Bunge lapitisha sheria kupigwa faini ya milioni 1 kwa watakaotupa taka hovyo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka 2017, ambapo pamoja na mambo mengine umeweka adhabu ya kulipa faini ya Sh 200,000 hadi Sh 1,000,000 au kifungo cha mwaka mmoja hadi miwili jela, kwa kosa la kutupa taka ovyo.

Kabla ya muswada huo, faini ya kosa hilo ilikuwa Sh 50,000 na kifungo kisichozidi miezi 12.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia, amepinga Serikali kuongeza ushuru kwenye vinywaji baridi, huku kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ikipinga faini za magari barabarani kufanywa sehemu ya mapato ya Serikali.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni jana baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kusoma Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2017, Ghasia alisema kamati yake inaitaka Serikali iangalie upya tozo 14 zilizobakia katika shule binafsi ili nazo ziondolewe kwa lengo la kupunguza gharama uendeshaji kwa shule hizo.

Wakati Ghasia akisema hayo, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha, David Silinde, alisema Serikali inatakiwa kuacha tabia ya kugeuza makosa ya barabarani kuwa sehemu ya chanzo cha mapato yake.

Badala yake, alitaka elimu itolewe kwa watumiaji wa vyombo vya moto barabarani ili kupunguza idadi ya makosa hayo.

“Kuna taarifa zisizo rasmi, kuwa maofisa usalama barabarani wamekuwa wakipangiwa idadi ya magari wanayotakiwa kuyakamata kwa ajili ya kukusanya fedha.

“Kutokana na taarifa hizo, askari wa usalama barabarani wamekuwa kero kwa watu kwa sababu wamekuwa wakiwabambikia makosa waendesha vifaa vya moto na kuwafanya waone ni kero kutumia vyombo hivyo,” alisema Silinde.

Katika hatua nyingine, Silinde alisema Serikali ya CCM imekuwa ya kibaguzi na inaonyesha nia mbaya kwa vyama vya upinzani ingawa vimesajiliwa kisheria.

Naye Waziri Mpango, alisema Muswada wa Fedha wa mwaka 2017, umelenga kuzifanyia marekebisho sheria 15 zinazohusu masuala ya fedha, kodi, ushuru, tozo na mawasiliano.

“Marekebisho hayo, yatafanyika kwa lengo la kuweka, kurekebisha, kupunguza au kufuta viwango vya kodi, ushuru, ada na tozo mbalimbali na kuboresha ukusanyaji wa kodi.

“Sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Benki Kuu, sura ya 197 ambapo tunataka kuweka sharti la ulazima kwa taasisi za Serikali kufungua akaunti na kuhifadhi mapato na fedha zake Benki Kuu.

“Nyingine ni Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, sura ya 306 ambapo tunalenga kupanua wigo wa mauzo ya hisa za asilimia 25 zitakazouzwa na kampuni ya mawasiliano kwenye soko la hisa kwa kutoa fursa kwa Watanzania, au taasisi yoyote ya kitanzania.

“Fursa hiyo pia itawahusu Watanzania wanaoishi nje ya nchi, kampuni zinazomilikiwa kwa pamoja baina ya Watanzania na raia wa nje, raia na kampuni ama taasisi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au raia na makampuni kutoka nchi nyingine.

“Kuondoa sharti la kuuza hisa katika soko la hisa kwa kampuni ndogo za mawasiliano zenye leseni na kubaki na kampuni kubwa zenye leseni ya mtandao au huduma.

“Lengo jingine ni kuwezesha mamlaka ya masoko ya dhamana baada ya kushauriana na waziri mwenye dhamana na masuala ya masoko ya dhamana, kutoa maelekezo ya namna kampuni iliyoundwa kufikia mauzo ya hisa asilimia 25 itakavyoweza kufikia mauzo ya kiwango husika kwa kadri hali ya soko itakavyoruhusu,” alisema Dk. Mpango.

Akizungumzia marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, sura ya 147, alisema kwa kuzingatia mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi wa viwanda, kiwango cha ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini kimepunguzwa au kubakia ilivyo sasa.

Naye Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alitaka Serikali iweke nguvu zaidi ya kukusanya kodi kwenye michezo ya kubahatisha na kuipeleka kwenye mazingira.

Aliendekeza pia tozo hiyo iongezwe kutoka asilimia sita hadi 12 kwa mapato yatokanayo na michezo hiyo na pia Serikali iongeze tozo hiyo kwenye leseni katika michezo hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema), aliiomba Serikali iondoe Sh 40 kwenye mafuta ya taa kwani kiasi hicho kitaongeza mzigo kwa Watanzania wengi wasio na nishati ya umeme.

Mbunge huyo pia aliitaka Serikali kututumia suala hilo kama njia ya udhibiti na kutaka mfumo ya wa uchakachuaji wa mafuta uimarishwe.

Chanzo: Mtanzania
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,482
2,000
Yaani kosa la kutupa taka ovyo faini ndo iwe one million..? Halafu nilidhani suala hili la usafi liko ndani ya majiji, manispaa na halmashauri..
 

Mkwere Sumbawanga

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
684
1,000
Jambo jema ili tuwe na mazingira safi ila faini ingekuwa angalau laki tano inatosha, pia wakamataji wa wanaotupa taka ovyo wasipopenda rushwa ni mtaji mzuri wa kipato kwa serikali hii faini
 

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
Nimecheka sana km mazuri.
Teh teh teh teh mbavu zinauma kwa kicheko.
Ndiyo nimeamini hawa wanajua kusoma na kuandika. Kwa akili zao wanafikiri kila mtu anauwezo wa kutoa 1 m? Hii nchi imefirisika. Baada ya kuona rambi rambi siku hizi hazipo wamekuja na hii.
Wajenge magereza mengi.
Teh teh teh Aliyependekeza anatoka chama cha makanikia?
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,387
2,000
Nimecheka sana km mazuri.
Teh teh teh teh mbavu zinauma kwa kicheko.
Ndiyo nimeamini hawa wanajua kusoma na kuandika. Kwa akili zao wanafikiri kila mtu anauwezo wa kutoa 1 m? Hii nchi imefirisika. Baada ya kuona rambi rambi siku hizi hazipo wamekuja na hii.
Wajenge magereza mengi.
Teh teh teh Aliyependeza anatoka chama cha makanikia?
Wale wale Chama cha Ndiyoooooooo.Tuna shida sana
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,481
2,000
Kwani bado tuna bunge? Kila kitu kinaamuliwa na mtu mmoja tu ambaye wakati wengine wakikatazwa kuandamana yeye anaruhusu maandamano ya kumpongeza yeye kila kona ya nchi. Huu ni uonezi wa hali ya juu. Mwezi huu tunapoelekea kufunga mwaka utashangaa kila mkuu wa mkoa au wilaya akitangaza maandamano ya kumpongeza mzee. Tumeona pwani, tutaona na kwingine. Just a matter of time. Kila mkuu wa sehemu fulani atataka amalize mwaka wa fedha wa serikali kwa pongezi kwa mzee na pongezi hizo usishangae zikaambatana na maandamano ambayo wengine wamekatazwa. A country of one man show.
 

God Heals

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
687
1,000
Hiyo faini ya kutupa taka ni kubwa sana. Ila kwa kuwa "wengi" ni kujua kusoma na kuandika tu wacha watukomeshe watu wa mwisho.

Mimi ningewaelewa endapo hizo faini wangeziadhibu kwa watu/washirika/kampuni zinazochukua kandarasi za kuzoa hizi taka kwanza. Maana madudu wanayotufanyia huku mitaani, Mungu ndiye anajua.
 

sambeke

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
685
1,000
Nimecheka sana km mazuri.
Teh teh teh teh mbavu zinauma kwa kicheko.
Ndiyo nimeamini hawa wanajua kusoma na kuandika. Kwa akili zao wanafikiri kila mtu anauwezo wa kutoa 1 m? Hii nchi imefirisika. Baada ya kuona rambi rambi siku hizi hazipo wamekuja na hii.
Wajenge magereza mengi.
Teh teh teh Aliyependeza anatoka chama cha makanikia?
Sasa unacheka nini ikifika wakati wa kura mnajidai mko busy na ajira uchwara, eti hamuwezi kupigwa jua vumilieni mpaka 2025
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,882
2,000
wazo ni zuri ila ilibidi serikali na halmashauri zake zifanye home work yao,maeneo yawe safi,mapipa ya kutupa taka yawepo na alama za kuyatambua ziwepo ili kuzuia watakaosema hatukuyaona,vyoo vijengwe na vihudumiwe angalia pale kariakoo kuna public toilets wapi?,again hii ni mihemko.
 

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
Sasa unacheka nini ikifika wakati wa kura mnajidai mko busy na ajira uchwara, eti hamuwezi kupigwa jua vumilieni mpaka 2025
Nacheka kwa sbb ya faini ya milion 1. Kwa akili yako fupi unafikiri watafunga wangapi?
Ukiangalia watu weng wanaishi kwa dola 1. Huyu mama ntilie atatoa hiyo hela? Waweke mapipa meng ya kutupa uchafu na elimu itolewe.
Kwa akili yako ya funza, unafikiri hii adhabu ipo sawa?
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,349
2,000
Hii ndio tatizo la kuamini utupaji ovyo wa takataka unafanywa makusudi kumbe jamii haijajengwa tangu utotoni kuhusu issue ya utupaji taka ovyo.....kwanza watumbie kwa hiyo sheria ya faini 50,000 ni wangapi wamelipa ama hali ya utekelezaji ukoje then mpaka wakapandisha (ninamaanisha kama watu walikuwa wakikamatwa tu wanalipa akimatwa analipa, nadhani ndio tutapata sababu ya kusema wananchi wameidharau faini ya 50,000 kwa kuiona ndogo na ndio maana serikali imeamua kupandisha)

Kwa uzoefu tu hiyo faini iliyokuwepo haitekelezwi kwa vitendo japokuwa ni kweli watu wanafanya makosa sasa sijui hiyo 1 million itakuaje zaidi ya kubakia kwenye makaratasi.

Maoni yangu:
Kabla ya kuweka faini kubwa ilitakiwa manispaa husika kuweka sehemu za kutupia taka na sio zile container peke yake tu bali hata huku majumbani watu watenganishe taka na watoa huduma waweze kupita mpaka mtaani yaani kuanzisha vikundi vidogo vidogo ambavyo vitakuwa na jukumu la kukusanya taka majumbani na wananchi wanachangia japo hata kama buku kwa wiki na kikundi kinapeleka kwenye container za kutupia uchafu then manispaa inabeba inapeleka kutupa sehemu inapohusika. (hii inaondoa ile tabia ya watu kujilipua kwa kutupa mtoni na sehemu zingine lakini kama tukiendelea na utaratibu huu wa container ya kutupia uchafu lipo umbali wa kutembea dakika kadhaa kama ilivyo sasa tutegemee hii hali kutokuachwa)
 

Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
1,137
2,000
Serikali pia inapaswa kuangalia ni vitu gani vinasababisha uchafuaji mkubwa wa mazingira, ili vipigwe marufuku ili binaadamu asionekane kama ni sababu kuu. Nadhani ni wakati muafaka sasa vifungashio kama mifuko ya Plastiki kupigwa marufuku kwa kuzingatia ni moja ya sababu kuu ya uchafu kwenye mazingira yetu. It is time now to say no to Plastiki bags.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom