Mahindi ni Nishati.Bunge limesitisha kwa muda shughuli zake za leo ili kujadili changamoto ya bei duni inayowakumba wakulima wa mahindi nchini. Wabunge wameeleza kutoridhishwa na bei ndogo ya mahindi, bei ghali ya mbolea hivyo wameitaka Serikali kuiongeza hela NFRA ili inunue mahindi kwa wakulima.
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda amekiri uwepo wa tatizo la bei ndogo ya mahindi. Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kushughulikia suala hilo ambapo ameahidi kuwa kabla ya Bunge kuhitimishwa hapo kesho Serikali itatoa tamko bungeni kuhusu hatua ilizochukua.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imesikia kilio na Serikali na kupitia NFRA ilianza kununua mahindi kwa wakulima lakini imegundua kuwa uzalishaji wa mwaka huu ni mkubwa na Serikali imefanya mazungumzo na mataifa jirani ili kununua mahindi hapa nchini.
Hili halina maswali liko dhahiri.
Kilimo cha Mahindi ni Kilimo kisichokoma-Hili Ndilo zao letu la Msingi.
Tatizo ninaloliona katika hili zao ni hivi:
1.Kwanza kabisa ni nini BEP(Break Even Point)Ya Kilimo cha Mahindi kwa Ekari moja?
2.Kwa ni nini tunadhani Tsh 50000 kwa gunia ni bei ndogo?
3 Hayo Mahindi yako wapi?
Kwa nani?
Hii ni sawa na kufuga ndege walioko kwenye Miti huko shambani halafu unajihesabia kwamba ni Mali ya familia-Simply kwa sababu wamekaa juu ya mti wa nyumbani.
Tizama:
FWP walitoa takwimu za Post Harvest Losses kuwa ni mpaka 40%...
Hapa ndipo ilipo economic intelligence...
Serikali Itafute suluhisho l UHIFADHI WA MAHINDI KWA KUWEKEZA KWENYE MODERN SILOS-?integrated.
Silos nyingi kwa kila Mkoa..
Na hizo ziitwe FOOD BANKS-THEN BIASHARA IANZIE HAPO.
YAKO NA MENGINE MENGI BUT LET US START FROM THIS ANGLE.