Bunge letu kumbe ni uji kwa Mahakama Kuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu kumbe ni uji kwa Mahakama Kuu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Bunge la Kenya limeonyesha makali yake kwa kukataa kuburutwa na mahakama Kuu ya huko ambayo iliamua uteuzi wa Kibaki ulikiuka katiba ya nchi hiyo.......................

  bunge hilo kupitia Spika wake kenneth marende limeamua kamati za Bunge ziendelee na kuchunguza uhalali wa teuzi hizo bila ya kukwaza na maamuzi ya kimahakama.........................

  Hapa kwetu hata DOWANS haijaamuliwa serikali ya JK imelipiga stop Bunge lisijadili hoja ya Kafulila kwa madai ya kuwa suala lipo Mahakamani..................................hii inamaanisha bunge letu kumbe ni nyanya mbovu mbele ya mahakama zetu?

  Jingine kujadili DOWANS kwa bunge siyo lazima kujadili kama walipwe au la ila ni kuchunguza ni watendaji gani serikalini waliotufikisha hapa na kuaamua hatua za kuwachukulia jambo ambalo High Court kamwe haitalichunguza.......................

  Kinachojitokeza hapa serikali ya CCM inajaribu kutumia vibaya mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge na Mahakama kama kisingizio cha kulizuia bunge lisifanye kazi ambayo tuliwachagulia kwenda kuifanya.........................kuzuia accountability..............under the ruses of constitutional separation of powers................How absurd........................................
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  You are very right Rutashubanyuma: Hatuongelei DOWANS ilipwe au isilipwe "in the first place" lakini nani waliotufikisha hapo, hadi tukawa na DOWANS. Kwamba ilipwe au silipwe, IT IS ALSO obvious---ISILIPWE. Ikumbukwe kuwa WANACHI hawawezi kuwekwa mifukoni na wabunge au Spika, NEVER.
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Without cultivating Rule of Law, leaders will have arbitrary power, and that is what we do not want.... It will cost more the DOWANS
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hata hapa kwetu mahakama kuu iliwahi kutoa hukumu kuhusu mgombea binafsi bunge likaifanyia marekebisho katiba ili kubatilisha uamuzi huo. Labda suala la kujiuliza hapa, ni je marekebisho hayo yalifanywa na bunge lenyewe, au bunge lilitumiwa tu kwa maslahi ya watawala? Naamini hali haiko tofauti hata huko Kenya.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  subiri muone dana dana!
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Dowans yatupwa Bungeni
  Monday, 07 February 2011 21:28

  Habel Chidawali na Israel Mgussi, Dodoma
  SAKATA la Dowans bado linaendelea kuitoa jasho serikali, baada ya Bunge kusema halitaijadili kwa sababu suala hilo liko mahakamani.

  Hoja hiyo binafsi iliwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, kupinga malipo ya Dowans.

  Pia, Bunge limeonyesha wasiwasi wa kutotajadiliwa hoja binafsi kuhusu mabadiliko ya katiba kwa maelezo kuwa, Ibara ya 58 ya Katiba ya Muungano, haielezi kufutwa kwa katiba kama ambavyo wapeleka hoja walivyotaka.

  Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillila, alisema Bunge linatarajia kujadili hotuba ya rais ambayo ina vipengele 13 na maazimio mawili, likiwamo la kubadili baadhi ya kanuni za bunge.

  Kuhusu sakata la Dowans, Dk Kashilillah alisema wanabanwa kujadili kitu ambacho kipo mahakamani na kwamba, tayari hoja hiyo ilikuwa imekamilika kwa kupitia hatua zote.

  "Mheshimiwa Kafulila alikamilisha kila kitu, kwani alileta kusudio na baadaye tukamtaka alete maelezo ya kina na akafanya hivyo, lakini tumekaa na kuangalia kwa mapana kuwa, hoja yake haiwezi kujadiliwa Bunge haliwezi kujadili kitu ambacho kipo mahakamani," alisema na kuongeza:

  "Tena napenda ninyi waandishi muelewe kuwa, Bunge haliwezi kuingilia kitu ambacho kipo mahakamani kama ambavyo, mahakama haiwezi kuingilia kitu ambacho kipo bungeni."

  Alisema ofisi yake ilikuwa imepokea makusudio ya hoja binafsi, likiwamo suala la katiba ambalo liliwasilishwa na wabunge; Anjela Kairuki, Rashidi Mohamed na Machalya.

  Hoja nyingine ambayo imetupwa, ni ile iliyowasilishwa na Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangwala, ya kutaka kuangalia upya mikataba ya madini.

  Dk Kashilillah alisema hoja hiyo iliwasilishwa Dk Kigwangwala ipo kwenye hatihati ya kujadiliwa kwa kile kilichoelezwa kuwa, bado ina upungufu.

  Kwa upande wake, Kafulila alisema hajapewa taarifa rasmi kuhusu kuondolewa hoja yake na kwamba, anachoamini bado hoja hiyo inaweza kujadiliwa.

  Bunge la Kumi katika mkutano wake wa pili, linatarajia kuanza leo kwa kuapisha wabunge sita wa viti maalumu ambao walipitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kabla ya kuanza kujadili hoja ya Spika ya kufanya mabadiliko ya baadhi ya kanuni, baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.

  Pia, utafanyika uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali baada ya kutangazwa na spika, wenyeviti watatu wa kusaidia Spika na Naibu Spika kuendesha vikao vya Bunge na kuunda kwa Tume ya Utumishi wa Bunge.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Katibu wa BungeDk Thomas Kashillilaalisema Bunge linatarajia kujadili hotuba ya rais ambayo ina vipengele 13 na maazimio mawililikiwamo la kubadili baadhi ya kanuni za bunge.

  Kuhusu sakata la DowansDk Kashilillah alisema wanabanwa kujadili kitu ambacho kipo mahakamani na kwambatayari hoja hiyo ilikuwa imekamilika kwa kupitia hatua zote.

  "Mheshimiwa Kafulila alikamilisha kila kitu, kwani alileta kusudio na baadaye tukamtaka alete maelezo ya kina na akafanya hivyo, lakini tumekaa na kuangalia kwa mapana kuwa, hoja yake haiwezi kujadiliwa Bunge haliwezi kujadili kitu ambacho kipo mahakamani," alisema na kuongeza:

  "Tena napenda ninyi waandishi muelewe kuwa, Bunge haliwezi kuingilia kitu ambacho kipo mahakamani kama ambavyo, mahakama haiwezi kuingilia kitu ambacho kipo bungeni." 
  This is a piece of rubbish..........................kazi ya Bunge na ya Mhakama Kuu inabidi zitofautishwe...........siyo kilichoko Mahakamani Bunge haliwezi kukijadili?...........................Bunge lishughulikie masuala ya uwajibikaji na Mahakama ishughulikie uhalali wa kulipa au la....................................................
   
 8. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Bunge kutojadili hoja binafsi ya Dowans

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu Dodoma na Dar; Tarehe: 8th February 2011 @ 08:27

  SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited, limechukua sura tofauti baada ya Bunge kutupilia mbali hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR) ya kutaka lijadaliwe bungeni.

  Wakati Bunge likitoa uamuzi huo Dodoma, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM) amepeleka hoja nyingine, kuitaka Serikali itoe tamko bungeni kuhusu lini hali ya umeme itatengemaa nchini, huku akitaka hoja hiyo itolewe ufafanuzi katika tamko hilo.

  Katika hoja hiyo ya January, alisema "jambo hili likibaki bila maelezo, inaweza kujengeka sura kwamba Serikali ilikosa umakini na maadili hayakuzingatiwa."

  Jijini Dar es Salaam nako wanachama wa CUF, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, waliandamana kupinga malipo ya kampuni hiyo, huku wakitoa mwito wa suala hilo kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri ili Rais apate ushauri wa chombo mahususi kwa kazi hiyo.

  Lakini katika barua ya January, ya Februari 3 mwaka huu kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja yenye kichwa cha habari ‘Taarifa ya Serikali Bungeni Kuhusu Umeme Nchini', anaitaka Serikali kutoa taarifa ikibainisha ni lini itapeleka mahakamani pingamizi dhidi ya utekelezaji wa hukumu ya kuilipa Dowans.

  Hukumu hiyo iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) inalitaka Shirika la Umeme (Tanesco) kuilipa kampuni hiyo Sh bilioni 94.

  "Mheshimiwa Waziri, mnamo tarehe 6 Januari 2011 ulizungumza na waandishi wa habari na kueleza kwamba Serikali inajipanga kuilipa Dowans tuzo iliyoamuliwa na ICC, lakini kwa kuwa mzigo huo ni mzito kwa umma, kumekuwa na fikra, likiwamo pendekezo la Kamati ya Wabunge wote wa CCM kwamba ni muhimu kutumia mianya ya sheria iliyopo kupinga rasmi kutekelezwa kwa hukumu hiyo," alisema.

  Aliitaka pia Serikali iueleze umma kupitia Bunge kuwa ni wanasheria gani waliotumiwa na Tanesco kwenye kila hatua katika shauri la Dowans, kuanzia kwenye ushauri kabla ya kuvunjwa mkataba wa kufua umeme, hadi ushauri baada ya kesi kuamuliwa na kiasi cha fedha walizolipwa kwa kila hatua na utaratibu uliotumika kuwalipa.

  "Ili kuwaondolea wasiwasi Watanzania ambao wengi wao wanaamini Tanesco ilishindwa kesi ya Dowans kutokana na upungufu wa weledi kwa wanasheria walioiwakilisha kwenye kesi, nashauri taarifa ya Serikali ieleze utaratibu unaotumika kuwapata wanasheria wanaoiwakilisha Serikali na Tanesco kwenye mashauri yake," alieleza January.

  Miongoni mwa mashauri hayo ni pamoja na lile lililofunguliwa na Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) dhidi ya serikali na Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kesi za Uwekezaji (ICSID).

  Kesi dhidi ya Tanesco ni ya Oktoba mosi mwaka jana na dhidi ya Serikali ni ya Juni 11 mwaka huo huo. January anataka wananchi waelezwe ni nini hasa kinachodaiwa katika kesi hizo.

  Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah akizungumza juu ya ratiba nzima ya vikao vya Bunge hilo alisema hoja ya kampuni hiyo pamoja na kupelekwa kwa maelezo ya Kafulila, haiwezi kujadiliwa kutokana na Bunge hilo kushindwa kuingilia Mahakama.

  "Kwa kawaida na kwa mujibu wa kanuni, Bunge haliwezi kujadili hoja ambayo tayari iko mahakamani na hata Mahakama yenyewe huwa haina nguvu kujadili hoja inayojadiliwa bungeni, kifupi hoja hii kwa bahati mbaya haitajadiliwa, kwa sababu tayari iko mahakamani," alisema.

  Kwa upande wa hoja ya kuundwa kwa Katiba mpya, Kashillilah alisema hoja hiyo pia haitawasilishwa bungeni hapo kutokana na kukiuka Katiba hasa baada ya mmoja wa wabunge waliowasilisha makusudio yao kuhusu hoja hiyo, kutaka Katiba ya sasa ifutwe.

  Aliwataja baadhi ya wabunge ambao waliwasilisha kusudio lao la kutaka Katiba mpya kuwa ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) na Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (CCM).

  Alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hoja yeyote ili iweze kupitishwa na kujadiliwa na Bunge, lazima ikidhi vigezo ikiwamo kutokiuka Katiba.

  Pamoja na hayo, tayari Serikali imeanza mchakato wa kupeleka hoja bungeni kwa ajili ya kubadili Katiba hivyo hakuna haja ya kuendeleza mjadala huo.

  Kuhusu ratiba nzima ya mkutano wa pili wa Bunge hilo la 10 alisema Spika wa Bunge atawasilisha hoja ya kufanya mabadiliko ya kanuni za Bunge baada ya Rais kubadilisha Baraza la Mawaziri.

  "Pia kuna baadhi ya wizara ambazo zimebadilishwa na kusababisha baadhi ya idara nazo kuhamishwa hivyo kutokana na mabadiliko hayo inabidi Kanuni zibadilishwe na kusaidia uundwaji wa Kamati za Bunge ambazo nazo zinatakiwa kuendana na mfumo wa wizara zilizopo," alisema.

  Aidha, alisema kwa mujibu wa ratiba hiyo Spika wa Bunge atatangaza Kamati mpya za Bunge hilo, kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge ambapo alitoa vipaumbele 13 vya kufanyiwa kazi na kusomwa kwa maazimio mawili.

  "Hakuna muswada utakaojadiliwa, ila mitatu itasomwa kwa mara ya kwanza na kurejeshwa katika mkutano wa tatu wa Bunge hili la 10 utakaofanyika Aprili," alisema.

  Alisema pia kutafanyika uchaguzi wa wenyeviti watatu watakaomsaidia Spika na Naibu Spika na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge.
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Kiutaratibu hoja yoyote ile lazima iende kamati husika kabla ya kuamuliwa nini cha kufanya huyu Makinda ni dikteta na anazuia mijadala ya kitaifa Bungeni................................na wakati umefika wa kuangalia jinsi katibu wa bunge ajira yake iache kuwa ni ya kiserikali na iwe ya kibunge.......................
   
 11. N

  Ndeusoho Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kipindi chote cha nyuma tumekuwa tukipelekwapelekwa hivi hivi. Kwa sasa kuna mwamko wa kipekee miongoni mwa watanzania. Hiki ni kipindi kizuri sana kutuma ujumbe kwa watawala na wale wanaotumiwa na watawala kuwa kila jambo lina mwisho wake. Tatizo tulilo nalo ni kuwa tuna wanafiki wengi miongoni mwetu ambao pamoja na viapo vya uongo wanavyokula hawasimamii haki wala maslahi ya nchi bali wapo kwenye ubinafsi hata kama nchi inaelekea kubaya. Jambo ambalo nawaunga mkono wana JF wapenda haki ni kuwa haya wanayopigania sio kwa manufaa yao bali kwa taifa hili na vizazi vijavyo. Hebu hawa wabinafsi wajiulize hivi wakiondoka leo watakumbukwa kwa lipi kwenye nchi hii? Vipingamizi vyote tunavyoviona leo kuhusiana na mambo muhimu kwa taifa ni kukosekana kwa usafi wa dhamira, nia na matendo miongoni mwa waliopewa dhamana. WanaJF wanaona mbali ndio maana hawavunjiki moyo na hakika Tanzania yenye neema itapatikana tu.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  nilijua tu ni lazi ma watapinga Dowans kutinga bungeni kwa sababu taaarifa zimeshavuja kuwa jamaa walishamaliza kulipwa pesa zao, na baadhi zilitumika kwenye kampeni za CCM, sasa mnataka nini kingine zaidi
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  JK wetu anasubiri vikao vya AU, UN, nk na kuhutubia kwenye sherehe mbalimbali ili kukanusha masuala mbalimbali yanayomhusu! Kusema kweli kwa sasa hatuna Rais, 2015 naona ni mbali sana wandugu!
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  PHP:
  NAchohofia ni kwamba hakuna hata mbunge mmoja awe wa upinzani au CCM ambaye yuko tayari kurudia kufanya kampeni na hata hao akina Kafulila wangeandaa tu hoja ya kutokua na imani na Raisi kwa lapse of duties (Iwaje Raisi aseme hawajui akina Dowans ina maana amesinzia kazini na state machinery yote?) kwa kutofanya au kutii kiapo cha katiba... Speech ya JK Dodoma ni self confension na evidence tosha kwamba Raisi JK amelala na ame-lapse katika duties kwa kuto-protectkuto-defend mali za watanzania na kwa sasa anatafuta mahala pa kutokea...Najua akina Tundu Lisu wanasoma humu labda wazo hili watalifanyia kazi maana inabidi JK aondolewe kinga huko bungeni hata kama ccm ni wengi tutajua ni akina nani walipo bungeni kimaslahi watakokuwa wanamsadia ili asitoke ofisini...
  Spot on.......................................
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  PHP:
  JK wetu anasubiri vikao vya AUUNnk na kuhutubia kwenye sherehe mbalimbali ili kukanusha masuala mbalimbali yanayomhusuKusema kweli kwa sasa hatuna Rais2015 naona ni mbali sana wandugu!
  Kura ya maoni dhidi ya JK inaweza sasa kuangaliwa kama ni muarobaini wa kuachana na huu ufisadi...........................
   
 16. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yap. You are right again.
   
Loading...