Bunge lawaka moto: Lissu, Msigwa na Lema watolewa nje!

Wametolewa nje na Naibu speaker kwa kosa la kuongea/Kuwasha MIC bila ruhusa ya Naibu Speaker
Kuna haki hapo?
Wamevunja kanuni, baada ya kuona Naibu spika akiwabania upinzani na kuwapa upendeleo wa wazi wale jamaa wa chama tawala. Ni kweli hawajaonewa lakini tatizo ni kwamba sheria za Bunge sijui ni kanuni za Bunge zinafanya kazi kwa wapinzani tu1 Huku waziwazi zikikibeba chama tawala. Mi nafikiri katiaka katiba mpya inayokuja Spika na Naibu wake wasiwe watanzania. Sanasana napendekeza awe Mchina, Mjapani au Mkorea.
 
Wametolewa nje na Naibu speaker kwa kosa la kuongea/Kuwasha MIC bila ruhusa ya Naibu Speaker
Kuna haki hapo


kila lenye mwanzo haikosi kuwa na mwisho. naipata laivi hapa mwanza TBC bila chenga (kingamuzi) nimepatwa na hasira sana ndugu zangu. sasa kama huwezi kusha MIC utaptaje mwongozo wa spika? kudadadeki
 
Hii ni hatari sana kwa hawa wanaongoza bunge kwa manufaa ya CCm,swala tuwatie adabu kwa wananchi kuichagua CDM
 
Hivi lukuvi ana mamlaka gani kuchambua hotuba kwa mda wote? Je kwanini lukuvi akiomba utaratibu au mwongozo hupewa kwa haraka? Mbona lukuvi alipoomba utaratibu aliomba kwa kuwasha mic. Spika,naibu, na wenyeviti wao jirekebishen la sivyo bunge litawashinda.
 
Hizo sheria, kanuni na utaratibu ina apply kwa chadema tu? Mbona wabunge wa ccm wanaongea bila kufuata hizo taratibu and no action taken?
 
sio utoto mkuu, hawa watu wanafanya mambo kwa makusudi na hata bila kuangalia maslahi ya taifa, ukiamua 'kufuata sheria' ina maana cdm wameumia (na tayari wameshaumia huko nyuma). Hii ndiyo njia pekee iliyobakia ...mwaga ugali nasi tunamwaga mboga! La muhimu kuliko yote ni kuwa UMMA unaona na kujua kinachoendelea. Watch out
Ni ule ule utoto wa CDM, Hata ningekuwa spika ningewatoa nje wanaozomea wakati wenzao wanaongea. Haiwezekani CDM tu wajione ndio wana haki ya kuongea.
 
Wametolewa nje na Naibu speaker kwa kosa la kuongea/Kuwasha MIC bila ruhusa ya Naibu Speaker<br />
Kuna haki hapo?
<br />
<br />
Kwani ni lazima waende mjengoni dom? Kwa nini wasije huku mwembe yanga wakalianzisha la mtaaa hadi kieleweke?
 
ni kweli tz hakuna amani kuna utulivu tu na uoga, kama hawaamini waache kutembelea mahoteli makubwa, waje huku uswahilini, kwenye baa, magulioni waone watu walivyokata tamaa. wengi wanaishia afadhali ya jana, mabenk kila siku yanauza vitu vya watu, haya sasa wenye biashara ya vitu vinavyoooza haraka kama pension, vokado, apple kutoka south huyu huyu kakosa umeme, je mkopo hatarudishaje ikiwa vyanzo vya nishati ya umeme vimemfilisi?
 
Anayeliharibu hili bunge ni Lukuvi, kila siku yy ndo anaomba mwongozo hata jana ndio kasabisha Wenje atolewe nje kwa miongozo yake ya kipuuzi hlf anajiona sana kisa jana mke wake alikuwa bungeni.
 
Hongera makamanda! washeni moto mkuubwa tu hao mabwanyeye naona wanashindwa kuuzima! kama vipi njooni kwetu wananchi tuingie mtani tuwatoe hao wezi
 
Ni ule ule utoto wa CDM, Hata ningekuwa spika ningewatoa nje wanaozomea wakati wenzao wanaongea. Haiwezekani CDM tu wajione ndio wana haki ya kuongea.
kuna wabunge wanaongoza kwa kuzome,kuwasha mic,kukejeli na ushabiki wa kichama kama wabunge wa CCM..
 
Wamevunja kanuni, baada ya kuona Naibu spika akiwabania upinzani na kuwapa upendeleo wa wazi wale jamaa wa chama tawala. Ni kweli hawajaonewa lakini tatizo ni kwamba sheria za Bunge sijui ni kanuni za Bunge zinafanya kazi kwa wapinzani tu1 Huku waziwazi zikikibeba chama tawala. Mi nafikiri katiaka katiba mpya inayokuja Spika na Naibu wake wasiwe watanzania. Sanasana napendekeza awe Mchina, Mjapani au Mkorea.

Dah! Mkuu umefikiri sana, Ni kweli mkuu yaani nimefurahi kwa hili wazo. Unajua hata kwenye mpira inatokea kuletwa refa kutoka nje pale uaminifu unapopotea. Itapendeza spika JET LI na naibu wake ni CYNTHIA ROTHROCK
 
wabunge watatu wa chadema wametolewa nje ya bunge baada ya kuomba muongozo bila ya ridhaa ya naibu spika, na hii ni baada ya lema kuwasilisha hotuba yake ya kambi ya upinzani. na baada ya kuwasilisha lukuvi aliomba mwongozo wa spika kwa kusema kuwa hoja ya lema aliyowasilisha ni ya uchochezi na akanukuu maneno ambayo yapo kwenye hoja "kuwataka askali wagome ili walipwe vizuri na kuondokana kukaa katika nyumba za bati (full suti) na c kwenda kuua wananchi wasio na hatia yaani na ya pili ni kheri ya vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha haki za binadamu" na ndipo msigwa, lissu na lema mwenyewe nao wakaomba mwongozo na ndipo ndugai alipowatoa.
 
Kisa ni kitendo cha Naibu wa Spika kumpatia muda mrefu Lukuvi kuongea kuitetea serikali kuhusu na Hotuba ya Lema, Kambi ya upizani wamekataa kitendo hicho cha kupatiwa muda mrefu wakati si hotuba. Naibu wa spika ametumia kiti kuwatoa nje ya ukumbi kwa kazi za siku ya leo. Mambo yalikuwa magumu kweli kiasi cha hata Lukuvi mwenyewe kushindwa kumalizia hotuba yake.

Nilimuona Lukuvi akitoa 'hotuba' badala kuomba mwongozo kama alivyodai. Na ni wazi kuwa Lukuvi hata Naibu Spika Ndugai wana uelewa mdogo sana tena sana kuhusu uendeshaji wa mijadala ya bunge yenye vyama tofauti vya kisiasa. Mh Lema kwenye hotuba yake ameweka wazi ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja kunukuu taarifa za kichunguzi toka mashirika mbalimbali lakini bado Lukuvi anasema kuwa Lema ametoa hotuba ya kichochezi!!! Watu 52 wamekufa kwenye mikono ya vyombo vya dola bila maelezo sahihi, hakuna uchunguzi au hatua zozote za kinidhamu dhidi ya wahusika. Sijui Lukuvi ana maoni gani kuhusu vifo hivyo?

Kitu kilichonistua zaidi ni pale Lukuvi aliposema kuwa Lema anawaambia polisi wasitii amri za mabosi wao. Kenya sasa hivi aliyekuwa mkuu wa polisi ana kesi ICC -kule Hague. Pengine mkuu huyo wa polisi wa Kenya alipewa amri boss wake lakini mauaji yakitokea anayewajibika ni yeye sio sio bosi wake. Lukuvi anatakiwa atambue kuwa sheria inamtambua aliyetenda kosa na sio 'boss'.

Kwa maana yangu askari wetu ni bora wakafuata ushauri wa Lema wa kutotii amri za 'kuua' maana hawana mamlaka kisheria kufanya hivyo.
 
Ni ule ule utoto wa CDM, Hata ningekuwa spika ningewatoa nje wanaozomea wakati wenzao wanaongea. Haiwezekani CDM tu wajione ndio wana haki ya kuongea.

Mkuu tujaribu zaidi kuangalia chanzo cha tatizo ni nini?Kwa nini wafanye huo utoto hali wao ni watu wazima?Ni lazima kuna kitu kimewakera,kabla ya kuwatoa nje huyo spika mdogo alitakiwa kuwapa nafasi ya kujitetea kwanza ili tuelewe kuna tatizo gani,hapo ndio tutaona haki iko wapi.
 
Back
Top Bottom