Bunge letu Dodoma Kuwa Wakunga wa Katiba Mpya au 'Tahrir Square' ya Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge letu Dodoma Kuwa Wakunga wa Katiba Mpya au 'Tahrir Square' ya Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Feb 7, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  CCM kuwabana Mnyika, Kafulila bungeni


  [​IMG]

  Courtesy of : http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430742
  [​IMG]
  na Mwandishi wetu

  WAKATI mkutano wa 11 wa Bunge ukitarajiwa kuanza keshokutwa mjini Dodoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahaha kuzizuia hoja binafsi za wabunge wa upinzani zisijadiliwe bungeni ili kulinda masilahi ya kisiasa ya chama hicho na serikali yake, Tanzania Daima Jumapili limeelezwa.

  Hoja hizo ni ile ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), inayotaka Bunge lijadili na kutoa mwongozo utakaoweka mchakato utakaowezesha kuandikwa na kuridhiwa upya kwa Katiba ya nchi.

  Nyingine ni ile ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) inayoitaka serikali itoe maelezo nchi imefikishwaje mpaka ikashindwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilirithi mkataba ‘hewa' kutoka kwa Kampuni ya Richmond.

  Tayari wabunge hao kwa nyakati tofauti kila mmoja ameshawasilisha kwenye ofisi ya Bunge taarifa ya kutaka kuwasilisha hoja yake binafsi katika mkutano wa Bunge unaoanza keshokutwa.

  Taarifa kutoka ndani ya CCM na ofisi ya Bunge zinasema chama hicho kwa kumtumia spika wa bunge, Anne Makinda ambaye ni mwananchama wake mtiifu, kimepanga kuizuia hoja ya Mnyika kuhusu katiba kwa kutumia njia kuu mbili; moja ni serikali kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuweka mchakato wa katiba na tume ya kuusimami na pili ni kuwatumia wabunge wake wawasilishe hoja ya Katiba kama Mnyika.

  "Spika atasema hoja ya Mnyika haiwezi kujadiliwa kwa sababu analotaka kuliwasilisha tayari anaweza kulichangia katika muswada utakaowasilishwa na serikali bungeni kuhusu tume na mchakato wa katiba.

  "Pili, watasema kuna wabunge wengine pia waliowasilisha hoja kama yake, sasa tumpe yupi, tumuache yupi….na muda hautoshi kujadili hoja zote na wala kanuni haziruhusu kujadili suala hilo hilo moja kwa hoja nyingi tofauti," alifafanua kigogo mmoja wa CCM kwa sharti la kutotajwa jina lake.

  Kuhusu hoja ya Kafulila itakavyozuiwa, taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, watatumia kisingizio cha suala la Dowans kuwa mahakamani ili kuzuia lisijadiliwe bungeni.

  "Watasema Bunge haliwezi kujadili suala linaloshughulikiwa na mhimili mwingine wa dola (Mahakama)", alisema mtoa taarifa wetu.
  Hata hivyo, akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Kafulila, alisema msingi wa hoja yake ni kutaka kuangalia namna serikali ilivyoshindwa katika kesi hiyo wakati mkataba iliourithi Dowans una utata mkubwa wa kisheria na kwamba suala hilo haliwezi kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mahakama.

  Alisema kuwa mazingira ya kesi yenyewe yanaonyesha kuwa hujuma zimefanywa katika uendeshaji huo ndiyo maana yeye amejipanga kuwasilisha hoja hiyo ili Bunge lijadili na kujua kwa kina kilichotokea kwenye kesi hiyo.

  Alibainisha kuwa Tanzania ilishawahi kuvunja mkataba kibabe na Kampuni ya City Water ambayo ilipokwenda ICC ilishindwa pia lakini katika kesi ya Dowans inaonekana kuna mazingira yenye utata zaidi.

  Alibainisha kuwa Rais Kikwete amekiri Richmond ilikuwa haina uwezo wa kuzalisha umeme hivyo mkataba wake ukawa batili hivyo katika mazingira hayo kampuni hiyo haiwezi kuirithisha kampuni nyingine mkataba usio halali.

  "Hebu niambie Ndugu yangu kuna mwizi ameingia ndani na kuiba vitu, ukamuona na kuanza kumkimbiza, wakati ukikaribia kumkamata anaubwaga mzigo aliouiba, je, hutakwenda kumshitaki kwa sababu ya kuwa hukumshika na mzigo?" alihoji Kafulila.

  Aliongeza kuwa hivyo ndivyo inavyofanya serikali ya CCM ambayo sasa imebanwa katika sakata la Dowans na inaamua kuuacha mzigo huo ili isikamatwe.

  "CCM wamekwama kwa sababu wananchi, wanasiasa tumelipigia kelele suala wa malipo haya ya Dowans, sasa wanatafuta pa kutokea, Kikwete na watendaji wake hawawezi kukwepa kuwajibika.

  Wajiuzulu ili tutafute viongozi na watendaji wengine ambao watakuwa mstari wa mbele kujali matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi," alisema.

  Kuhusu hoja binafsi hiyo kupitishwa na Bunge linaloanza kesho kutwa, Kafulila alisema huu ndiyo mtihani mkubwa kwa Spika Anne Makinda na wabunge wa chama tawala kwa sababu hoja hiyo inagusa masilahi ya taifa.

  Alisema kama Makinda atatumia ufundi wa kanuni kuzuia hoja hiyo basi ajue hasira za wananchi zitakuwa kubwa kwa chama tawala na pia tatizo la umeme halitaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

  "Ninachokifanya mimi ni kuangalia namna tutakavyotoka kwenye matatizo ya nishati ya umeme ambayo tuna mikataba mibovu pamoja na kutokuwa na umeme wa uhakika, wakifanya hila wataumia.

  Alibanisha kuwa Kanuni ya 150 ya bunge, inaweka wazi kuwa Bunge linaweza kuvunja kanuni yoyote kwa ajili ya lengo la kutimiza jambo fulani lenye maslahi ya umma.

  Kama kuna kanuni itakayozuia mjadala wa Dowans itabidi ivunjwe ili kuruhusu hoja hiyo kinyume na hapo mambo yatakuwa mabaya zaidi kwa CCM.

  Alibainisha kuwa sekta nzima ya umeme ina upungufu, hivyo ni wakati mufaka kuweka mfumo utakaoliwezesha taifa kusonga mbele badala ya wajanja wachache kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha.

  "Dowans ni sehemu ya hoja, mambo mengi yanapasawa kufanyiwa kazi, huu ndiyo mwanzo wa kujua mambo mengi," alisema.


  SOURCE: Tanzania Daima.


  HOJA YANGU:

  Mtu yeyote akiangalia vizuri mwenendo wa mambo tangu ratiba yetu ya uchaguzi ukamilike hapa Oktoba 2011 na matokeo kuwa yalivyokua, ni dhahiri kwamba wananchi wa Tanzania tupo kwenye hamaki ya ndani kwa ndani ambayo kulipuka kwake lini na kwa mtindo upi bado hautabiriki.

  Ufisadi, utawala wa kidhulma, madharau, kiburi na kejeli za baadhi viongozi wetu na wale waliokaribu nao yote kwa pamoja na matatizo ya uchaghuzi uliochakachuliwa, ajira kiundugu, na huduma za serikali kwa umma kutolewa kwa misingi ya kiitikadi, mpaka sasa, yametuelekeza kwenye kusisitiza kupata MABADILIKO YA KIMFUMO KWA WANANCHI KUJITUNGIA KATIBA MPYA na wala si kutafuta mabadiliko tu ya sura ya viongozi wapya kuingia madarakani.

  Sasa Bunge letu Dodoma linavyorejea kaini mwezi huu huku mada nzito nzito za wananchi zikiwa ni

  (1) kulitegemea kuanzisha mchakato wa kuandika KATIBA MPYA kupitia bungeni,
  (2) Tume Huru ya Bunge kuchungua Matokeo ya kura za Urais,
  (3) kuundwa upya kwa Tume Huru ya Uchaguzi nchini, na
  (4) wabunge kutekeleza wajibu wake ya msingi kusimamia Rasilmali ya taifa

  ili kutolea msimamo wa kudumu KASHFA YA UTAPELI WA DOWANS, je Bunge hili litafikia mahala kutii kuzaliwa kwa njia ya matakwa rasmi wananchi au watachagua kutekeleza maoni tu ya viongozi wachache na vikundi katika jamii yetu (vikiwemo matakwa ya vyama vya siasa) badala ya maslahi ya taifa??


  Je, wananchi tukipuuzwa tena katika haya madai ya msingi kwa kutumia visingizio vyovyote vile Bunge linawea likachukuliwa rasmi kutekeleza wajibu wa kwa wananchi wa Tanzania au kulielekeza 'Nguvu ya Umma' ijitafutie tu majibu kivyake kwenye 'Tahrir Square' ya hapa hapa nchini kwetu??

  Si ajabu mtu mahala akawa anajifariji kana kwamba wananchi tutakua tumesahau japo ka-nukta.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Courtesy of : http://www.skyscrapercity.com/showthread.php?t=430742

  Mtihani uliopo mbele ya bunge letu safari hii ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote ule.

  Matumaini ya mwisho ya wananchi waliowengi waliojikatalia tamaa na aina ya uongoi tulionao nchini sasa yapelekwa kwa Spika Mama Anna Makinda, Job Ndungai na waheshimiwa wabunge kutolea dira mambo ya msingi ambayo mpaka sasa yameshikiliwa bango kila kona na nchi.

  Aina ya mtihani uliowekwa shingoni mwa kila mheshimiwa mbunge na wapiga kura safari hii, bila kujali chama chake, dini, ubara wala visiwani, ni kutaka kuwapima kwa dhati kabisa na tukapate kujiridhisha kwamba (a) UTII WAO UKO KWA MASLAHI YETU KAMA UMMA TUNAOWACHAGUA AU BORA ZAIDI (2) UTII KWA VYAMA VYAO VYA KISIASA na vikundi vinginevyo tu??

  Hivyo, kwa wabunge wanaoona mbali, wenye matumaini ya kuwekeza katika ubunge wake siku a usoni hana budi kujichagulia sasa hivi kati ya hayo mambo mawili hapo juu. Makosa katika kutumia busara zao kushughulikia vuguvugu inayoendelea nchini huenda ikabadilika kuwa makosa ya kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo.

  Sasa swali langu ni kwamba je wadau wa bunge kama vile (1) Viombo vya habari, (2) Vyama vya Siasa, (3) Wanaharakati, (4) Wasomi nchini (5) Wanafuni vyuoni, (6) Vyama vya Wafanyakazi, (7) Taasisi za Kidini na (8) Wapiga Kura kwa ujumla, ambao kwa bahati mbaya sana walionekana kusinzia katika wajibu wao, safari hii tumejindaa kiasi gani na mmbo ya Bungeni Dodoma huku Taifa zima linapogeza macho na matumaini ya mwisho kupatikana huko????
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Uprising in North Africa: Any lesson for Tanzania?
  Monday, 07 February 2011 00:01

  [​IMG]

  MY CONSCIENCE:Makwaia wa Kuhenga,

  AS I am penning this perspective, the situation in Egypt is ominous as it may, God forbid, lead to civil war.

  Because what began as an uprising participated by people in one voice wishing to see the back of their leader, now the tables seem to have been turned.

  There was reportedly a counter-group supportive of the President of that country now in power over the last three decades. The two groups were confronting each other with stones, molotov cocktail bombs and other weapons at Cairo's Tahrir [Liberation] Square.

  But Egypt could be described as an apex of what could be described as mass action by the populations in Tunisia, Algeria, Jordan and Yemen - an action which is unprecedented in recent history. It had one objective only: throwing out respective governments!

  Tunisia was the catalyst. After nearly a month of popular uprising, the President of Tunisia, Zine El-Abidine Ben Ali (pictured) ran away to Saudi Arabia on January 14, 2011.

  Never in recent memory have a people with an iron will for change forced out a government with bare hands in a protracted uprising.

  In the past, people elsewhere have taken up arms, and organized in guerilla warfare. But this is a new phenomenon – mass demonstrations and marches on a daily basis to achieve the same results!

  Already, there have been significant results. In Yemen, the leader there has said he will not stand again for re-election. In Egypt, President Mubarak has said he will not seek re-election but will stick on until new elections in September.

  But at issue here is not whether he will leave power or not; at issue is his sense of responsibility to his people. Does he give the impression as sufficiently responsible not to create another problem to his people?

  The prospect of a civil war, which is enticed at the launch of this perspective, is the worst prospect any responsible leader would wish for his people.

  The question to ask is: Are these lightly armed people we had seen on television reportedly "supportive" of him as spontaneous as the earlier massive crowd of men, women and children we had seen for a whole week?

  Who put or organized the latter group into action? These are the worrying questions that the international community and friends of Egypt must be addressing themselves. (1) The prospect of pitting one's own people against another for the sake of clinging to power is, to say the least, most criminal.

  But Egypt is for Egyptians. It will be the Egyptians people who will sort out themselves. What is relevant for the rest of us in the developing world or Third World is what lesson we pick from this uprising in North Africa and the Middle East.

  A read of the developments in these countries in North Africa and the Middle East point to (2) various factors as the root cause. Among which is a restive unemployed youth, poverty, a lootocracy and an aristocracy.

  Now since there is a saying in Kiswahili, inter alia: Ukimwona mwenzio ananyolewa na wewe kimbilia maji na sabuni loweka nywele zako! [When you see your compatriot getting a shave, quickly get ready by applying water and soap to your hair (3) it is both urgent and important to take a hard look at our landscape here.

  If one wants the truth, it is a truism that just like the restive youth in North Africa, the Middle East and elsewhere, (4) we have a serious, if not a very serious problem of rising unemployment in this country.

  In fact thousands if not millions of able-bodied young people are roaming about in urban areas doing nothing but hawking all sorts of goods, which are mostly foreign-produced.

  But the leadership is looking away or (5) pretending all is well – comforting itself with that empty and meaningless political jargon of "maisha bora kwa wote" [good life to all!] Nobody is worried of the fact that this country is actually sitting on a powder keg or time bomb.

  Just take a bus ride or drive your car around Dar es Salaam or just to Morogoro around 200 km away. You will be shocked. These young people will invade your car or bus – all selling one thing – bottled water or cashew nuts; none of which few want to buy – or simply look away!

  "Mzee, nunua hata kipaketi kimoja nipate hela ya kula" [old man, please buy off me so that I can eke a meal! these otherwise able-bodied youth would beg you.

  This is just one among the many problems which have been compounded by the leadership's full blanket embrace of a market force economy.

  Although we (6) seem to have resolved the problem of aristocracy, thanks to the current Constitution that sets the limit of a presidential term, we seem to have learned nothing from the leadership example of the founding father of this country, Dr. Julius Nyerere.

  (7) Mwalimu Nyerere allowed no NGO to be run by neither his spouse nor his children to run for political office when he was still in power.

  Much more, there was a (8) leadership code binding leaders not to confuse business with public office. Are these values still present with us? (9) Are we free of a lootocracy? Then what are all these noises about Messrs.

  Dowans and Richmond? Let the powers that be watch-out from what has happened in North Africa!

  HOJA YANGU:

  Kwa mtaji wa maswala mbalimbali ambayo Mzee Makwaia wa Kuhenga aonekana kuibwa hapa, ikiwa ni sehemu tu ya mengine mengi ambayo vijana tunayalalamikia pasipo kusikilizwa wala kutiliwa manane na chombo chochote nchini licha ya dhuluma na ufisadi kila kona ya taifa letu, kuna uwezekano kweli mtu yeyote atakua anajifunza kitu huko serikalini na hasa ndani ya CCM au??

  Mambo anayoyazungumzia wa Kuhenga bado yanaturudisha kule kule kwenye swali hapa bado kwamba je VIJANA JAWABU SAHIHI YA MATATIZO YETU bado tuyatarajie kutoka Bungeni Dodoma safari hii huenda wakatekeleza matakwa ya umma au ni matakwa ya viongozi ndio yatakayoendelezwa kama miaka yote ili sisi wengine majibu tukayatafutie kwingineko tu??

  Wana-JF sisi wenyewe tunajifunza nini toka huko kaskazini mwa bara letu??
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  SOURCE: African project showcased in Poland | BiztechAfrica - The African ICT News Portal

  Bunge lilivyoanza mjini Dodoma leo; kila mwananchi kichwani swali ni kwamba je hiki chombo muhimu KIKATIBA kutoa maamuzi na kusimmia rasilmali zetu kwa mustakabali mzima wa taifa letu SAFARI HII HUENDA KIKACHEZA NAFASI YAKE STAHIKI KAMA CHOMBO CHA WANANCHI kutokupingana na matakwa ya Umma kuhusu uandikwaji wa KATIBA MPYA bila udali wowote??

  Kama kuna chombo ambacho wananchi hatutaki kukiona kikiingilia mchakato mzima wa wananchi kuandijiandikia upya katiba, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, bila kuingiliwa na TAASISI YA URAIS / IKULU ambao kikatiba ni wtendaji tu na wala hawahusiki na utungaji wa sheria?

  Ni matumaini yetu sote kama taifa kwamba Bunge letu litaona sababu a msingi kabisa tena kwa udhati mkubwa kutuokoa na ile sura isiyopendeza sana ya Mubarak KULAZIMIKA kukubali mabadiliko makubwa sana, kibao ndani ya hali ya purukshani ndani ya nchi yake kule Misri huku jasho likichuruzika ovyo kutokana mabano makali kupindukia ya 'Nguvu ya Umma'.

  Kila mmoja akumbuke kwamba sisi kama nchi hatuna KINGA MAALUM ya kujikwepea nayo dhoruba za alichokiita majuzi Mama Clinton kama 'A PERFECT STORM OF CHANGE' (Dhoruba za Kimbunga Cha Mabadiliko Kwa Mtazamo wa 'Nguvu ya Umma') inayoendelea hivi sasa kuabisha watawala madikteta, mafisadi na dhalimu kote duniani.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,177
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tofauti zetu ni kubwa mno kuungana...

  Baya zaidi hatutaki kukubali tuna tofauti (pretending)...
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni viongozi wetu tu mafisadi ndio wanaotofautiana KATIKA KIPIMO CHA RUSHWA WATAKAOOPOA KWETU ila sisi wananchi wa hali ya chini, kama ulikua hujui, tuko pamoja zaidi ya Jeshi la Siafu.

  Walalahoi wa Tanzania, kama hali halisi ilivyokwishajionyesha kwingineko duniani penye mageuzi ya kwali kupitia 'Nguvu ya Umma', tumenganishwa zaidi na zaidi na UMASIKINI WETU WA KUPINDUKIA nchini kwa kiwango ambacho hakuna alama yoyote ya KIITIKADI itakayotupangua msitari safari hii mpaka kieleweke!!!

  Vita mbeeelle, uzalendo wa hia nayo mbeeele kama tai!! Atakayekatisha vibaya mbele ya Nguvu ya Umma huko Bungeni Dodoma shauri yake atajilaumu mileele!!! Safari ndio hiyo imeanza na kwa dhoruba zote endapo hakuna wa kutusikiliza na kuendelea kupuuzwa hapa.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Anti-government protesters sit and lie inside the tracks of an Egyptian Army tank Photo: AP

  3:24PM GMT 07 Feb 2011

  SOURCE: Egypt crisis: demonstrations continue amid government talks - Telegraph

  UJUMBE HAPA:

  Kwa mtaji wa azma ya Nguvu ya Umma kwa kiwango hiki, hata mizinga kamwe HAIWEZI KUUA WAZO LA MABADILIKO YA KWELI tunavyotaka sisi wananchi ila tu waweza wakaua tu miili yetu.

  Wazo la mabadiliko na mchakato wa KATIBA MPYA mbeele kama tai!!!
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Janja za nyani zilizoanza kule Bungeni Dodoma itakutana na nguvu kubwa haijapata kuonekana nchini kwa miaka mingi!!

