Bunge lawaka moto; Kamati ya Mrema, Cheyo zaibua ufisadi wa kutisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge lawaka moto; Kamati ya Mrema, Cheyo zaibua ufisadi wa kutisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 7, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu na ile ya Mashirika ya Umma, zimeibua ufisadi wa kutisha ulioligeuza taifa kuwa shamba la bibi.

  Kamati hizo ambazo zinaongozwa na Augustine Mrema (TLP), John Cheyo (UDP) na Zitto Kabwe (CHADEMA), ziliwasilisha taarifa zake za mwaka wa fedha wa 2008/2009 jana bungeni.

  Katika halmashauri za wilaya nchini, ufisadi mkubwa umebainika kuwepo katika ununuzi wa spea za magari kwa kuongeza bei isiyo halisi, bei ya kughushi katika ununuzi wa mafuta, matumizi makubwa kwa ajili ya posho kuliko utekelezaji halisi wa miradi kama ya (TASAF), Mazingira na miradi mingine ya maendeleo.


  Akiwasilisha taarifa ya kamati yake, Mrema alisema kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2008/2009, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ilitumia sh milioni 2.9 kwa ajili ya kutengeneza pikipiki ya Kichina, iliyonunuliwa kwa bei ya chini kuliko ile iliyotumika kuitengenezea.


  Alisema katika Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kamati yake ilibaini kuwa halmashauri ilitumia sh milioni 15 kwa ajili ya kununua spea ya gari (Injector Pump ya Land cruiser had top).


  "Lakini tulipofuatilia kwa kupiga simu kwenye duka lililouza spea hiyo, tuliambiwa bei yake ni sh milioni tatu," alisema Mrema na kuwaacha wabunge wakibaki na mshangao.


  Mbunge huyo wa Vunjo aliendelea kusema kuwa kuna wilaya nyingine ambayo hata hivyo hakuitaja, waligundua kuwa ilitengewa sh milioni 12 kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi, lakini kati ya hizo sh milioni kumi zilichakachuliwa na sh milioni mbili tu ndizo zilizowafikia walengwa.


  Kwa mujibu wa Mrema, katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha, taarifa za CAG zimebaini kuwa mali za sh milioni 111.2 zilitumika kununulia mali za halmashauri mbalimbali, lakini hazikuandikwa kwenye vitabu vya mali za halmashauri husika na sh milioni 158, zilitumika kununulia mafuta ambayo matumizi yake hayajulikani.

  Akiendelea kuibua ufisadi katika halmashauri za wilaya katika kipindi cha mwaka wa fedha 2008/2009, Mrema alisema sh milioni 792.9 katika halmashauri 40 nchini, zililipwa kama mishahara hewa kwa watumishi waliokwisha kufariki dunia na wengine kustaafu.


  Lakini wakati sh milioni 792.9 zikilipwa kama mishahara hewa, sh bilioni 1.7 za mishahara isiyokuwa na wenyewe haikurejeshwa hazina na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.


  Huku akisikilizwa kwa makini na wabunge, Mrema alisema kiasi hiki cha mishahara hewa kina uwezo wa kujenga madarasa 113 ya shule za msingi nchini.


  "Shilingi bilioni 328.2, zilizotolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika halmashauri 132, hazikutumika, sh bilioni 1.9 zilizokusanywa kama mapato ya ndani, katika halmashauri 43, hazikurejeshwa na mawakala kwenye halmashauri husika.


  "Katika mwaka huo huo, halmashauri 113, zilikuwa na jumla ya madeni yaliyofikia sh bilioni 35.6, katika mwaka huohuo, vitabu 1,341 vya makusanyo ya mapato mbalimbali, havikupatikana kwa wakaguzi katika halmashauri 50. Kutaja mifano michache tu," alisema Mrema.


  Ili kukomesha tabia hiyo, Mrema alisema kamati yake imependekeza mambo kadhaa ikiwemo kamati za Bunge za usimamizi kufuatilia fedha hizo mara zinapotolewa.

  Kuhusu mishahara hewa, Mrema alisema waliohusika kwanza wazirejeshe, pia Hazina iache utaratibu wa kutuma pesa kwenye akaunti ya watumishi moja kwa moja bila kupitia kwa waajiri wao.

  Cheyo na Kamati ya Hesabu za Serikali  Wakati Mrema akiibua ufisadi katika halmashauri za wilaya nchini, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu, John Cheyo, aliishukia Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba kuna makampuni ya kitalii ambayo yamekuwa yakifanya kazi bila leseni, hivyo kuikosesha serikali mapato.


  Alisema msako uliofanywa na wizara husika, ulibaini kuwa makampuni 23 yalikuwa yakifanya kazi bila leseni, hivyo kuikosesha serikali mapato. Aliilipua pia Wizara ya Fedha na Uchumi kwamba Februari 25 mwaka 1999, ilisamehe ushuru wa makampuni ya madini kulipia ushuru wa mafuta ya dola za Marekani 200,000.


  Akizungumzia deni la taifa, Cheyo alisema limefikia sh trilioni 6.4 na kwamba linaendelea kukua kwa kasi. Mbali ya deni la taifa, Cheyo pia alisema wizara kadhaa zina mzigo wa madeni, hali ambayo inaweza kuathiri bajeti ijayo.


  Akitolea mfano, alisema Wizara ya Miundombinu ilikuwa na madeni ya sh 742,920,080.58 na mihadi iliyofikia sh 178,596,360,000.


  Alisema yapo madeni mengine kadhaa ya wizara na idara za serikali kama vile elimu, Jeshi la Polisi, Magereza na Wizara ya Afya na kuongeza kwamba madeni hayo yanatokana na uzembe wa maofisa masuhuli. "Haya ni madeni ambayo wizara inaenda nayo katika mwaka wa fedha unaofuata. Wasiwasi ni kwamba madeni haya yataathiri bajeti inayofuata kwa kulipia madeni," alisema Cheyo.


  Kamati ya Zitto Kabwe


  Kwa upande wake, Zitto Kabwe alisema kuwa fedha nyingi za umma zimepotea katika suala la manunuzi ya mali za umma.

  Akitolea mfano, Zitto alitaja manunuzi yasiyozingatia sheria ya manunuzi kama yale yaliyofanywa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) ambapo sh 102,285,441 zilitumika.


  Pia alizungumzia Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwamba linapaswa kuwezeshwa kama serikali ilivyokuwa ikifanya lilipokuwa likiendeshwa kwa ubia ambapo ilikuwa ikipata sh milioni 500 kila mwezi.


  Tundu Lissu amvaa tena Ngeleja


  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, jana alimvaa tena Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimtaka ajibu kwa ufasaha majibu ya maswali ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), aliyetaka kujua Shirika la Umeme nchini (TANESCO), linapata wapi fedha za kununulia mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL.


  Lissu (CHADEMA) ambaye juzi alitoa kauli bungeni kwamba Waziri Ngeleja ni muongo na kutakiwa kuthibitisha kesho, aliomba mwongozo wa Spika akitaka waziri huyo ajibu maswali ya Zitto kwa ufasaha. "Mheshimiwa Spika, kanuni zinasema waziri atakuwa na wajibu wa kujibu swali la mbunge kwa ufasaha ndani ya Bunge isipokuwa kwa swali linalohitaji takwimu na vielelezo vingi. Swali la Mbunge (Zitto), halihitaji takwimu za aina hiyo. Naomba ajibu kwa ufasaha," alisema Tundu Lissu.


  Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema kuwa mwenye uwezo wa kumtaka waziri ajibu swali kwa ufasaha ni Spika na kama mbunge anaona jibu lake halijakamilika, anapaswa kufuata taratibu. Someni kanuni vizuri," alisema.


  Awali akijibu swali la msingi la Zitto, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Kampuni ya IPTL, hutumia sh bilioni 15.62 kwa mwezi kwa ajili ya kugharimia ununuzi wa mafuta mazito ili kuendesha mitambo hiyo.


  Waziri Ngeleja, alisema kiasi cha sh bilioni 46.4 au wastani wa sh bilioni 15.62 kila mwezi huitajika kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa tani 36,800 za mafuta mazito (HFO) kwa kipindi cha miezi mitatu.


  Ngeleja alisema kuanzia Novemba 15 mwaka 2010 hadi Februari 14, 2011 sawa na tani 400 ya mafuta mazito hutumika kwa siku.


  Alisema pamoja na hatua zote hizo, hivi sasa kampuni mbili za Oryx na Total ndizo pekee zinazofanya biashara ya mafuta mazito na ndizo zilizoombwa kushiriki katika mchakato wa ununuzi wa mafuta hayo.


  Waziri Ngeleja alisema utaratibu unaotumika kupata kampuni za Oryx na Total ni kwa ‘Restricted Tendering' ambapo kampuni za mafuta zilitakiwa kufikisha mafuta katika maghala ya IPTL kuanzia Novemba 2010.

  Aidha, alisema katika hali ngumu kama hiyo maamuzi ya serikali yalihitajika kufanyika kwa haraka ili kupunguza ukali wa mgawo wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya taifa.

  Alisema fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo ya IPTL hutoka katika mfuko mkuu wa serikali.


  Waziri Ngeleja pia alisema serikali bado ina nia ya kuibadili mitambo ya IPTL kutumia gesi, lakini inashindwa kufanya hivyo kutokana na kesi iliyopo mahakamani iliyofunguliwa na IPTL dhidi ya TANESCO.


  Hata hivyo majibu hayo yalimfanya mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani kuuliza swali dogo la nyongeza ambapo alihitaji kufahamu fedha hizo za kununulia mafuta hayo mazito zinatoka katika bajeti gani.

  Alisema kwa sasa TANESCO iko kwenye mvutano wa kisheria na IPTL na kila siku hulipa sh bilioni 3.6 na kuziingiza kwenye mfuko maalumu na kuna zaidi ya sh bilioni 1.6 zimehifadhiwa humo.


  "Ni kweli fedha hizo haziko kwenye bajeti lakini namtaka mbunge aje pale kwenye ofisi zetu tumuonyeshe wapi fedha hizo zinatoka," alisema Ngeleja. Jibu hilo ndilo lililomfanya Lissu kuomba mwongozo wa Spika kutaka Ngeleja ajibu kwa ufasaha.
   
 2. M

  Majasho JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  big up Mrema na Cheyo, kinachonishangaza kamati ya serikali ya mitaa ilikuwa chini ya Slaa in the last five years, mwaka wa kwanza wa Mrema, 4 and half years to go
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KWA MTAJI WA VIWANGO VYA UFISADI WA KI-MFUMO ZAIDI NCHINI, DAWA YA KUDUMU YA UGONJWA HUU WA 'UFISADI WA KI-MFUMO' NCHIN TIBA YAKE YA KUDUMU NI MPAKA 'KATIBA MPYA' NA WALA SI HIZI 'HUDUMA ZA KWANZA' ZITOLEWAZO NA KAMATI ZA BUNGE!!!

  Acha hao Wenyeviti wa kupachisha Kamati mbalimbali za Bunge wakatutolee tiba za muda mfupi kwa UFISADI uliokithiri nchini kwa kujitangazia kwamba mara huyu kagundua hili yule kagundua lile.

  Lakini ukweli wa mambo ni kwamba Tanzania tunahitaji KUJENGA Mfumo Mpya unaojisimamia na kujidhiti yenyewe bila mianya mingi inayotulzimu kila siku kutumia nguvu nyingi kuchunguza UBADHIRIFU wa mali ya umma badala ya kutumia nguvu kama hizo kupiga hatua zaidi kimaendeleo kwa kutumia hizo rasilmli zinazotumika kama gharama ya ufuatiliaji hapa. Jibu la mfumo kama huo (a stringently self-checking system of governance) jibu lake liko kwenye KATIBA MPYA.

  Nadhani mpaka hapa tuachane kabisa na kuvutwa attention zetu kwenye side-issues wakati ambapo masula mazito kama kuundwa upya kwa katiba inapozungumzwa ndani ya taifa letu. Acha akina Mrema, Zitto, Cheyo na wengine wote hao wagunduesana tu mi-uchafu mingi huko lakini sisi kata Umma wa Tanzania FOCUS yetu kama taifa safari hii kamwe haitoondolewa kwenye suala nyeti la Muswada wa kuundwa kwa Baraza la Taifa la kuratibu Katiba Mpya na hatima yake nchini.

  Katu sitopoteza muda wangu kujadili SYMPTOMS ya wizi wa rasilmali za Umma nchini wakati najua fika kwamba CHANZO ya hayo yote ni kule kuzeeka na kuchakaa ovyo kwa katiba ya nchi.

  Tiba kwa ufisadi ndani ya wizara na au taasisi fulani ni jambo jema sana tu japo kwa wakati husika tu, ila nikishirikiana kufa na kupona pamoja na Watanzania wenzangu kulipa gharama yoyote ile kuleta Katiba Mpya yenye kuwakilisha matumaini ya leo na kesho na hadi hapo basi nitakua niacha urithi wa heshima sana kuwapa wananchi mamlaka zaidi kudhibiti ufisadi kama hayo waliogundua akina Mrema kwa msingi na mtindo endelevu zaidi.

  Sasa tuchague katia ya mikakati endelevu au ule wa zima moto na tuwe tayari kuishi na matokeo ya chaguo letu siku zote!!
   
 4. S

  Shiefl Senior Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Majasho, kama ulivyoweka jina lako Majasho naamini kweli wewe unafanana nyoka ambaye katika biblia tunaambiwa alimdanganya Adam na Eva wakala tunda na Adam akaambiwa kwa jasho utakula

  Kwa mda wote Dr Slaa ameibua ufisadi mpaka wa Maraisi wa nchi siyo wa hizi million 15 au chache za Halmashauri ambazo wewe unataka kubeba sifa.

  Nenda kasifie chumbani kwako na siyo kumwita Dr wa watu padri hapa.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wewe ni kati ya mipumbavu, mikurupukaji, midini tuliyo nayo JF...
   
 6. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mimi sitaki story za kuibua ufisadi. Nataka mtu makini wa kuibua mbinu makini za kuzuia ufisadi. Wenzetu waliotutangulia wametupatia program inayokusadia kutumia pesa yako kulingana na bajeti maarufu kama EPICOR system. Itakupatia kumbukumbu zote za matumizi na inaku limit unapoanza kwenda zaidi ya ukomo wa bajeti. Waswahili sisi hatuipendi kabisaaaaa. Hatutaki ukweli. CAG ameasa vizuri na amesema, tusiwe mahili eti kujibu hoja bali tuwe mahili kuzuia hoja. Taarifa zote za mapato na matumizi zilitakiwa kuwa kwenye soft copy, zitumwe kwenye kamati ya ALM, wazisome hukohuko, wajibizane kimtandao atakaeshindwa kujustify ndie aitwe kwa hatua zaidi. Kuita wakurugenzi na wakuu wao wa idara wa halmashauri kuifuata kamati dsm ni matumizi mengine mabaya ya fedha za umma. Mafuta na spea za magari, posho nk. No! We are not serious. Tatizo, je, kamati ni mahali wa software?
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mimi sitaki story za kuibua ufisadi. Nataka mtu makini wa kuibua mbinu makini za kuzuia ufisadi. Wenzetu waliotutangulia wametupatia program inayokusadia kutumia pesa yako kulingana na bajeti maarufu kama EPICOR system. Itakupatia kumbukumbu zote za matumizi na inaku limit unapoanza kwenda zaidi ya ukomo wa bajeti. Waswahili sisi hatuipendi kabisaaaaa. Hatutaki ukweli. CAG ameasa vizuri na amesema, tusiwe mahili eti kujibu hoja bali tuwe mahili kuzuia hoja. Taarifa zote za mapato na matumizi zilitakiwa kuwa kwenye soft copy, zitumwe kwenye kamati ya ALM, wazisome hukohuko, wajibizane kimtandao atakaeshindwa kujustify ndie aitwe kwa hatua zaidi. Kuita wakurugenzi na wakuu wao wa idara wa halmashauri kuifuata kamati dsm ni matumizi mengine mabaya ya fedha za umma. Mafuta na spea za magari, posho nk. No! We are not serious. Tatizo, je, kamati ni mahili wa software?
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hii report aliyosoma Mh. Mrema ni ya hesabu za Serikali za Mitaa zilizowasilishwa Bungeni mwezi April 2010 wakati huo Mrema hakuwa Mbunge. Mpaka 2010 mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali za Mitaa alikuwa ni DR Slaa mpaka Bunge lilipovunjwa. Mh Mrema alichaguliwa January 2011 tuu mwaka huu hivyo report aliyosoma ni mwendelezo wa kazi iliyofanywa na kamati iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dr. Slaa. Naandika haya kwa maana sifa zote mnaelekeza kwa Mh. Mrema wakati yeye amesoma tuu report iliyoachwa na mtangulizi wake. Kwa upande wa Mh Cheyo na Zitto hao walikuwa wenyeviti wa kamati zilizomaliza muda wake hivyo wamehusika kikamilifu katika kuandaa taarifa walizosoma Bungeni
   
 9. M

  Majasho JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  we ni chadema ndio maana imekutachi...ukweli siku zote unaumwa..chadema wenyewe nyinyi ni wadini..washenzi
   
 10. M

  Majasho JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  yeye ni padre na atakuwa padre..fikra za upande mmoja zinakupotosha, chadema mkiambiwa ukweli mnakasirika...padre analitewa makaratasi na nyaraka kuhusu ufisadi yeye anazisema kwenye majukwaa, alipewa pia jukumu la kuchunguza serikali za mitaa lakini yeye alizunguka kukijenga chama badala ya kufuatilia..hata mimi mtu akiniletea nyaraka za ufisadi naweza kuziongelea hapo jangwani...
   
 11. H

  HisiaZAkweli Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kazi rahisi kama unavyoona...hupewi nyaraka...unapewa na vitisho vingi na vya aina yake...usidharau kitu eti kwa kuwa we unaweza...wangapi hawakuthubutu,jiulize???:disapointed:
   
 12. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Mimi naona gazeti wamewapa sifa hawa jamaa kuliko kazi waliyofanya. Story inazungumzia milllion 10 to 30 wao wanasema ufisadi mkubwa. Mbona wanapokuja na story za mabillion mhalili hazipi uzito hivyo kwa kuwa zinawagusa vigogo. Kulinganisha kazi Slaa na ALM ni mzaha wa hali ya juu. Mimi naona hizi kamati this time zinafanya kazi nje ya mipaka yao ndiyo sababu wanatuletea viskendo mtoto hapa badala ya kufuatilia issue za maana. Halimashauri zina miradi mingi mikubwa halafu wao wanazungumzia million 10, halafu waita ufisadi wa kutisha utafikiri hatujawahi kusikia vitu kama EPA, Kagoda, Meremeta, IPTL, Richmond, Dowans n.k!!!
   
 13. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Challenge the issue, leave the man alone. In case you fail to challenge issues know that you dont belong in here, you are not a great thinker...
   
Loading...