Bunge lawaka moto: Lissu, Msigwa na Lema watolewa nje!

Sehemu ya hotuba ya Lema, leo bungeni. Kuna paragraph moja (nitaiweka baadae katika mjadala huu) Naibu Spika alimzuia kuisoma kabisa. Hivi lini Magamba hawa watakubali kukosolewa na kujibu hoja za wapinzani wao kwa hoja zenye mantiki. Serikali ya CCM wajenge hoja wasipayuke (Argue! Don't shout, Prof. Shivji in Intellectuals at The Hill).

"Mheshimiwa Spika,Mpigania haki za watu weusi wa nchini Marekani, Hayati Dr. Martin Luther King, Jr. aliwahi kusema kwamba "peace is not the absence of war but merely the presence of Justice", yaani "amani si hali ya kutokuwepo vita, bali ni uwepo wa haki". Kwa kipimo hiki cha amani, nchi yetu haina amani kama viongozi wa serikali na wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanavyodai kila mara. Hii ni kwa sababu, licha ya ukweli kwamba Tanzania hakuna vita, pia ni dhahiri Tanzania sio nchi ya haki. Nathibitisha;"

wajukuu zangu hali zenu,

kwanza niwakumbushe kitu kimoja, .....HAKI BILA YA WAJIBU, FUJO.....................

TAFAKARI...........................................HAKI,ELIMU, .............................................WAJIBU.

mkuu ume join 2006 na hii ni post yako ya kwanza. pole kwa hilo, ila mbona sijakuelewa unamaanisha nini? naona km umekopa misemo ya shibuda vile.

ndugu mrekebisharika,umesema vema lakini unazungumzia matokeo bila kiini! Ni sawa na kulaani kwanza vurugu bila kwanza kulaani wasiotenda haki!

Inakuaje m'bunge atolewe njee ya ukumbi wa bunge pale anapotetea maslahi ya taifa,? Kweli ina maana gani ya kuwepo wabunge wa upinzani bungeni? Ni aibu tupu.

Mh. Lema, lisu na mchungaji wametolewa njee ya bunge kwa kusema tanzania haina amani bali ni nidhamu ya uoga? Nini kazi ya wabunge wa upinzani bungeni kama sio kuikosoa serekali..? Kwa stahili hii ni bora au nashauri wabunge wote wa upinzani waligomee bunge tuu kuliko kudhalilishwa hivi kwa mnaofuatlia bunge nadhani mmenielewa naomba kuwakilisha

mungu ibariki tanzania

Hapo kwenye red hapajakaa sawa! Kwa hiyo sisi wapiga kura ndio tuna nidhamu ya uoga au wanamaanisha nini hao wabunge?

Tatizo ninaloliona ni kwamba kunakuwepo na double standards, kama mbunge wa upinzani akikosea hatu zinakuwa a bit tight kulinganisha na hatua zinazochukuliwa iwapo mbunge wa ccm atafanya kosa hilohilo. I think it is high time now Wabunge wa upinzani wakajaribu kupractice caution in their doings cos hainisaidii kitu mimi kama mpigakura kusikia mbunge wangu katolewa nje kisa alingea bungeni bila kupata idhini ya spika/naibu spika au M/kiti. I hate it all,..... is it that hard just to go by the rules of the game?

Nadhani Bungeni linatawaliwa na sheria,kanuni na taratibu.Je kila mbunge akiongea bila kufuata utaratibu bunge litaendeshwa vipi ?.

Hebu wambie mwana, kanuni, taratibu lazma zifuatwe...hv hawa vijana wanaoshabikia cdm wanamtindio wa ubongo ama?

Nadhani Bungeni linatawaliwa na sheria,kanuni na taratibu.Je kila mbunge akiongea bila kufuata utaratibu bunge litaendeshwa vipi ?.

ndio tabu ya kuchagua wahuni nakuwapeleka bungeni wanazani pale ni kilabu cha pombe kila mtu anaropoka bila utaratibu.

Hiyo ni dalili ya anguko KUBWA SANAAA! Magamba watakiona cha moto 2015.Amin

Nadhani Bungeni linatawaliwa na sheria,kanuni na taratibu.Je kila mbunge akiongea bila kufuata utaratibu bunge litaendeshwa vipi ?.

Hapo kenya tu hawana hata mic bungeni? Ni spika tu kuimba order order order? Sasa hawa magamba wanafikiri pale ni room ta mitihani?

Kuna Mbunge mmoja wa CCM alishawambia wenzake hapo mjengoni, mchawi wa CCM sio CDM, bali ni watendaji wa CCM wenyewe!!!! Itawahusu baadae..........!!!! Na huyo mbunge akaongeza " Tanzania ni nchi pekee inayomshangaza hata Mungu" ....

Nadhani Bungeni linatawaliwa na sheria,kanuni na taratibu.Je kila mbunge akiongea bila kufuata utaratibu bunge litaendeshwa vipi ?.

tatizo ni pale wanapoomba nafasi ya kuomba muongozo wananyimwa. Wafanyeje ili wasikilizwe unadhani??

Labda naomba mwongozo hapo. Hivi ukitolewa bungeni je wanarudi tena au wanarudi kwenye next session.

[Kisa ni kitendo cha Naibu wa Spika kumpatia muda mrefu Lukuvi kuongea kuitetea serikali kuhusu na Hotuba ya Lema, Kambi ya upizani wamekataa kitendo hicho cha kupatiwa muda mrefu wakati si hotuba]

Muda ni muhimu sana hasa unapokuwa pale mjengoni, na hii ni kwa wale wenye ufahamu na uchungu wa hii nchi. Unapoona mtu anapewa airtime kubwa huku kunamambo mengi sana ya kupresent lazima watu wa riot tu!!! Na huyo kiti anaendesha Bunge kwa Jazba sana...!! bado anafikiri hili Bunge ni mabunge yaleyale ya ndio mzee!!!

Mungu hawafishi wanafiki, magamba wameila hii nchi imebaki tupu, mambo yote yatakuwa hadharani tu mwaka.

ccm wanabuni hila wasijibu hoja za msingi sababu wana dola,Cdm hawana jinsi otherwise wakubali matokeo mwisho waitwe vyama vya msimu! Dawa ya moto ni moto

Sehemu ya hotuba ya Lema, leo bungeni. Kuna paragraph moja (nitaiweka baadae katika mjadala huu) Naibu Spika alimzuia kuisoma kabisa. Hivi lini Magamba hawa watakubali kukosolewa na kujibu hoja za wapinzani wao kwa hoja zenye mantiki. Serikali ya CCM wajenge hoja wasipayuke (Argue! Don't shout, Prof. Shivji in Intellectuals at The Hill).

"Mheshimiwa Spika,Mpigania haki za watu weusi wa nchini Marekani, Hayati Dr. Martin Luther King, Jr. aliwahi kusema kwamba “peace is not the absence of war but merely the presence of Justice”, yaani “amani si hali ya kutokuwepo vita, bali ni uwepo wa haki”. Kwa kipimo hiki cha amani, nchi yetu haina amani kama viongozi wa serikali na wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanavyodai kila mara. Hii ni kwa sababu, licha ya ukweli kwamba Tanzania hakuna vita, pia ni dhahiri Tanzania sio nchi ya haki. Nathibitisha;"

sasa hicho kifungu kina shida gani? magamba bana watakwambia eti ni uchochezi...

kanuni za bunge zinasema taarifa inayotolewa inatakiwa iwe fupi na hata maswali yanapaswa kuwa mafupi ndio maana hata moses machali alizuiwa kuuliza swali lake kwa sababu lilikuwa lefu. Kwa nini lukuvi aruhusiwe kutumia muda mrefu kiasi hicho????????????????????????????????

CCM wanacheza ngoma ya CHADEMA, yaani ki-strategy CHADEMA wanapaa nje na ndani ya bunge. Unapomtoa mpinzani nje ya bunge wakati yeye ndiyo sababu ya watu kuwa na shauku ya kuangalia bunge ni kama, unawatia hasira wananchi na kuzidisha chuki dhidi ya majority. Bunge hili lilitakiwa kuendeshwa na Sitta, alikuwa anajua kucheza ngoma ya wananchi, matokeo yake leo hii Sitta amejingea heshima kubwa kwa kuwa fair kwa masilahi ya nchi. CCM wanajikaanga kwa mafuta, Spika na washirika wake wanacheza kuwafurahisha waliowaweka katika nafasi hizo badala ya kuangalia Taifa. 2015 si mbali, wataiba kura ila hawataongoza bali watatawala, kiongozi ni yule mwenye ridhaa ya wananchi ambao hufanya nao kazi kwa maendeleo, mtawala ni yule anayetumia mabavu kujiita kiongozi na huyo kamwe hana nafasi mbele ya wananchi.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom