Bunge: Leseni mpya utafiti wa gesi zisitishwe

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2]
gas+TZ.jpg
[/h]


Na Sharon Sauwa



16th July 2012








Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imeiagiza serikali kusitisha utoaji wa leseni mpya za utafiti wa gesi hadi hapo maandalizi ya sera ya gesi itakapokamilika ili pamoja na mambo mengine, itoe mwongozo wa uendeshaji wa sekta hiyo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Suleiman Zedi, alipokuwa akizungumza katika semina iliyoandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha cha Utafiti wa Misitu (Cifor) kwa lengo la kuelezea Maendeleo ya Biofuel, haki ya raslimali za nchini na serikali.
Zedi alisema nia ya kuiagiza serikali kusitisha utoaji wa leseni hiyo ni kuweza kuwa na miongozo katika sekta hiyo inayokuwa kwa kasi nchini.
“Sasa hivi kila kampuni inaingia mkataba wake na serikali, tunataka kuwa na mwongozo ambao utasimamia sekta hii,” alisema.
Alisema ugunduzi wa gesi unaonekana mwaka huu umetokana na leseni za utafutaji zilizotolewa chini ya mwaka 2003.
Alisema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lilikuwa limeshaanza utaratibu wa kutoa leseni mpya za utafutaji wa gesi.
Hoja hiyo iliibuka baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lambeli, kutilia shaka mikataba ya gesi iliyopo nchini haitalisaidia taifa kwa kuwa asilimia 90 itakayozalishwa itasafirishwa kwenda kuuza nje.
Alisema jambo hilo lilimsononesha na kutamani kujificha chini ya uvungu wa kitanda.
Akijibu hoja hiyo, Zedi aliwatoa wasiwasi wabunge kwa sababu kiasi cha gesi kitakachozalishwa nchini hakitaweza kutumika chote nchini kwa kuwa ni kingi mno.
“Tatizo sisi kama nchi yetu itanufaika na nini? Tatizo si kuuza nje ya nchi kwa kuwa kiasi kitakachozalishwa kitabaki kingi hatutaweza kukitumia chote kuzalisha umeme na matumizi ya nyumbani,”alisema .
Kwa upande wake, Lembeli alisema Watanzania wameshuhudia katika madini, wawekezaji wakichimba na kuondoka huku wakiwa hwajunufaika vya kutosha na raslimali hiyo.
Alitaka mikataba hiyo kupelekwa bungeni ili wabunge waichambue na kufahamu Watanzania watanufaika na nini.
Kwa upande wa Biofuel, wabunge hao walitaka uandaaji wa sera hiyo kusitishwa hadi pale kutakapofanyika utafiti wa kina kuhusiana na nishati hiyo na faida zake kwa wananchi.
Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama (CCM), alitaka hata idara inayoshughulika na nishati hiyo katika Wizara ya Madini na Nishati kufutwa.
Pia alitaka mashamba yaliyochukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Kisarawe na Kilwa, kurejeshwa kwa wananchi kwa kuwa sasa hayafanyi kazi baada ya wawekezaji hao kuyatelekeza.
Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwaijage, alisema haoni haja ya kuzalisha Biofuel kwa sasa kwa kuwa kipaumbele cha taifa ni kuzalisha chakula kwa wingi.
Pia alishauri miradi ya Biofuel isimamishwe hadi pale kutakapofanyika utafiti wa kina na sera kupelekwa bungeni, kujadiliwa na kupitishwa.
Akijibu hoja hizo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Profesa Emmanuel Luoga, alisema suala la kusimamisha uzalishaji kwa makampuni yaliyowekeza katika miradi hiyo ni gumu kwa kuwa wanavyo vibali vilivyolewa na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC).
“Masharti huwa mwekezaji anapaswa kwenda TIC na kuomba ardhi lakini wengine wanapita na kufanya ushawishi mlango wa nyuma ambapo wanakwenda wenyewe kutafuta ardhi na kuomba vibali serikalini,” alisema.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom