kwa wabunge wengi.
Njaa ni upande wa uongozi wa bunge, wanashindwa kutenda kiwapasacho kwa sababu ya kulinda mkate.
Kutokujitambua ni upande wa wabunge waliowengi kufikiria kusimamia hata hoja mbovu ni sawa almuradi imetokea upande wao hivyo wanafikiria wanawakomoa walio wachache kwa vile wanajifanya wanajua kila kitu.
 

UKAWA2

JF-Expert Member
Apr 22, 2014
2,185
2,000
Yote hayo kwenye kichwa cha habari ni majibu sahihi.Ila nafikiri hilo la ubashite ni tatizo kubwa.
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,579
2,000
Wadau naomba tusaidiane kuliokoa Bunge letu japo Kwa ushauri.Bunge letu kuyumba Na kutokuwa imara kama mabunge yaliyopita tatizo ni nini?
Elimu ndogo Kwa wabunge wetu?
Kuwa la kichama sana Kwa maanavya CCM?
Uongozi mbovu?

Naomba tujadili labda litajirekebisha.
Shida ni bunge kuwa controlled na serikali?? Huwa linakuwa na meno pale wabunge wa upinzani wanapokuwa wengi sana at least 40:60 ya chama tawala ndipo kunakuwepo na uhalisia.

2.Pia ushabiki wa vyama unapunguza ufanisi mfano kambi ya upinzani na CCM hapo kila mtu atavutia jambo lenye maslahi kwa chama chake yaani ni ngumu sana lusinde kuisifia bajeti kivuli kma ilivyo ngumu kwa mnyika kusifia bajeti ya serikali kuu!!!

3.Pia imejaa wanasiasa kuliko wataalam. Yaani professionals ni wachache sana wengi ni wanasiasa hivyo wanafanya kazi kwa kuangalia maslahi ya kisiasa zaidi kuliko kuchambua na kufanya taaluma ziwaongoze maana kuna miswada hupitishwa bungeni na unashangaa kuna PHd holders na walikaa kimya tu

4.Elimu nayo ni shida. Rasimu ya warioba ililiona hili sema kwa sababu zilizo obvious haikupitishwa na ndio tunajikuta wabunge hawatumii utaalam kabisa kujadili mambo ya msingi ya kitaifa..... siku ya kupitisha maazimo ya bunge kuhusu TEGETA ESCROW yaani ni wabunge wa4 tu ndio walikuwa wanajaribu kuiweka hayo maazimio kwenye procedure za kisheria lisu chenge zitto na mdee wengine wote kimyaaaaaa...... hta mswada wa cybercrime waliochangia kwa majedwali ya marekebisho na kuchambua zile vifungu ni wabunge kma watatu tu!!!!! Nkajua shida ni elimu maana waliochambua walienda deep sana kisheria!!!!
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,579
2,000
Tatizo ni upinzani uchwara uliyopo unaoongozwa na mihemko badala ya ukweli. Hawana subira wala uvumilivu. They don't care about procedures. Wako kama vitoto vilivyodekezwa.
Kwahyo wabunge wa upinzani ndio huwa wanapitisha miswada mibovu kwa kura za NDIOOOOOOO??? na kma hawafuati procedure je unajua chanzo ni nni?? Hivi spika akitenda haki kuna mpinzani ataanza unachosema kukiuka kanuni???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom