Bunge lasitisha Shughuli zake ili kujadili bei ndogo ya Mahindi nchini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Bunge limesitisha kwa muda shughuli zake za leo ili kujadili changamoto ya bei duni inayowakumba wakulima wa mahindi nchini. Wabunge wameeleza kutoridhishwa na bei ndogo ya mahindi, bei ghali ya mbolea hivyo wameitaka Serikali kuiongeza hela NFRA ili inunue mahindi kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda amekiri uwepo wa tatizo la bei ndogo ya mahindi. Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kushughulikia suala hilo ambapo ameahidi kuwa kabla ya Bunge kuhitimishwa hapo kesho Serikali itatoa tamko bungeni kuhusu hatua ilizochukua.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imesikia kilio na Serikali na kupitia NFRA ilianza kununua mahindi kwa wakulima lakini imegundua kuwa uzalishaji wa mwaka huu ni mkubwa na Serikali imefanya mazungumzo na mataifa jirani ili kununua mahindi hapa nchini.
 
Soko liko nje. Nchi ifunguliwe kwelikweli wakulima/wafanya biashara wajiconnect na masoko ya nje kama umasikini wa kutupwa utaendelea kuwepo nchini. Hii kuendekeza umachinga badala ya kuvutia vijana kwenye kilimo inaua nchi.

Kenya sasa ndio imekuwa dalali mkuu wa Tanzania. Mazao yanakimbiziwa Kenya ndio yawe exported. Viongozi Tz wamekalia talalila za kisiasa huku wanawawekea kauzibe wanaotaka kujiendeleza kimataifa kupitia kilimo.
 
Kulipo kulipia ununuzi wa ndege ni kheri Serikali ikazipeleka hela hizo NFR wanunulie hayo mahindi kwa bei nzuri.

Nchi nyingi serikali zao zinanunua mazao ya wakulima wao hata Kama soko lipo zuri.

Aidha ikitokea uzalishaji umekuwa mkubwa kulipo mahitaji ya ndani Serikali pia inaingilia kwa kununua mazao yote yaliyobaki na kuyahifadhi.

Au Serikali zao zinawalipa wakulima fedha kufidia gharama zao za uzalishaji huku wakiachiwa mazao yao wayatumie kwa namna nyingine Kama chakula cha mifugo.

Yaani kwa kifupi Serikali zao zinafanya juu chini mkulima asipate hasara kwa namna yeyote ile.
 
Nchi za SADC ni walaji wakuu wa mahindi. Kutokana na Globalisation wakazi wengi wa nchi hizi wanaishi Ulaya, Marekani na Australia. Hawa ni wateja wazuri wa unga wa mahindi.

Kampuni ya Iwisa ya South Africa imefanikiwa kupeleka unga wa Iwisa nchi zote nilizotaja hapoejuu. Waganda pia wanasafirisha unga wa Maganjo kwenda Sweden.

Wasomi wetu mnakwama wapi?
 
Akili yako ni kusipend tuuuuuu kuinvest hapana.

Hongera sana
 
Serikali ifungue mipaka ya soko la nje ili tukauze huko. Hakuna haja ya kujadili Mambo ya kizembe hivyo. kwani hawajui tatizo? Au wanataka waunde kamati za kijinga
 
Tanzania kuendelea kwa akili hizi hata miaka 10,000 haiwezekani.

Miaka zaidi ya 60 ya uhuru bunge linajadili kuuza mahindi kama mahindi badala ya kuuza bidhaa zitokanazo na mahindi kweli......!

Hakika hata huko shuleni tunafundishana ujinga ujinga tu.
 
Soko liko nje. Nchi ifunguliwe kwelikweli wakulima/wafanya biashara wajiconnect na masoko ya nje kama umasikini wa kutupwa utaendelea kuwepo nchini. Hii kuendekeza umachinga badala ya kuvutia vijana kwenye kilimo inaua nchi.

Kenya sasa ndio imekuwa dalali mkuu wa Tanzania. Mazao yanakimbiziwa Kenya ndio yawe exported. Viongozi Tz wamekalia talalila za kisiasa huku wanawawekea kauzibe wanaotaka kujiendeleza kimataifa kupitia kilimo.
Machinga wamekuwa kipaumbele kuliko sekta ya kilimo.

Hii ni aibu ya karne mashamba ni mengi lakini nani atakubali kulima mahindi gunia 50tsh mpaka 60tsh wakati kwenye umachinga mtu unapata mpaka laki kwa siku?

Acha siasa zishike mkondo wake siku moja wanakiji mikoani ndio watakumbuka kujikwamua wenyewe
 
Yaani swala la kununua mahindi ni la kubembelezana, wakati mamlaka ya hali ya hewa imetabiri upungufu mkubwa wa mvua ambao utapelekea kushuka kwa mavuno, au mtafanya collabo na machifu mlete mvua.
 
Nchi za SADC ni walaji wakuu wa mahindi. Kutokana na Globalisation wakazi wengi wa nchi hizi wanaishi Ulaya, Marekani na Australia. Hawa ni wateja wazuri wa unga wa mahindi.

Kampuni ya Iwisa ya South Africa imefanikiwa kupeleka unga wa Iwisa nchi zote nilizotaja hapoejuu. Waganda pia wanasafirisha unga wa Maganjo kwenda Sweden.

Wasomi wetu mnakwama wapi?

Miaka ya nyuma kuna mtu alileta unga wa mahindi nakumbuka mpaka baadhi ya miji kama Milton Keynes walinunua na kufumba na kufumbua mzigo uliisha

Ila tangu hapo jamaa hakuleta tena na sijui alipatwa na nini
Labda uhujuma uchumi kwa kupeleka unga nje ya nchi, hatuwezi kujua laana zetu huwa zinaibuka tu
 
Toka mwanzo nilisema, pesa waliyopewa NFRA ni matusi kwa wakulima wa nchi hii!! Wakulima wanadhoofishwa na pia tunaiweka nchi hatarini kwa kukumbwa na janga la njaa endapo mvua hazitakuwa nzuri msimu ujao wa kilimo! Pesa za Tozo baadhi zipelekwe NFRA maana kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu, waongezewe pesa!!!
 
Bunge limesitisha kwa muda shughuli zake za leo ili kujadili changamoto ya bei duni inayowakumba wakulima wa mahindi nchini. Wabunge wameeleza kutoridhishwa na bei ndogo ya mahindi, bei ghali ya mbolea hivyo wameitaka Serikali kuiongeza hela NFRA ili inunue mahindi kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda amekiri uwepo wa tatizo la bei ndogo ya mahindi. Ameeleza kuwa Serikali inachukua hatua za haraka kushughulikia suala hilo ambapo ameahidi kuwa kabla ya Bunge kuhitimishwa hapo kesho Serikali itatoa tamko bungeni kuhusu hatua ilizochukua.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imesikia kilio na Serikali na kupitia NFRA ilianza kununua mahindi kwa wakulima lakini imegundua kuwa uzalishaji wa mwaka huu ni mkubwa na Serikali imefanya mazungumzo na mataifa jirani ili kununua mahindi hapa nchini.
Hayo masuala ya nchi jirani ni upuuzi tu, NFRA inunue kwanza hayo mahindi, then ndio utaratibu wa kuuza nje ufanyike!
 
Yaani swala la kununua mahindi ni la kubembelezana, wakati mamlaka ya hali ya hewa imetabiri upungufu mkubwa wa mvua ambao utapelekea kushuka kwa mavuno, au mtafanya collabo na machifu mlete mvua.....

Yaani halafu kuna mijitu inajisifu inanunua ndege
 
Toka mwanzo nilisema, pesa waliyopewa NFRA ni matusi kwa wakulima wa nchi hii!! Wakulima wanadhoofishwa na pia tunaiweka nchi hatarini kwa kukumbwa na janga la njaa endapo mvua hazitakuwa nzuri msimu ujao wa kilimo! Pesa za Tozo baadhi zipelekwe NFRA maana kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu, waongezewe pesa!!!

Halafu watu wanajisifu wananunua ndege hizo hela za kununulia ndege zipelekwe NFRA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom