Bunge lapitisha sheria ya kuanzishwa mahakama ya ufisadi


N

Ndeko

Member
Joined
Jul 31, 2012
Messages
85
Likes
66
Points
25
N

Ndeko

Member
Joined Jul 31, 2012
85 66 25
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana lilipitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho Mbalimbali, ambayo pamoja na mambo mengine, yamempa Jaji Mkuu mamlaka ya kuanzisha Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ya Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa muswada huo uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, adhabu kwa watakaokutwa na hatia zimeongezwa, huku mahakama hiyo ikiwekewa mazingira wezeshi ili iendeshe kesi hizo kwa haraka.

Mazingira wezeshi
Muswada huo wa sheria ambao kwa sasa utakuwa ukisubiri Rais ausaini ili iwe sheria kamili, umekusudia kuanzisha divisheni hiyo ya mahakama, ambayo itakuwa na majaji wake na watumishi wake wanaojitegemea.

“Divisheni Maalumu ya Mahakama Kuu, itakuwa na majaji pamoja na watumishi wengine, ambao wanahusika moja kwa moja na kesi za rushwa na uhujumu uchumi tu.

“Hatua hii itawezesha kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kusikilizwa kwa urahisi, ufanisi na kwa haraka,” alisema Masaju wakati alipokuwa akisoma muswada huo kabla ya kupitishwa na Bunge.

Hatua hiyo ya kuwa na majaji maalumu na wafanyakazi wake, Masaju alisema imelenga kuondoa udhaifu uliojitokeza wakati wa kushughulikia kesi za rushwa na uhujumu uchumi, kwa kuwa majaji waliokuwa wakisikiliza mashauri hayo, walikuwa hao hao wanaosikiliza mashauri mengine ya jinai, madai, katiba na mengine yanayofunguliwa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa Masaju, hali hiyo ilisababisha uendeshaji wa kesi za rushwa na uhujumu uchumi, kutokuwa na tofauti na uendeshaji na usikilizwaji wa kesi zingine.

Mazingira mengine wezeshi yanayotengenezwa na sheria hiyo kwa divisheni hiyo, ni thamani ya fedha inayohusishwa na makosa hayo, kuwa inaanzia Sh bilioni moja.

“Inapendekezwa kuwa pale makosa ya rushwa na uhujumu uchumi yanapohusisha thamani ya fedha, basi makosa yatakayofunguliwa katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, yawe ni yale ambayo thamani yake haipungui Sh bilioni moja,” alisema Masaju.

Lengo la kuweka thamani hiyo ya fedha, limeelezwa kuwa ni kuiwezesha divisheni hiyo kujikita kusikiliza makosa makubwa ya rushwa na uhujumu uchumi, ili makosa madogo yasiyofikia thamani hiyo, yasikilizwe na mahakama za wilaya, mahakama za hakimu mkazi na Mahakama Kuu.

Thamani hiyo ya fedha, imetajwa pia kusaidia kuharakisha usikilizwaji wa makosa hayo bila kuathiri ufanisi na kupunguza msongamano wa mashauri katika divisheni hiyo.

Hata hivyo, divisheni hiyo pia kwa mujibu wa sheria hiyo itasikiliza makosa mengine ya rushwa na uhujumu uchumi bila kujali thamani ya fedha, kutokana na namna makosa hayo yalivyotendeka, asili yake na ugumu wa kuyawekea thamani ya fedha.

Pia Mkurugenzi wa Mashitaka amepewa mamlaka ya kutoa hati ambayo itataka mashauri mengine yatakayofunguliwa, yasikilizwe katika divisheni hiyo kwa maslahi ya umma.

Kifungo, utaifishaji mali
“Marekebisho mengine yanayopendekezwa… ni kwamba makosa ya rushwa na uhujumu uchumi chini ya sheria hii iwe ni kifungo cha gerezani, kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja na hatua nyingine za kijinai, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizopatikana kutokana na makosa hayo,” alisema Masaju wakati akiwasilisha muswada huo.

Kifungo hicho kimeongezwa kutoka katika sheria ya sasa ambayo ndiyo inayorekebishwa, ambayo ilitaka kifungo kisizidi miaka 15.

Kwa mujibu wa Masaju, maneno hayo “kifungo kisichozidi miaka 15”, yaliipa Mahakama mamlaka ya kutoa adhabu ndogo zaidi, ilimradi tu adhabu hiyo haizidi miaka 15, jambo lililoonekana kuwa baadhi ya adhabu zilikuwa ndogo kuliko uzito wa makosa.

Katika kutaifisha mali za waliokutwa na hatia, sheria hiyo imeweka masharti ya kuzuia kutumika kwa sheria zinazohusu ufilisi au uamuzi wa kufilisi kampuni, kwa mali ambayo inachunguzwa chini ya Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi.

“Marekebisho hayo yanalenga kukabili vitendo vya watu au kampuni kujifilisisha wakati uchunguzi unapoanza dhidi yao na pia kuhakikisha kuwa mali zote zinazohusika na kosa linalochunguzwa, au linaloendelea mahakamani, inaendelea kuwepo hadi uchunguzi au kesi husika itakapohitimishwa,” alisema Masaju.

Hatua hiyo imetajwa kuwa na nia ya kuiwezesha serikali kutaifisha mali hiyo, wakati kesi husika itakapokamilika na ikathibitika kuwa ina uhusiano na kosa la rushwa na uhujumu uchumi lililothibitishwa mahakamani.

“Kwa ujumla hatua hii ni njia mojawapo ya kuwafanya watu waogope kutenda makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na pia kuhakikisha kuwa mhalifu, hanufaiki na uhalifu alioutenda kwa kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi,”
alisema.

Ulinzi wa mashahidi
Marekebisho mengine yaliyoingia katika sheria hiyo, yanahusu ulinzi wa mashahidi, ambapo Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), kwa kushauriana na Mkurugenzi wa Mashitaka, wanatakiwa kuweka utaratibu wa kuhakikisha usalama wa shahidi pamoja na familia yake.

Lengo ni kusaidia usalama wa mashahidi wa kesi hizo, ili mashahidi wawezeshwe kutoa ushahidi wao bila woga, kwa kuwa kesi hizo zinahusisha watu wenye fedha na makosa yanayofanyika ni ya kupanga.

Maoni ya wabunge
Akichangia maoni yake kuhusu muswada wa sheria hiyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe, alisema tangu amekaa bungeni, hajawahi kuona majadiliano ya kina kwenye kamati kati ya Kamati ya Bunge na serikali ambayo yalidumu kwa wiki mbili.

Wabunge wengine, akiwemo Hussein Bashe wa Nzega Mjini (CCM), Mbunge wa Ileje, Janet Mbene (CCM), Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba (CCM) na Mbunge wa Muheza, Adadi Rajab (CCM), walitaka Serikali kuiwezesha mahakama hiyo kimafunzo na kifedha, ili itekeleze wajibu wake.
 
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
5,147
Likes
5,577
Points
280
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
5,147 5,577 280
Tunataka kuona mafisadi kweli wanapelekwa huko, mafisadi katika nchi wanajulikana sitegemei kuona mnapeleka vibaka huko, na lazima kuwe na tafsiri sasa ya ufisadi na fisadi na lazima wananchi waelezwe tofauti ya fisadi na kibaka ili tujiridhishe kweli mnaowapeleka ni mafisadi..

Tunahitaji pia kuona hiyo mahakama inaanza haraka na kutoa hukumu haraka bila kusubiri wakati wa kampeni na kuwatoa watu muhanga ili kura zitoshe tena.
 
B

babtut

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2015
Messages
1,100
Likes
696
Points
280
B

babtut

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2015
1,100 696 280
Kuna watu watapotea hapa si mchezo.
Hao majaji wakae chonjo, kesi za hela mingi nazijua shida yake
 
T

TUNDE

Senior Member
Joined
Apr 23, 2016
Messages
127
Likes
77
Points
45
T

TUNDE

Senior Member
Joined Apr 23, 2016
127 77 45
Wananchi tunasubiri kwa hamu kubwa mahakama hii ya mafisadi kwa sababu kuna baadhi ya watendaji wasio waaminifu waliifanya nchi ya Tanzania kama shamba la Bibi. Mfano hai ni Chuo cha Ufundi Arusha
 
K

kindafu

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
1,142
Likes
943
Points
280
K

kindafu

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
1,142 943 280
lowasa na genge lake tumbo joto.
Kwa taarifa yako, hata kama kweli Lowassa ni fisadi, kumbuka kuwa alifanya ufisadi huo akiwa ccm na hivyo washirika wake wako humo humo ccm! Ni wachache sana walikuwa na ujasiri wa kuvuka mto pamoja naye, hivyo mtakapoanza naye jiandaeni pia kuangukiwa na nyumba yenu wenyewe! Hakuna fisadi aliye mtu mmoja, daima ana washirika ktk ngazi mbali mbali! Ni swala la muda tu!
 
sir longo

sir longo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Messages
1,025
Likes
472
Points
180
Age
30
sir longo

sir longo

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2014
1,025 472 180
Kwa taarifa yako, hata kama kweli Lowassa ni fisadi, kumbuka kuwa alifanya ufisadi huo akiwa ccm na hivyo washirika wake wako humo humo ccm! Ni wachache sana walikuwa na ujasiri wa kuvuka mto pamoja naye, hivyo mtakapoanza naye jiandaeni pia kuangukiwa na nyumba yenu wenyewe! Hakuna fisadi aliye mtu mmoja, daima ana washirika ktk ngazi mbali mbali! Ni swala la muda tu!
mm sipo kichama, kama kuna watu alishirikiana nao (lazima wapo), itawahusu pia
 
M

MSHAURI_WA_NCHI

Senior Member
Joined
Nov 10, 2015
Messages
139
Likes
68
Points
45
Age
48
M

MSHAURI_WA_NCHI

Senior Member
Joined Nov 10, 2015
139 68 45
Sina hofu wataanza na waliolifikisha taifa hapa tulipo. Tunawajue na wamekuwa wakilifarakanisha taifa kwa wizi mkubwa was fedha za umma na kulazimisha madaraka kwa kununua watu. Tuanze nao bila aibu na wafungwe na Mali zao zibinafshwe ikiwemo majumba waliyionunua ulaya kwa Mali za wanyonge.
 
B

Bekabundime

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Messages
1,698
Likes
1,234
Points
280
B

Bekabundime

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2014
1,698 1,234 280
lowasa na genge lake tumbo joto.
ndoto za vijiweni hizo kama lowasa ni fisadi siku nyingi angekuwa mahakamani,lkn tauchachoona ni stori za kumfunga paka kengele
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,715
Likes
49,556
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,715 49,556 280
Mkuu nimeipenda hii ya kutoa ufafanuzi naomba huu uwe mfano kwa taasisi zingine kuwa na tabia ya kujibu tuhuma kwa wakati, mkuu tunaomba muwe mnatuwekea na tarehe ya barua
 

Forum statistics

Threads 1,235,533
Members 474,641
Posts 29,225,795