  Kama si mzaza tu wa kutaka kuchezea Nyuvu ya Umma na azma yetu kama ambavyo tulivyowaagiza waheshimiwa wabunge wote huko basi huenda ikawa KIBERITI NA PETROLI kwa hao watu wanaoanza kubadilisha KANUNI ZA MCHEZO wakati tayari timu ziko uwanjani.

  Wapenda mabadiliko wote walioko ndani na nje ya Bunge kamwe hawataruhusu GHILIBA hata tone. Masiki kumbe utulivu wetu huu ndani ya takribani wiki 3 CCM tayari walishachukulia kwamba mambo yamekwisha na kwamba MAZOBA WAO TAYARI USINGIZI TUMEANZA KUUCHAPA???

  Ni makosa makubwa mnooooo!!!!
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  [​IMG]

  Mr Slaa, who campaigned on an anti-corruption platform last year, is among those detained

  [​IMG]

  Opposition Calls for New Constitution in Tanzania
  Police dispersed hundreds of opposition supporters who were yesterday planning to demonstrate...

  MY TAKE:

  CCM ujumbe wenu mliotutumia kule bungeni Dodoma kwa kuanza tena KUCHAKACHUA KANUNI NA TARATIBU ZA BUNGE wenzenu tumeusoma na bado tunawaachieni siku za kuwasomeni zaidi kujua lengo leni ni kuua matakwa yetu Nguvu ya Umma kama tulivyoagiza huko Bungeni au vipi??

  Tunaendelea kuwafuatilieni nao kumbe sauti zetu hazijaeleweka kwenu bado kutaka KATIBA MPYA bila ghiliba zozote kama hizo mlizoanza nazo leo. Na katika hili wewe 'Mtoto wa Mkulima' na Spika kamwe hatutowaelewa .

  Mambo ya kuwatisha baadhi ya wabunge nayo kwa kuvunja kinga ya bunge na kujipenyeza kumpelekea barua ya mahakama ili kumnyamazisha nayo pia tunalitazama. Wanaharakati na watetezi wa Haki za Binadamu na nyinyi pia tunamatumaini ya kwamba mambo haya ya ajabu ajabu ya CCM ndio hivyo yameanza.

  Waheshimiwa, Msidanganyike na African Union wala nini, hapa haki ya wananchi kamwe haipotei!!!!
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MCHEZO WA CCM ICHAKACHUE KANUNI NA TARATIBU ZA BUNGE
  HALAFU WAPIGANAJI WANAPOPINGA BASI BAADHI YETU HUGEUKA KUWALAUMU
  BADALA YA KUILAUMU CCM KAMWE HAIKUBALIKI


  [​IMG]tz.jpg

  595 × 300 - Police clashed with Chadema party supporters in Arusha, Tanzania on news2.onlinenigeria.com


  Uliwahi kuona wapi TARATIBU ZA MICHEZO zikibadilishwa mara tu baada ya Timu kuingia uwanjani kuanza kucheza kabumbu?? Hizi ghiliba za CCM na nyingine nyingi ambazo ziko njiani kamwe hazitovumilika na WAPENZI WA DEMOKRASIA.

  Na tunaamini kwamba hata wale watu ambao wako kwenye usingizi mzito, ambao mnanufaika na dhuluma na ufisadi wote wa serikali ya CCM, nanyi pia hivi karibuni mtazinduka tu.


  Hili la mtu kudhulumiwa halafu mdhulumiwa kuendelea kulaumiwa anapoamua kupiga mayowe, Ndugu Msando Alberto, ni utaratibu wa zamaaani ambao wengi tulishausahau kabisa.

  Tunawapa pole sana wale walijipandia Jahazi la 'Amani na Utulivu bila HAKI'!!!
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  [​IMG].

  Mama Makinda, safari hii taifa likitetereka shauri ya wewe kuruhusu CCM kupenyeza ujanja ujanja wa kila aina hapo Bungeni basi moja kwa moja ukae ukijua kwamba Watanzania wenzako kilio chetu tutakielekeza kwako na kuingia nayo katika historia ya taifa letu bila kukwepa.

  Kuna kipindi tutawataka majibu kama matakwa ya Mafisadi ndio muhimu zaidi kwa bunge letu au maslahi ya umma.

  [​IMG]
  cc Julien Harneis


  [​IMG]
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Bunge laanza kukata makali ya Chadema
  Monday, 07 February 2011 21:37 Waandishi Wetu, Dodoma[​IMG]Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe  KAMATI ya Kanuni ya Bunge jana iliridhia mabadiliko ya kanuni kwa kufanya kambi rasmi ya upinzani kubeba vyama vyote na sio Chadema pekee.

  Hatua hiyo ya Kamati ya Kanuni tayari imelalamikiwa na Chadema kwamba ina lengo la kukidhofisha chama hicho.

  Katika kikao leo Bunge leo linatarajia kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni ikiwamo ya tafsiri mpya ya kambi rasmi ya upinzani.

  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kamati ya Kanuni ambayo pia Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe alihudhuria baada ya mabadiliko hayo, kamati zote za kudumu za usimamizi wa fedha zitagombewa na vyama vyote vya upinzani.

  Lakini, jana Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri ya Chadema, John Mrema wamepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda inayoeleza nia ya Bunge kuondoa neno kambi rasmi ya upinzani bungeni ili kufanyia marekebisho.

  "Tumepata taarifa kuwa Spika wa Bunge kwa kutumia nyongeza ya (8) ya kanuni chini ya kanuni ya 115 "kamati za kudumu zisizo za sekta" kifungu cha 3 (1) kinachompa mamlaka ya kuunda Kamati ya kubadili Kanuni za Bunge aliunda kamati hiyo yenye lengo la kufanya marekebisho ya Kanuni za Bunge,"alisema Mrema.

  Mrema alisema Chadema kimegundua kuwa miongoni mwa sababu za kuundwa kwa kamati hiyo ni kutaka kufanyia mabadiliko kipengele hicho ambacho kitapunguza nguvu ya upinzani bungeni na zaidi nguvu ya Chadema ambacho ndicho chama chenye sifa za kusimamia na kuhoji Serikali.

  Alisema kwa mujibu wa utamaduni wa mabunge ya Jumuiya za Madola, chama kikuu cha upinzani ndicho chama mbadala wa chama tawala na kina sifa za kusimamia na kuhoji Serikali juu ya mambo mbalimbali hasa kwenye kamati tatu za Bunge zinaofahamika kama Kamati za Kudumu za Bunge.

  Kwa mujibu wa kanuni za sasa, wabunge walio nje ya kambi rasmi ya upinzani bungeni hawaruhusiwa kuingia na kuongoza kamati hizo tatu za Bunge ambazo ni za mashirika ya umma, serikali na mitaa na ile ya hesabu za serikali.

  "Mara baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika wa mwaka 2010, Chadema tulipata wabunge wengi ambao walikiwezesha chama kuwa na haki ya kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kifungu cha 14 kifungu kidogo cha 3,"alisema Mrema.

  Mrema alifafanua kuwa mabadiliko hayo ya kanuni yanafuatia barua ilioyoandikwa na vyama vingine vya upinzani vikiongozwa na CUF kwenda kwa Spika na kutaka neno kambi rasmi ya upinzani bungeni lifutwe.

  Alisema lengo la vyama hivyo ambavyo kwa sasa havikuwa na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bungeni na havikushirikishwa kwenye kambi iliyoundwa na Chadema ni kutaka kuwa na haki ya kuunda umoja wao unaojulikana kama minority camp.


  Wakati chama hicho kikitoa maelezo yake hayo habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya vikao vya vyama vya siasa na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge zilisema kuwa moja ya kanuni zitakazorekebishwa ni ile inayotambua uwepo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

  Kanuni hiyo inatoa nafasi kwa chama cha upinzani kinachofikisha asilimia 12.6 ya wabunge kuwa kambi rasmi ya upinzani ambapo kwa sasa ni Chadema yenye wabunge takribani 70.

  Hali hiyo iliviacha kando vyama vingine vya CUF, NCCR, TLP, UDP vyenye wabunge wachache vikilalamika kutoshirikishwa katika kambi hiyo hivyo kuzua mvutano vikiitana kuwa na kambi yake ndogo ya upinzani.

  Iwapo mabadiliko hayo yatatokea vyama vya upinzani vitakuwa vimefungishwa 'ndoa' ya lazima baada ya kulumbana kuhusu nafasi ya kambi yao.

  HOJA YANGU:


  1. Mama Anna Makinda anatafuta kubadilisha kanuni ya Bunge kulaziisha CUF kujiunga na CHADEMA Kambi Rasmi ya Upinzani KWA MASLAHI YA NANI???

  2. Chama Cha CUF, kama ingalikua ni kule gerezani angelitazamwa KAMA BINADAMU MWENYE JINSIA ZOTE MBILI (moja ya kike na nyingine ya kiume - Hamerphrodite). Hivyo wakati wa kulala kwanza CUF kingetengwa kwenye Chumba Cha peke yake mpaka wataalam wa tiba waje wabainishe wazi kwamba ni jinsia yake gani hasa inayofanya kazi na lipi limelala ndipo uamuzi wa kupelekwa kwenye gereza la watu wa jinsia gani inpotolewa.

  Kwa mantiki hiyo hapo juu kisiasa hapa nchini CUF inajinsia ya CHAMA CHA UPINZANI ua chama hiki kina jinsia ya CHAMA TAWALA??? Kamwe wananchi hatuwezi kuwaruhusu kuchezea demokrasia yetu jinsi mpendvyo nyinyi wenyewe hapo.

  Haikubaliki kwa man tiki zote KIDEMOKRASIA kwamba katika siku moja ambapo vikao vya bunge la Zanzibar na hili la Muungano vinapoendeshwa basi CUF kihudhuria visiwani KAMA SERIKALI ndani ya taifa la Tanzania na pale unapoteremka tu ferry kwa Bakhresa sasa CUF ni Chama Cha Upinzani ... no way!!!

  CCM ilivyobagua vyama vingine nchini katika mazungumzo / muafaka wa Maalim Seif na Makamba kule visiwani bila kupiga darubini mbele kuona UTATA WA KISHERIA kutekelezwa kimuungano, sasa wanywe tu walivyolikoroga. Waunde serikali yao ya muafaka hadi huku bara CUF kukaa upande mmoja bungeni na CCM - hilo halina mjadala.

  3. Haki ya CHADEMA kuchagua vyama vya kushirikiana navyo bungeni ni sharti iheshimiwe kwa kila hatua sawa sawa na jinsi ambavyo CCM kilivyojichagulia kushirikiana na CUF Visiwani na kuviacha vyama vingine vyote nchini nje ya uhusiano huo.

  4. CUF kilipopata nafasi kama hii wala Hamad Rashid hawakulazimishwa wala kuchagua kushirikiana na CHADEMA; kulikoni leo???

  5. Kafulila amapogeuka na kubeza CHADEMA kutimiza sifa za kuwa chama rasmi ya upinzani bungeni inamaana katumwa na nani???


  SHERIA ZA NCHI KUANZISHA VYAMA VINGI NA KANUNI ZETU ZA BUNGE ZIHESHIMIWE KWA KILA NUKTA NA HERUFI WAKATI WOTE!!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  HISIA ZA WATANZANIA JUU YA NJAMA ZA CCM NA CUF KULA SERIKALINI, NAKO KAMBI YA UPINZANI WAKALE WOA, NA HATARI YAKE KUTUREJESHA KIMTINDO KWENYE MFUMO WA CHAMA KIMOJA KA MAJUTO YA WALAHOI NCHINI:

  +1 #49 mwanamapinduzi 2011-02-08 21:22 mwanamapinduzi chadema ndio cha tunachotegemea sisi wananchi kupata mabadiliko wengine wengine hao ni vibaraka ndugu zangu msikate tamaa sisi chama chetu lazima tushinde hawa wameshinda na kuona siasa inawashindinda sasa wanataka kupunguza makali lakini hawatuwezi
  Quote

  +1 #48 mwanaharhkati 2011-02-08 21:08 mfa maji haachi kutapatapa. ccm maji imeshawafika shingoni wanatafuta wa kuwashika mkono. CHADEMA moto uleule msikubali kubadilisha msimamo. kafu wa kosa jipya.
  Quote

  +1 #47 Mtanzania 2011-02-08 20:29 Hivi katika bunge lililopita, CUF si walikuwa ndo kambi rasmi ya upinzania wakishirikiana na UDP, na hawakuwashiriki sha CHADEMA, sasa hii ya CUF kutaka fungamano na wanamageuzi wa kweli imetoka wapi? Hivi si Cheyo waliyeungana nae aliyepinga hata maamuzi ya kambi ya upinzani na wao hata wakamwadabisha? Nani niposu sana katika hili hata asipone kuwa CUF ni mamluki wa CCM? Dawa yao si mbali tutakapoikomboa TZ kutoka kwa makucha ya mashwahiba wao CCM ndo mtatueleza kama mawe yakipikwa yanaivaga na kuni zikabaki!!!
  Quote

  +1 #46 rts 2011-02-08 19:01 wewe timoth inaonesha kiasi gani ulivyo kiazi,nani kakwambia ukubwa wa nchi na watu ndo maendeleo,india ndo nchi masikini kutokana na population.israel ndogo kuliko zanzibar na wanaiongoza dunia nzima,usiropoke ,zanzibar wakipata viongozi safi ndani ya miaka 5 inaweza kutoka kwenye third world country.kutoka na population ndogo.
  Quote

  +1 #45 swry 2011-02-08 17:58 hata Mungu amechoswa na uchafu wa ccm. 2ko nyuma yenu, msikate tamaa. hawa wezi mwisho wao umefika.halafu huyo spika naona amekula yamini kuwa hatawapa nafac . ya kuongea. nataka waelewe kuwa nyie ndo cc. mckubali kuunyimwa haki zenu. na kama hawataki kuwackiliza coni faida ya ninyi kukaa kama wackilizaji. mmefanya vizuri kutoka. onesheni mcmamo. GOD B WITH U.
  Quote

  +2 #44 WA MLIMANI 2011-02-08 17:05 Jmani hivi hawa CUF hawajui kama ccm yafa? naona wanajipendekeza sana bila hata kujua sasa sisi Watz twakichukia cuf pia. Mwanzo tulifikiri ni wapinzani tukawaunga mkono sasa hivi wao ni mdebwedo tu. Hamad Rashid kwa kutaka kwako madaraka sasa unaamua kuiua cuf kabisa. Sawa wacha tuone
  Quote

  -5 #43 amriK 2011-02-08 15:44 Jamani CHADEMA NI WAOGA WANAOFIA WATAMEZWA KAMA TANZANIA INAVYOOFIA KUMEZWA KWENYE JUMUHIYA YA AFRIKA MASHARIKI. SASA HIVI KINACHOTUPELEKA NI UKABILA NA UDINI KAMA ALIVYOSEMA ZITO KABWE. HAMTUPATI. KUSEMA KUWA LEBANON, MISRI, NA TUNISIA SIKUBALIANI KWANI BAADA YA HAPO VIONGOZI WAPYA WAKIPATIKANA HALI NDIO ITAKUWA TETE ZAIDI DUNIANI. WATANZANIA SOMENI NYAKATI
  Quote

  -2 #42 Chuma Ulete Zanzibar 2011-02-08 15:08 Chadema lazima isimame Imara,vuguvugu la tunisia na Misri,Syria, Lebanon yamewaumiza Waislam wa Bongo na sasa wanaona Aibu.inabidi sasa hata uovu huu wa Serikali ya JK wauchunie maana wanaamini wakubwa wao waliotarajia wajiunge OIC wawapige Tafu Wamepigika kuliko hata wao wenyewe(waislam wa bongo),So huwezi omba jamvi msibani,kelele zote za OIC kushne mwanawane,Tujag e mwanawane!!!
  Quote

  -1 #41 MK KUWAKA Ltd.ZBAR 2011-02-08 14:58 Hamad RASHID,Huo ndo Uislam Safi kweli kuhujumu mageuzi, au kwa sababu CCM sasa ni chama cha waislam? Ndo unaamua kuua upinzani kwa sababu unapinga Uislam(CCM)?Wewe uliishawishi kanuni hiyo sasa leo haifai?Halafu nyie Vipago CCM inamaana Hamadi ndo Spika anaamua kila kitu kudadeki.Leo akiomba kubadilisha kanuni za Bunge Makinda uwe Rais na JK awe Redio inaonekana mtakubali.Hata maandamano sasa ni halali kwa CCM na CUF wao hawapigwi mabomu kabisa,Huu ni Usenge na unamwisho tu kudadeki
  Quote

  -1 #40 ANN 2011-02-08 14:11 ChADEMA SONGENI MBELE SISI TULIOWACHAGUA TUNA TAKA KUONA KAZI HAO WAMEANZA KUTAPATAPA LAKINI SI TUKO PAMOJA NDOA YAO NA CHAMA TAWALA NDO INATUCHANGANYA. KWA VILE MKO MAKINI TUNAJUA MAMBO YATAENDA TU HATA WAKILAZIMISHA KUUNGANA NA NINYI
  Quote

  SOURCE: http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/9105-bunge-laanza-kukata-makali-ya-chadema .
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  +3 #39 Timothy 2011-02-08 14:07 Msuguano wa Vyama vya upinzani unaashiria nini?
  Kwa kifupi ni mwisho wa Chama tawala. Wana CUF wanashindwa kusoma alama za nyakati wanapeleka mapendekezo ya kudhoofisha upinzani ili hali nao ni wapinzani. Watanzania tunajua kwani sisi ndio waajiri wa hawa wanasiasa na mwisho wao unakaribia. Kwa upande wa Bara CUF hakina nguvu yoyote na kwa visiwani kimeshakuwa CCM B. Hawa si wapinzani tena kwani wana KATIBA yao na Serikali yao ambayo haihusiki na sisi wa Bara. Kwanza Unguja na Pemba ilitakiwa iwe Mikoa miwili hata mmoja kwani havina sifa ya kuwa nchi. Wapiga kura wote wa Zanzibar hawafikii wapiga kura wa Mikoa kama Rukwa au Mara. Chadema acheni kulumbana na mamluki tengenezeni sera imarisheni chama ngazi za Chini msisubirie kampeni ya siku 70. Wananchi tunajua nani wa kumchagua. Tupange na mikakati ya kutoibiwa kura mwaka 2015. We need a CHANGE.
  Quote

  -1 #38 Mahumbu Netu 2011-02-08 14:04 Kweli mage unaendelea 'KUPREY FOR YOU CHADEMA'INAONESHA NI JINSI GANI 'USISI'ulivyokukaa kooni na wenzio mnaojiita CHADEMA.Tupo hapa hila zenu chafu mlizozificha zitazidi kugundulika na viongozi wenu wa dini na udini usio na macho.Quoting margareth:
  tupo nyuma yenu chadema na zaidi we prey for you ili muendelee kufichua maovu. hatukustaili kuwa kama tulivyo sasa tanzania.​
  Quote

  +1 #37 konambaya 2011-02-08 13:53 CHADEMA NAAMINI NDIO CHAMA PEKEE KINACHOWEZA KULETA MABADILIKO SI VYAMA VINGINE AMBAVYO VINAONEKANA KUWA MAKADA WA CCM CUF,NSSCR NA UDP NDIO MWISHO WAO KWANI WANANCHI TUNAONA KINACHOENDELEA WANATUMIWA NA CCM KUIDHOOFISHA CHADEMA ILI CCM IENDELEE KUFANYA UFISADI,

  WOSIA: CHADEMA INGIA BUNGENI CHAPENI KAZI KISHA NJOONI KWA WANANCHI TUPO PAMOJA KWANI HUWEZI ZUIA MVUA KWA MIKONO

  MAKINDA: TUNAKUSIKITIKIA SANA MAKINDA MAANA BADALA YA KUTUINGIZIA HOJA ZA MAANA ZA KATIKA MPYA NA DOWANS UNAINGIZA UCHAFU WA KUTUPANDISHIA HASIRA WANANCHI DHIDI YA CCM CHAMA CHAKO CHA MANYANG'AU. WE WILL TEACH URE CCM THE LESSON 2015 WEWE ENDELEA NA MADUDU
  Quote

  +1 #36 PMN 2011-02-08 13:50 Hakuna asiyejua kuwa Hamad Rashid ndiye aliyeshinikiza Bunge mwaka 1995 kuunda Kanuni inayotambua KAMBI RASMI ya Upinzani Bungeni. Na Leo tunashuhudia anavyotumia hoja za nguvu badala ya nguvu za hoja kufuta kile alichokiamini miaka 10 iliyopita. Huu ni uchu wa Madaraka wa CUF uliokithiri. Sitashangaa, kama muujiza ukitokea, mwaka 2015, kama CUF wataongeza idadi yao ya wabunge, hapo Hamad Rashid atakuja na hoja ya kufuta tena anachokiamini leo. U[NENO BAYA] huo!!
  Quote

  +1 #35 albert 2011-02-08 13:45 Nashanga na hivi vyama vingine vya upinzani. CUF,NCCR,UDP, ni kwa nini hamwezi kuangalia nguvu zenu na muziangalize Kwa kile chama chenye nguvu na uwezo mkubwa.malumbano ya nini.kama kweli mnataka kelekeza nguvu zenu kuleta maendeleo kwa watanzania sasa hivi ni kuonyesha nguvu zenu zinaelekea upande mmoja siyo,CUF kuelekeza kushoto, UDP kulia,NCCR Magharibi,CHADE MA kaskasini.Kama kweli mmeamua kuleta mabadiliko kwa watanzania toka sasa mjipange kwa pamoja kuanza vita vya mapambano ya kujenga tanzania.Watanzania wanataka amani na wanataka kuona vile mtamaliza wafisadi msiwaonee huruma kabisa.Tamaa hazijengi nchi, ila kwa pamoja kama mtaweka masilai ya watanzania waliowapa kura zao na kile mlichowahahidi wakati wa kuomba kura sasa wanataka kuona mapambano yenu ya maendeleo.Tunanwatakia kila la heri na mema kwa watanzania.
  Quote

  -1 #34 BISHA 2011-02-08 13:44 Tunawaomba CHADEMA wasiungane kabisa na CUF sio kwa ubaya wala nini kwa sababu CUF walishaungana na CCM na kuongoza serikali. Sasa lazima kuwe na chombo cha upinzani cha kuwakosoa wao na serikali yao.

  Na tunaomba SPIKA aweke wezi hiyo siri ya CUF na CCM sio kusema CUF ni wapinzani tu. Sisi hatuwaelewi hawa CUF wapo upande gani mpaka sasa wao wanajipeleka kama mpira usiokuwa na refa. Wanacheza ilikufurahisha watu sio washabiki, wafunge wasifunge mradi wapate vyeo. Upande wa CCM wameweka goli kipa na upande wa upinzani wanaweka goli kipa sasa watafunga upande gani hao wachezaji kama sio kudanganyana tu ndugu zanguni watanzania.

  Ni afadhali hata mpira wa makaratasi wa watoto unaingia goli na wanahesabi goli kuliko ngonjera za hii CUF. Wabunge wa CHADEMA msife moyo Endeleeni kuwakosoa hata kama mtakuwa nje ya hiyo kambi yao jengeni hoja, tena mtakuwa na uhuru wa kuyapasua majipu vizuri zaidi, ham[NENO BAYA]sa watu wa kuwaunga mkono hata baadhi ya hao wabunge wa sisiem.
  Quote

  0 #33 Henry 2011-02-08 13:29 Jamani ifike wakati tuwe na akili tambuzi,unapose ma CUF chini ya uongozi wa viongozi wao ni chama cha ukweli ktk upinzani nashindwa kuelewa.Utapo turejesha Zimbabwe sijui kama unajua huo muungano ulizaliwaje nikuongezee na Kenya pamoja na hiyo Zanzibar.Ina maana chama kili[NENO BAYA] madarakani hakipaswi kushindwa na kikishindwa tu kinalazimika kuunda serikali ya umoja? Hawa CUF na R.Hamad wao mbona hawakutoa ombi hilo walipokua wakiiongoza kambi hiyo kwa misimu miwili yote hadi sasa wanapoonekana kuikosa nafasi hiyo? Sasa kati ya hawa wawili nani mloo wa madaraka kama siyo kwamba anatumika? Hivi kweli unaweza wewe ukajitofautisha kwa kuukana uafrika na kudai kuwa wewe ni mtanzania tena wa asili.Eti CUF ni sehemu ya serikali Zanzibar tu na bara ni chama pinzani.Hivi bunge la Jamhuri linawakilisha mambo ya bara tu ama na Zanzibar ikiwemo,ama wazanzibar hawahudhurii bunge hili?Kama kweli utafikiri sana jibu utalipata hata kama usipolitoa hadharani.
  Quote

  +1 #32 USONGO 2011-02-08 13:09 Wabunge wa CHADEMA msipate shada ya kuhangaika nao mtasumbua muda wenu bure. Hudhurieni bunge, toeni hoja zenu zilizopo kama kawaida.

  Rudini kwa wananchi waachieni waendelee kuchakachua ndio wanaendelea kukiimarisha CHADEMA zaidi hakitakufa. Wananchi wanataka kuona upinzani sio vigeugeu. Tunajua CUF ni CCM B na akina NCCR, UDP NA TLP wanataka kuwasambaratish a.

  Kuweni na msimamo wenu wa kujenga hoja tu. Waache waendelee kuvurunda kwani hali si wanaiona watasaliti amri wenyewe. Tunafuatilia sana jinsi wanavyowanyanya sa. Hatuoni sababu ya SPIKA kuingilia suala lenu la kambi ya upinzani. Huo ni udikteta, uonevu usiovumilika na jinsi hawa CUF wanavyo penda madaraka.

  Mazingira yanayotengenezw a ni kama yale ya ARUSHA ya kuvurugavuruga ya umea na udiwani. Na wanajua nyinyi na tushio waache wagawane hayo madaraka yatawatokea puani.
  Quote

  -2 #31 peter mtuli mhaui 2011-02-08 12:32 Nimesoma vzuri na nimewaelewa watu waliotoa coment zao. watanzania wanashindwa kuelewa siasa ya sasa hivi duniani ipoje. CUF hawana makosa. na Maalim SEIF wa CUF ni Mpinzani wa kweli kwani alimkosoa Myerere Hadharani naweza kumfananisha na Mandela wa Afrika ya kusini kwani Mbona wameungana baada ya kuteswa. Kosa ni la Chadema wanakurupuka. jamani angalieni Zimbabwe. ulimwengu wa sasa ni Tofauti. Chadema kaeni pamoja, acheni uroo wa uwzili vivuli. sasa hivi sias hizo hazipo. unagneni kwa maslahi ya Taifa. nani ajui kama Bila ya Tume Huru upinzani hawapati nchi? CUF wameshinda mara ngapi hawjatangazwa? CHADEMA,CHADEMA ... CHAMA MNAKIUA...NAAMINI KAMA ANGEKUWEPO NOB MAKANI YASINGEKUWA HAYO.
  Quote

  +1 #30 abuuahmad 2011-02-08 12:25 Kiboko ya kifungu ni kifungu...
  Quote
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  +2 #29 Honorable 2011-02-08 12:24 Chadema msihangaike na Anna Makinda, Cuf na CCM yao; tuendelee kujenga hoja za kuwapa wtanzania matumaini na mwelekeo mwema wa nchi yetu; kwani watanzania wanajua sasa kuwa Chadema ndo inayoinyima CCM usingizi; hivi vyama vingine vinatumika tu; Chadema ndo chama kilichopata ridhaa ya wananchi wa Tanzania kama chama cha upinzani, wanaotaka kuungana na nyie watawafuata; Lakni cuf sisi wananchi tumeikataa! Waungana na CCM ni ruksa! NCCR, UDP, TLP tafuteni muafaka nao hao wanaweza wakafaa, lakini na wao wakijifanya wajuaji waacheni waangamie! maana anayeipinga chadema anapingana na umma na anapingana na Mungu.
  Quote

  +1 #28 YUDATADE MBOWE 2011-02-08 12:23 CHADEMA ndiyo chama kikuu cha upinzani kwahiyo wanatakiwa waongoze kambi ya upinzani bungeni kwani vyama vingine vya upinzani ni mamluki wa ccm, nayo chadema inatakiwa ijipange sawasawa kwa ajili ya kuchukua inchi 2015
  Quote

  -2 #27 mshipi 2011-02-08 12:20 KAMA KUKOSOA BILA KUTOA SULUHISHO NDIO UPINZANIA BASI CHADEMA NDIO CHAMA PEKEE CHA UPINZANI. WASIWASI WANGU NI KUWA ISIJE IKAWA CHUI KAVAA NGOZI YA KONDOO, KWANINI HAWATAKIKUUNGAN A NA WENGINE AU WANA WAALIMU WENGINE WASIOKUA WANASIASA??? "IN GOD WE TRUST"
  Quote

  0 #26 Nyaindi 2011-02-08 11:42 CCM na CUF wanashirikiana kuidhoofisha Chadema na harakati zote za kuibua maovu ya chama hiki kandamizi,watan zania tuwe macho nchi ni yetu sio ya vyama vya siasa,kama uko makini na una matazamo wa mambo yanayotokea lazima uyapime kuwa ni kwa maslahi ya nani?
  Quote

  0 #25 METHOD 2011-02-08 11:22 JAMANI TUACHE UTANI CCM BILA KUWA NA UMOJA NDNI YA UPINZANI CCM ITAENDELEA KUONGOZA MILELE...TUJARIBU ANGALI MIFANO HALISI PALE KENYA AMBAKO NDIO KUNA UKOMAVU WA KISIASA KULIKO SISI ILI KUIONDOA KANU ILI BIDI UFANYIKE MUUNGANO WA ODM NA VYAMA VINGINE NDIO KANU WAKANGOKA MADARAKANI...LEO CHADEMA KIMEIBUKA GAFLA KIMEISHA JIONA CHENYEWE KINA NGUVU YA KUIONDOA CCM MADARAKANI...TUSIJIDANGANYE UWEPO WA CCM MADARAKANI UTAENDELEA DAIMA KWA HALI HII YA KUTENGANA. KWA MAONI YANGU NAOMBA VYAMA VYOTE VYA SIASA VYENYE WABUNGE WAJIUNGE PAMOJA ILI KUIKABILI CCM VILIVYO 2015....WAKATI WA KUANZA KUFANYA MIKAKATI NDI HUU NA SIO KUFIKA 2015 NA KUANZA KUKURUPUKA...WA'TZ TUSIINGIZE SIASA YA ZANZIBAR NA BARA,NI SEHEMU MBILI TOFAUTI KISIASA.
  Quote

  +1 #24 Katiba TANGANYIKA 2011-02-08 11:22 Yaani serikali ya JK inataka kuhakikisha wanabana na kuua vyama pinzani kwa kutumia mianya ya katiba!

  Makinda ana jua kabisa utaratibu wa mabunge ya nchi za jumuia madola kunakuwa na Chama tawala , MAIN OPPOSITION PARTY, MINORITY PARTIES

  Iweje avuruge utaratibu huo? kwanini anawaridhisha CUF na sio CHADEMA? aelewe kwamba kufanya hivo kwanza ni kinyume cha taratibu, na pili CUF ipo kwenye calition hivo ni kuipendelea CCM.

  Madaraka hayo inabidi anyang'anywe sbb ni kutumia madaraka kwa faida binafsi za chama tawala, wkt spika atakiwi kuelemea upande wwt bungeni bali awe neutral na kuondoa mapungufu ya kisheria kunufaisha vyama vyote kwa faida ya wananchi.
  Quote

  +2 #23 margareth 2011-02-08 11:01 tupo nyuma yenu chadema na zaidi we prey for you ili muendelee kufichua maovu. hatukustaili kuwa kama tulivyo sasa tanzania.
  Quote

  +1 #22 LENGAI 2011-02-08 10:49 CHADEMA mkiungana na CUF Watanzania wote tunawahama. Tunataka mshike nchi 2015 hivyo msiungane na watu vigeugeu please nawaombeni sana. CUF ni tawi la CCM na tunataka kumtoa Rais wa CCM kabla ya 2015.
  Quote

  -4 #21 Kasuku 2011-02-08 10:26 Jamani eeh, mie nataka niulize swali, Mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni au ni kiongozi wa kambi ya CHADEMA bungeni?

  +2 #20 mdau halisi 2011-02-08 10:18 Quoting said yusufu:
  Ndugu watanzania CHADEMA wametaka wenyewe. Bila ya kuungana tusijidanganye hatuwezi kuitoa CCM. sasa wawe na akili CHADEMA wasiwe na chuki watajimaliza kwani CUF ni wajanja watatumia chuki ya chadema na Chama hicho kitakuwa ndo mwisho wake. wakae pamoja wapate suluhu wawe kitu kimoja kwa manufaa ya taifa.​
  CHADEMA iungane na nani? CUF? Mbona CUF wameshaungana na CCM? CHADEMA ilitaka sana umoja lakini ikagundua kwamba CUF wapenda madaraka na wasaliti wameshakuwa lao moja na CCM, kwa hiyo ni hatari sana kuwashirikisha kwenye vikao vya upinzani maana watakuwa mapashikuna wa CCM. CHADEMA kina nguvu sana, vyama vingine navyo kama vile TLP, NCCR mageuzi si muda mrefu watagundua kuwa sambamba na CUF ni kujiangamiza wenyewe, CUF ni kikulacho ki nguoni mwako. Wanauchu wa kushika madaraka hata ikiwa ni kuwasaliti wananchi. CHADEMA songeni mbele, Anna Makinda amepanga mabaya sana dhidi ya upinzani bungeni, siri hizo tunazijua lakini hatafika mbali, ajue atahatarisha maisha yake mwenyewe akicheza na maisha ya watanzania. Sasa hivi hatutaki kabisa fedheha tunataka bunge litupe majibu ya fadhaha za kimaisha tunazozipata.
  Quote

  +3 #19 CAROLINE 2011-02-08 09:50 CHADEMA ndio chama cha upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa hawajaungana na CCM. CUF ni tawi la CCM kwani wameungana ili mpenda madaraka Maalimu Seif Sharifu Hamadi awe makamu wa Rais. CHADEMA tuko nyuma yenu na lazima mchukue nchi 2015 kwani CCM na CUF w[NENO BAYA]. Tunasubiri watekeleze ahadi walizotoa kwa Watanzania. Reli ya Tanga kwenda Musoma na viwanja vya ndege.
  Quote

  +2 #18 Rutasingwa 2011-02-08 09:49 Ama Kweli kuna mijamaa haijaelimika..Napendekeza comment za ki[NENO BAYA] ziwe blocked..! Huwezi mtu mzima na akili yako ukawalaumu CHADEMA kwa kuwakataa CUF wakati unajua fika kwamba CUF sio chama cha upinzani.Hii ni mbinu ya CCM kuvunja Nguvu ya CHADEMA. CUF ni chama kinachokufa na Survival yake inategemea fadhila za CCM. Usitegemee CUF kuigeuka CCM hata kidogo...! So, Kwa watanzania wooote...Inajulikana wazi kuwa..Mbunge 1 wa CHADEMA ni sawa na wabunge 20 wa CCM na CUF...! They can do what they want to do, bu they cant take it away from us...! Pipooooooooooz.....! Pawaaaaaaaaa..! Pipoooooooooooo oooz......! Pawaaaaaaaaaaaa a.
  Quote

  +2 #17 ZULFAT 2011-02-08 09:46 Naona kama watz hawaijuiu siasa wala demokrasia, wanapenda kuchapia mambo tu. hawa utasikia chadema hivi, ccm, vile, cuf haya. Mnachochekelea watz bara ni kuona znz kila siku watu wanauwawa, hakwishi migogoro, mnafurahi na kujifanya wachambuzi na wajuvi wa mambo. Sa hizi kuona znz kumetulia kunawatia kinyongo kwa kweli hamuipendi kabisa hii hali. Sasa ninawambia hivi. hata museme sijui CUF si upinzani, ni mamaluki MTAJIJU!!! kazi kwenu sisi huku kwa raha zetu. Mutabakia nyinyi huko kila siku kupigana na polisi sijui chadema chawavu, chajarife, WANAFIKI WAKUBWA NYIE!!!
  Quote

  -8 #16 batarokota 2011-02-08 09:44 chadema tumienibusara unganeni na wapizani wenzenu nccr,cuf,udp n.k kwa masilai ya nchi sio ya chama
  Quote

  +5 #15 mpenda haki 2011-02-08 09:35 makinda hongera kwa kufuata maamuzi ya hamadi rashidi na Cuf,kwani nani asiyejua kwamba cuf na ccm ni kitu kimoja?? ningeshangaa sana kama usingefuata ya cuf kwani wewe mwenyewe uliingia uspika kwa kura zao si unalipa fadhila?? si uliona hata arusha tlp walipokubaliana na ccm hata diwani wao mmoja tu walimchagua kuwa naibu meya?? Nguvu ya Watu iko nyuma ya Chadema,kwani sauti ya watu ni sauti ya Mungu.Tusubiri tuone ya Tunisia na Misiri.Hakika.
  Quote

  +7 #14 Mtanzania 2011-02-08 09:22 NAENDELEA KUSISITIZA, CHADEMA SI CHMA CHA MSIMU, HATA WAKIWEKA MAPINGAMIZI YA AINA GANI, NGUVU YA UMMA ITAJIBU. BADO TUNAIKUBALI CHADEMA. NAWATAKIA WABUNGE KIKAO CHEMA, ILA ANNE MAKINDA JIANDAE, BUNGE LITAKUSHINDA.
  Quote

  +6 #13 maharagejuma 2011-02-08 09:09 TANZANIA HAKUNA DEMOKRASIA NA NDIO MANA TUNATAKA KATIBA MPYA. UNAPOPEWA CHEO USITEGEMEE KUMPINGA ALIEKUWEKA HAYA NDIO MATOKEO YA KUPEWA CHEO. ANNA MAKINDA KAWEKWA PALE KWA MASLAHI YA CCM. NA CCM NI CUF NDIO MANA WANABADILISHA KILA KITU KUIDHOOFISHA CHADEMA. LAKINI NARUDIA TENA KUSEMA YANA MWISHO NA HAWA VIONGOZI WABABAISHAJI IPO SIKU TUTAWAFUNGA TU. WAO WANAMSIKILIZA HAMAD KWA VILE YUKO CUF MBONA HUKO NYUMA NI YEYE HAMAD NDIO ALISEMA SHERIA IBADILISHWE LEO TENA ANASEMA SHEIA IBADILISHWE MAKINDA ANABADILISHA. TUJIULIZE HIVI CUF NDIO WANGEKUWA NA WABUNGE WENGI SHERIA INGEBADILISHWA? CHADEMA ANDAENI MAANDAMANO NCHI NZIMA KUPINGA YOTE HAYA YA MAKINDA NA CCM YAKE. HAPO NDIO WATAKAPOONA YA MISRI NA TUNISIA TUKO TAYARI KUBADILISHA NCHI TUMECHOKA NA VIONGOZI WABABAISHAJI. ANDAENI MAANDAMANO TUKO TAYARI KUFA ILA TUTAJIANDAA VILEVILE. POLISI WAKI[NENO BAYA]ZA SAFARI HII NI MABOMU YA PETROLI ACHA TULETE TANGANYIKA YETU. CCM WAMEJISAHAU WANAONA KAMA WAO NDIO MIUNGU WATU.
  Quote

  -9 #12 said yusufu 2011-02-08 09:03 Ndugu watanzania CHADEMA wametaka wenyewe. Bila ya kuungana tusijidanganye hatuwezi kuitoa CCM. sasa wawe na akili CHADEMA wasiwe na chuki watajimaliza kwani CUF ni wajanja watatumia chuki ya chadema na Chama hicho kitakuwa ndo mwisho wake. wakae pamoja wapate suluhu wawe kitu kimoja kwa manufaa ya taifa.
  Quote

  -10 #11 smartboy 2011-02-08 08:51 Kwani serikali ndo imebadilisha kanuni? Sasa nani muhuni kati ya Anna na Slaa? Hehehe! mtakufa na uchu wenu wa mali? wasmoke bwan!
  Quote
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  +7 #10 bdo 2011-02-08 08:46 nia yetu ni kuwa na upinzani wa kweli na sio unajisi..Anna Makinda kaisha najisi bunge na kanuni kwa maslahi ya Wifi zake - CUF, TLP, NCCR, UDP, hapa hakuna kambi ya upinzani tena - ni rangi mbili, nashauri CHADEMA kama hiyo kanuni itarekebishwa basi jitoeni katika kambi ya upinzani na muwe wabunge huru ili mjiondoe na unajisi wa CCM na CUF, nguvu ya umma itawalida "peoples' power"
  Quote

  -1 #9 ikingili ntuware 2011-02-08 08:18 serikali ya Tanzania ni ya kihuni, kwanza makinda ni muhuni kwanini msiache wawakilishi wetu wafanye kazi yao kama tulivyowatuma kama hii serikali haiongozwi kihuni?acheni uhuniiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiii mambwa nyie.
  Quote

  +5 #8 Bams 2011-02-08 08:12 Kama kambi ya upinzani itajumuisha na CUF, basi ni aheri kutokuwa na kambi ya upinzani. Ni dhahiri kuwa CUF wakati wote itakuwa kwenye kambi ya upinzani ikifanya kazi kwa manufaa ya CCM na kudhoofisha upinzani. Aheri ukawa na jeshi la askari 100 wenye dhamira moja kuliko kuwa na jeshi la askari 1000 lakini ndani yake wakiwemo askari 100 wa adui yako. CUF kwa sasa ni mwiba mbaya kwa upinzani kuliko hata CCM.
  Quote

  +6 #7 mhogo mchungu 2011-02-08 08:09 Zote hizi ni mbinu za CCM kuthoofisha nguvu ya upinzani bungeni kwani CUF si chama cha upinzani tena bali kitakua mamluki.Ila CHADEMA msife moyo.Kazeni buti.Mwisho wa siku wananchi wataelewa nia yenu.
  Quote

  +7 #6 avemaria 2011-02-08 08:09 Tumezowea uhuni huu, na sasa kitakachofuata ni nguvu ya umma tuu hapa tanzania. The popular democracy ... no bullet can resist the peoples' power!!! Ona Tunisia, Ona Misri!!
  -15 #5 poa 2011-02-08 08:06 Chadema huo ubinafsi wenu utakuponzeni tulidhani chadema muko makini kwa maslahi ya wananchi kumbe sio hivyo ni kwa maslahi ya mbowe tu. acheni siasa za kikabila.
  Quote

  +6 #4 MTAMBUZI 2011-02-08 07:54 SASA HIVI NCHI INAENDESHWA KIHUNI KWA HILO LA MABADILIKO YA KANUNI KWA SABABU YA CHADEMA NI JAMBO LA KIHUNI. KATIKA MIHIMILI MIKUU YA SERIKALI NI MAHAKAMA TU WALAU INAPUMUA
  Quote

  +9 #3 flika 2011-02-08 07:32 Kwa kuwa CUF ni chama tawala Z'bar, wanataka kuua upinzania bara. Hivi hawa wanaoongozwa na makamu wa Rais wataikosoa nini Serikali? Kwa mbinu hii ya ccm, nina shaka ya mustakabali wa upinzani Tanzania. Ni hatari kutunga sheria kwa ajili ya mtu.
  Quote

  -12 #2 smartboy 2011-02-08 06:47 Ubinafsi na ufisadi haupo kwa serikali tu pekee yake, hata kwa wapinzani pia upo. Kung'ang'ania madaraka yote ya kambi ya upinzani bungeni eti kwa kisingizio cha uwingi wa wabunge ni ufisadi wa madaraka. Wbunge wote wanapaswa kutambua kuwa wapo kuwakilisha wananchi na ni jukumu lao kuangalia maslahi ya Taifa zaidi kuliko vyama vyao. Chadema wanatakiwa watambue hilo. sidhani kama kuna maslahi ya kitaifa kwa wao kujitenga na wapinzani wenzao kwa kuunda kambi yao pekee yao. naamini kushirikisha vyama vyote vya upinzani kwenye kambi mmoja kunatakuwa na upinzani wenye nguvu zaidi. ikiwa ktk bunge la sasa chadema, cuf, nccr, na udp wakiunganisaha nguvu pamoja watakuwa na nguvu kubwa ya hoja na maamuzi kuliko wakiwa kivyao.
  Big up spika kubadilisha kanuni hizo.
  Quote

  +7 #1 elibariki yerald 2011-02-08 06:28 huu nu uhuni wa kulazimisha ndoa isiyo na tija bali ni kuleta malumbano na kuua upinzani lakini hii ni CUF kuonea donge CHADEMA kuwashinda kwenye uchaguzi Lakini haina noma vijana fanyeni kazi watanzania watawatambua acheni hao mamluki waendelee kuwepo , kwasababu sike zota CCM ni wazee wa kuvunja sheria na kanuni kwanini wanaenda kinyume na sheria ya mabunge ya jumuiya ya madola ambayo waliridhia? huuu ni unafiki mkawashitaki huku .....nyamabafu
  Quote
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

  [​IMG]


  22.JPG

  525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

  Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

  Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

  Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

  Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

  Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

  Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

  Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

  Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

  Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

  (1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

  (2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

  (3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

  Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  NGUVU YA UMMA TUNAKUJA KUWATOLEENI MAAMUZI MAZURI ZAIDI KWENYE KILA SWALA LA GHILIBA FITINA NA USALITI WOWOTE UTAKAOTOKEA HAPO BUNGENI WALA MSIWE NA WASIWASI; MACHO YOTE KWENU

  [​IMG]
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  CHADEMA watikisa Bunge

  • Wabunge CUF, NCCR, wapigiwa chapuo na CCM

  na Irene Mark, Dodoma

  KIKAO cha Bunge jana kiligeuka ukumbi wa mapambano na mabishano makali ya hoja baada ya Spika wa Bunge kuruhusu mjadala kuhusu tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

  Hatua hiyo ya spika kuruhusu mjadala huo iliyotokana na ombi la wabunge wawili, Hamad Rashid Mohamed (CUF) na David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ilipokelewa kwa malalamiko makubwa na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Mjadala kuhusu suala hilo ulioanza asubuhi kwa wabunge kupigana vijembe, kuzomeana, kukejeliana na wakati mwingine kulazimishwa kufuta kauli zao ulihitimishwa na hatua ya wabunge wa CHADEMA kulazimika kutoka nje ya Bunge ili kupinga kushiriki katika mabadiliko hayo ya tafsiri.

  Wabunge hao wa CHADEMA wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, walitoka nje ya ukumbi muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha jioni.

  Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kufanya hivyo Novemba mwaka jana wakati walipoisusa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete.

  Kabla ya kutoka nje, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alilazimika kubadili uamuzi wake wa kutaka kumfanya Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah kuwa ndiye mchangiaji wa mwisho wa hoja hiyo kutokana na ombi la muongozo wa spika lililotolewa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).

  Akiomba mwongozo wa spika kwa mujibu wa kanuni ya 68 ya Bunge, Mnyika alimtaka Spika huyo kutoifunga hoja hiyo hadi hapo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, atakapopewa nafasi ya kuchangia hoja hiyo.

  "Mwongozo wa Spika… kuna taarifa za uhakika nimepata kwamba miongoni mwa wachangiaji wa hoja hii walioomba kuchangia lakini majina yao yamekatwa ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Sasa kwa mujibu wa Kanuni ya 68, hoja hii isifungwe hadi hapo kiongozi wa upinzani atakapopata nafasi ya kuchangia," alisema Mnyika.

  Spika aliridhia hoja ya Mnyika na Mbowe akasimama kuchangia mjadala akianza kueleza masikitiko yake na ya chama chake kutokana na hatua ya wabunge kuwalazimisha kuingia kwa nguvu katika ndoa wasiyoitaka.

  Mbowe alisema CHADEMA haiwezi kuingizwa kwenye ndoa wasiyoiridhia huku akifafanua kwamba maridhiano hayawezi kuchukua wiki moja au mbili na akawaonya wabunge wa CCM kutotumia wingi wao kupitisha kile alichokiita maovu.

  "Hatuwezi kuingizwa kwenye ndoa ambayo hatujaridhia. Napata hofu ya umoja wenu leo. Naamini kwamba maridhiano hayachukui wiki moja au mbili… leo mkitumia wingi wenu kufanya maamuzi mnafikiri mnajenga kumbe mnabomoa.

  "Tuache unafiki na kudanganyana, tatizo letu sio tafsiri kama mnavyotaka kuiaminisha dunia. Tatizo hapa ni dhana ya ushirika tunaoutaka… kuna mambo ya msingi ambayo tunayapigania na tutafanya hivyo ndani na nje ya Bunge.

  "Hatuna ugomvi na muafaka wa Zanzibar. Hatuna ugomvi na CUF, lakini tunatofautiana kimsimamo… Tunaamini kwamba siyo vizuri kubishana na kanuni, tunatakiwa kuziheshimu.

  "…Sitokubali kuongoza kambi ya upinzani kwa kulazimishwa. Huo ndiyo msimamo wa chama chetu," alisisitiza Mbowe kisha akasimama na kuwaongoza wabunge wote wa chama hicho kutoka nje kuwapisha wabunge wa vyama vingine kupitisha kanuni hiyo.

  Hata hivyo, wakati wabunge wa CHADEMA wakitoka nje wabunge waliobaki walisikika wakitoa maneno ya kejeli dhidi yao kama vile 'tumewazoea', 'weak politicians', 'waroho na wachoyo wa madaraka', 'wasichukue posho', 'wababaishaji', 'tulijua hilo', 'hawana pa kwenda' na maneno mengine.

  Akiwa nje ya ukumbi wa Bunge, Mbowe alisema kila wanapofanya maamuzi wanakuwa na taarifa za kuaminika hivyo hata uwepo wao ndani ya Bunge si bahati mbaya bali ni kuwakilisha wananchi.

  "Tunaliheshimu Bunge, tunawaheshimu wabunge, kanuni na watendaji wote wa Bunge lakini kamwe hatutowaheshimu kwa kuweka rehani haki zetu… tutalipigania hili ndani na nje ya Bunge," alisisitiza Mbowe.

  Hata baada ya kutoka nje ya Bunge, Naibu Spika Job Ndugai, aliwaongoza wabunge waliobaki kupitisha tafsiri ya kanuni husika huku akisema kwa CHADEMA kutoka nje si jambo la ajabu na wala mbingu haziwezi kushuka kwa ajili hiyo ambapo wabunge wa vyama vingine walikuwepo.

  Kwa mujibu wa Ndugai, hoja hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika na David Kafulila na Hamad Rashid wakitaka kuingizwa ndani ya kambi ya upinzani na kupinga kambi hiyo kuundwa na CHADEMA.

  Mchangiaji wa kwanza wa hoja hiyo kwa asubuhi ya jana alikuwa Kafulila ambaye alieleza kuwashangaa wabunge wenzake wa CHADEMA kwa uchoyo wa madaraka huku akisema hataaminika tena katika jamii.

  "Hivi ninyi mmeshinda kwa asilimia 20 mnakataa kushirikiana. Mngeshinda kwa asilimia 60 sijui ingekuaje! Mimi nadhani umoja wa kambi ya upinzani ni jambo muhimu. Tuache ubinafsi," alisema Kafulila aliyekuwa akishangiliwa na wabunge wa CCM, CUF na wa NCCR.

  Mchangia aliyefuata alikuwa ni Hamad Rashid (CUF), aliyesema suala la umoja wa kambi ya upinzani kushirikisha vyama vyote ni jambo jema, hivyo hakuna sababu ya wajumbe kukataa kupitisha ufafanuzi huo wa kanuni.

  Hata hivyo, mchangia huyu alilazimika kufuta kauli yake ya kuwataka wabunge waache kile alichokieleza kuwa ni mambo ya kitoto ya kuwanyoshea vidole wabunge wa Zanzibar kuwa wanaingia bungeni kwa kuchaguliwa kwa idadi ndogo ya kura.

  Alipotakiwa na kufuta kauli hiyo, Hamad alisema, "Mheshimiwa spika nafuta kauli hiyo, haya basi na tuache mambo ya kikubwa… hili la kusema mbunge kachaguliwa kwa idadi ndogo ya kura ni matusi.

  Zanzibar ni nchi kamili tuache dharau," alisisitiza Rashid ambaye katika Bunge lililopita alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), alikua miongoni mwa wabunge waliolazimika kukatisha mazungumzo yake kila mara kutokana na taarifa na miongozo ya Spika ambapo alilazimika naye kufuta kauli yake pale aliposema wabunge wa vyama vingine ni wanafiki.

  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), alijikuta katika wakati mgumu pale alipokuwa akichangia baada ya wabunge wenzake (sio CHADEMA) kuomba muongozo wa spika kila wakati.

  "…Hao walioleta hoja waliandika barua wakiomba kugombea nafasi za uenyekiti wa kamati zile muhimu ndiyo maana leo tuko hapa, waseme ukweli.

  "Hapa hoja iliyopo ni uenyeviti wa kamati za kudumu hasa zile kamati zinazoongozwa na kambi ya upinzani… hatuwezi kukubali chama chenye mbunge mmoja kuwa mwenyekiti wa kamati kama PAC mathalani," alisema Tundu.

  Hatua hiyo ya Lissu ilisababisha Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP) kuingilia kati na kutoa maneno makali huku wabunge wengine wakisikika wakitoa kauli za miguno.

  "Nimeiongoza hiyo kamati kwa miaka mitano bila ya matatizo… shut up your mouth," alisikika Cheyo akimwambia Lissu.

  Alipopata muda wa kuchangia, Cheyo aliwataka wabunge wa CHADEMA kuwa wavumilivu na akawaasa kupunguza jazba kwa kuwa siasa si chuki bali ni ushindani wa hoja.

  "CHADEMA kuna watu wazuri sana lakini mkumbuke kuwa siasa siyo chuki hata kidogo… nawaombeni sana muwe wavumilivu. Hivi nani kasema mtu akitoka CCM akaenda CHADEMA ndo anakua mzuri?" alihoji Cheyo

  HOJA YANGU:

  Swali letu hapo bado ni kwamba kwa mtaji wa CCM sasa kuanza kuvuruga HATA KANUNI ZA BUNGE, jambo ambalo lina nafasi ya kuzua dhoruba nzito nzito kisheria kwa kipindi kirefu sana nchini, wananchi tunailiza Bunge hili kweli litazaa KATIBA MPYA au Tahrir Square kwa taifa letu???????
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mchakato katiba mpya waanza Tuesday, 08 February 2011 20:54

  Exuper Kachenje na Habel Chidawali, Dodoma

  MUSWADA wa Sheria ya Kuunda Tume itakayoratibu mabadiliko ya Katiba utawasilishwa katika Kikao cha Tatu cha Bunge la Kumi, kitakachofanyika Aprili mwaka huu, Bunge limeelezwa.

  Hayo yalisemwa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akitoa tamko rasmi la Serikali kuhusu uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi.

  Pinda ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali bungeni, alisema hatua hiyo ina nia ya kuwa na katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa ya hali ya sasa.

  Akitoa salamu za mwaka mpya, Desemba 31, mwaka jana, Rais Kikwete alisema Serikali yake imedhamiria kuanzisha mchakato wa kuitazama upya katiba ya nchi ili kuwa na katiba inayoendana na taifa lenye umri wa Nusu Karne kwa kuunda tume maalum ya katiba itakayokuwa na wajumbe wa pande zote.

  "Serikali inatarajia kuleta katika Bunge lako la Tatu la Aprili Muswada wa Sheria itakayoratibu maoni ya wananchi na kutoa elimu kwa wananchi ili kufanikisha lengo letu la kuwa na katiba itakayotutoa katika miaka 50 ya uhuru hadi kufika umri wa karne," alisema Pinda.

  Likiwa katika ratiba ya shughuli za jana za Bunge kama Kauli za Mawaziri (Waziri Mkuu), tamko hilo la Serikali lilieleza pia kwamba Rais Kikwete alieleza pia nia yake hiyo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 34 ya CCM mjini Dodoma, Februari 5 mwaka huu.

  Pinda alisema kuwa Bunge la Kumi litapata nafasi ya kutaja majukumu ya tume katika sheria inayotegemewa kutungwa, utaratibu au namna tume hiyo itakavyofanya kazi.

  "..Bunge hili litapata nafasi ya kutaja majukumu ya Tume katika sheria inayotegemea kutungwa, utaratibu au namna Tume itakavyofanya kazi; namna ya kuwapata wajumbe wa tume hiyo, sifa za wajumbe hao na mambo mengine ambayo Bunge hili litaona yanastahili kuwekwa kwenye sheria hiyo," alisema Pinda.

  Alisema Serikali imetafakari namna nzuri ya kuendesha mchakato huo. Alisema katika kuandika Katiba ya sasa, Hati ya Muungano (Articles of Union) rais alipewa mamlaka ya kikatiba ya kuwateua wajumbe wa Tume ya Katiba kwa ajili ya kuandaa mapendekezo ya katiba ya Kudumu mwaka 1977, ambapo pia aliwateua wajumbe wa Baraza la Kutunga sheria kutoka pande zote za Muungano.

  Pinda alieleza kuwa utaratibu huo na ule uliofanyika mwaka 1983/84 na ule wa mwaka 1998 wa kuunda tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba na kuyawasilisha serikalini ni tofauti na utaratibu utakaotumika sasa kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.

  Kwa mujibu wa Pinda, katika utaratibu wa sasa Serikali ina lengo la kuwashirikisha wananchi wote katika mchakato huo wa kupata katiba mpya ili kuondoa malalamiko.

  "Serikali imedhamiria kuanzisha mchakato wa kuitazama katiba yetu upya, tuwe na katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoendana na mabadiliko na matarajio ya nchi yetu: ...Nia yetu ni kuwashirikisha wananchi na kuhakikisha kwamba wanashiriki kikamilifu," alisema Pinda na kuongeza:

  "Jambo hilo ni la kupanua demokrasia na kuhakikisha kunakuwa na katiba ya nchi inayoonyesha utashi wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano."

  Pinda alisema ni matumaini yake na serikali kuwa wananchi watatoa maoni yao kwa uhuru, uwazi na bila woga wakizingatia umoja wa kitaifa, amani na mshikamano ambavyo ni tunu za taifa la tanzania zinazopaswa kulindwa na kutunzwa kwa gharama yoyote.

  SOURCE: Mchakato katiba mpya waanza

  MAONI YANGU:

  Pamoja na serikali kuonekana kuelekea kukubaliana na umma wa Tanzania kwamba mchakato wa KATIBA MPYA uanzie Bungeni Dodoma, vile vile pamoja na umakini wa 'Mtoto wa Mkulima' katika maswala yenye maslahi ya taifa, CHADEMA hawana budi kuwashilisha haraka iwezekanavyo mswada huu katika bunge la hivi sasa ili huko mbeleni kusije kukatokea masuala ya kupiga danadana ki-muda mpaka tukaingia uchaguzi mkuu ujao bila katiba mpya.

  Endapo kutatokea uzembe katika hili basi uchaguzi mkuu ujao bila katiba mpya, na bila tume huru ya uchaguzi, moja kwa moja itakua ni sawa na watu kutafutana shari bure hapa. Kazi hizi za msingi zianze mara moja na sasa hivi.
   
Loading...