Bunge Leo laahirishwa Sababu wabunge wa CCM wanaenda kufanya kazi za chama na posho wamechukua

bunge limeahirishwa saa 4.45 kisa wabunge wa CCM wanakwenda kukutana na Mkt wa chama Dk Magufuli kumbuka kuwa wabunge Leo watajilipa posho zaidi ya mil 90 pesa za walipa kodi watanzania ili hali wanafanya kazi za chama. Haya ni matumizi mabovu ya Pesa zetu.

Haiwezekani wabunge Leo waone vikao vya maslahi ya taifa tena kikao cha Bajeti cha taifa hakina maana yoyote ila kikao cha chama ndio kina maana sana, Leo wabunge wao watajilipa posho bila kuifanyia kazi yoyote,



Sent using Jamii Forums mobile app
CAG ameshaliona hilo

In God we trust
 
Si utakuwa kupongeza na leo waruhusiwe woote wapongeze mpaka wakufuru kama Mwanri ili wakirudi Bungeni wawe na akili ya kutumia muda vizuri.

Manake hata wao hawako pamoja miongoni mwao kuna elites ambao wako karibu na Mwenye band na kuna wengine wenzangua na mie kama watoto wa kambo.

Mtegemee nishani zingine kwa kina kinakibajaj, Musukuma na mlingwa kwa utumishi uliotukuka. Pongezi zaidi kwa kumtoa katika reli Prof. Assad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM hawezi kukubali aibu za ndugai Kwa sababu:
1: Ndugai anaonesha dhahiri chuki binafsi dhidi ya CAG kwakumtaka ajihudhuru
2:Rais hawezi kukubali bali shinikizo kisa tu CAG kakosoa mfumo
3:Siyo kila jambo nila mtu kujihudhuru kisa tu labda mtu kapotoka maramoja
4:Ndugai Kwa kitendo cha kutoa shinikizo CAG ajihudhuru anataka kuuaminisha umma kama yeye hajawahi ikosea mihimili mwingine.
5:Kitendo cha kukingia kifua if idadi Kwa mgongo wa bunge Ni ulikuwaje wa katiba
 
JPM hawezi kukubali aibu za ndugai Kwa sababu:
1: Ndugai anaonesha dhahiri chuki binafsi dhidi ya CAG kwakumtaka ajihudhuru
2:Rais hawezi kukubali bali shinikizo kisa tu CAG kakosoa mfumo
3:Siyo kila jambo nila mtu kujihudhuru kisa tu labda mtu kapotoka maramoja
4:Ndugai Kwa kitendo cha kutoa shinikizo CAG ajihudhuru anataka kuuaminisha umma kama yeye hajawahi ikosea mihimili mwingine.
5:Kitendo cha kukingia kifua if idadi Kwa mgongo wa bunge Ni ulikuwaje wa katiba
Andika vizuri mkuu sio kujihudhuru ni kujiuzulu
 
Spika amekurupuka sana suala la CAG.
Lisipochukuliwa kwa umakini litaipotezea CCM na serikali yake heshima ,huku wabunge wa CCM na madiwani wao wakitegemea Mbeleko za kura za bunduki , risasi na mabomu badala ya Karatasi na kalamu.

Kiburi chote cha Ndugai na Wabunge wa CCM ni kutegemea kura za bunduki,risasi ,mabomu na virungu lakini wananchi wanachukizwa sana na tabia yao ya kupuuza maoni ya wananchi huku akiweka mbele maslahi yao.

Kuna tofauti gani na wapinzani waliokataa kufanya kazi na Mh. Rais na kutoka nje wakati wa kulifungua bunge?
Wabunge wa CCM nao wameanza kususia wateule wa Rais ? Huku ni kumhujumu Rais waziwazi.


Sent using Jamii Forums mobile app

Hongera kwa kusema ukweli, nusu ya wabunge wa ccm wameingia kwa kutumia nguvu ya dola na mbeleko ya tume ya uchaguzi, na sasa ndio wanajitangaza kwa lazima, hiyo ndio inayowapa jeuri kufanya watakalo.
 
Namhurumia sana Prof. Assad. Najihurumia mwenyewe kuwa mtanzania, nawahurumia watanzania tuakavyoteseka chini ya majinamizi ya CCM, Naumia jinsi watanzania tunavyonyanyasika na kodi zetu kuchezewa kijinga hivi.
Nasikitika sana kuzaliwa kwenye nchi la hovyo kama hili.
 
Hacheni kulalamika. Upinzani ungekuwa na significant number of parliamentarians at least to qualify a quorum, Bunge lisingeahirishwa [technically]. Kinachoitwa kuahirishwa kwa kikaocha Bunge ni technical kwa sababu ukiondoa wabunge wa CCM, wabunge wa upinzani hawafikii ikidi ya kuendesha kikao cha Bunge!

Akina Mbowe waliamua kuhujmu UKAWA ili wapate pesa kisha upinzania ukashindwa vibaya. Laana ya kushindwa huendelea hadi uchaguzi unaofuata. Anayekubali kuendelea kuongozwa na akina Mbowe anatafuta kuendelea kulalamikia washindi wa CCM bila kuwa na jitihada zozote za kujinasua. Wanachopata wabunge wa CCM ni motisha unayotokana na chama chao kushinda uchaguzi Mkuu, 2015. Viongozi wenu wakiendekeza tena malengo [yaliyojificha] ya kuvuna pesa badala ya kutafuta, kusimamia na kuvuna kura, wanachama/wafuasi wao hamtakuja kuacha kulalamika daima.
Kwa hiyo wewe pia ni dhaifu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la Mkulu ni kuwa inaekekea hajui maana halisi ya Ufisadi.... Inaekekea hajui kuwa Matumizi mabaya ya pesa au mali ya umma ni Ufisadi pia...!!
 
wacha wivu wa kike je na wale wanaotoka toka nje wakati wamechukua pesa za walipa kodi watanzania yanakuwa ni matumizi mazuri ya pesa zetu au. Umeonyesha dhahiri kuwa wewe una udhaifu zaidi
Lakini Bunge linaendelea hata wakitoka.

Pia msuguano unakia ni wa mjadala uliopo Mezani .
Sasa hili la Prof .Assad linakuaje ishu kubwa ya kuwafanya wabunge wa CCM wasusie kikao na spika wao?

Watanzania tuamke tuchague wabunge na madiwani wengi wa Vyama vya upinzani ili bunge lionyeshe ukomavu wa kidemokrasia.

Leo hii naibu angekua Wa Chama kingine basi wasingeahirisha Bunge.
Bunge lingeendelea na mjadala wasubiri akidi ya kupiga kura tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu Bunge limehairishwa muda Huu. Kuna Kikao cha Dharura cha Wabunge wa CCM na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli. Stay Tuned
Mkuu Tumbo Tumbo sijui Kwanini comments zako huwa nazikubali sana sana Mkuu...huwa nikiingia JF lazima niangalie Tumbo tumbo amesema nini Leo,Huwa nakufananisha na jingalao
Unajua unakubalika sana sana hapa JF Mkuu kwa Comments zenu!
Ni hayo Mkuu!
Najua majukumu yako ni Mengi ya chama na kule kwingine....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kama busara itatumika, Mheshimiwa Raisi atasuluhisha mambo kati ya Spika na CAG, kufanya hivyo atakisaidia chama chetu cha CCM kujitoa kwenye hivi viji scandals za kijinga zinatengenezwa na watu wasiokuwa na nia nzuri, utadhani wamelipwa na upinzani ama mabeberu na mashirika kuihujumu serekali na nchi yetu.

Lakini Raisi akija na muelekeo wa kumkomoa CAG, basi atakuwa amejenga ufa mkubwa kwenye CCM, na ni fursa kubwa kwa upinzani na mahasimu wake.

Tungoje na tuombe busara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom