Bunge lapitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 3 wa 2019

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,686
3,992
Siku ya Jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya majadiliano lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Namba 3) wa 2019.

Muswada huu unacover sheria takribani 8 ikiwemo Sheria ya Asasi za Kiraia, Makampuni na Vyama vya Kijamii. Katika kupita huko, Serikali imekubali kufanya marekebisho kadhaa kwenye Muswada

1. Kuweka utaratibu wa kujisajili kwa Makampuni na Asasi za Kiraia zitakazoshindwa kuhamisha usajili kutoka Kuwa Makampuni yenye hisa au Makampuni ya dhamana kwenda Asasi za Kiraia ndani ya miezi miwili iliyotolewa na Sheria.

2. Kufanya mabadiliko kuruhusu Taasisi za Imani/Za kueneza Imani kuendelea kusajiliwa na kuratibiwa na Sheria ya Vyama vya Kijamii

3. Kufanyia mabadiliko kifungu namba 25 cha Sheria ya Asasi za Kiraia ambayo inafafanua maana ya Asasi ya Kiraia ili kukidhi wigo wa Asasi zilizopo.

4. Kifungu namba 26 kinachompa Msajili wa Asasi za Kiraia nguvu ya kusitisha shughuli za Asasi ya Kiraia ikiwa inasubiri uamuzi wa Bodi ya Asasi, Kufanyia tathmini Asasi kila robo ya mwaka

5. Kifungu namba 27 ambacho kinampa nguvu Msajili kufanya upelelezi akitumia vyombo vya dola

6. Kifungu namba 28 ambacho kinazungumzia kufutiwa usajili kwa Asasi zitakazoshindwa kutimiza matakwa ya kisheria baada ya miezi miwili.

Ikiwa haya yamesemwa, bado haiko wazi ni mapendekezo yapi ya Wadau wa Asasi za Kiraia yamezingatiwa katika kufanya mabadiliko tajwa.

========

Katika Mjadala husika, Wabunge wa CCM kama ilivyo ada walikuwa wakiunga mkono hoja kwa kuzunguka huku na kule.

Wabunge waliochallenge Muswada ni Salome Makamba aliyetoa analysis rasmi ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Ally Saleh na Zitto Kabwe.

Salome Makamba

Kumekuwa na desturi ya bunge letu kutunga sheria zisizotekelezeka na hivyo kurudishwa bungeni katika kipindi kifupi ili kufanyiwa marekebisho, kambi rasmi ya upinzani inatasfiri desturi hiyo kama ni udhalilishaji wa bunge na wabunge

Wadau kadhaa walitoa wito kwa muswada huu kusogezwa mbele sababu hawakuona hata sheria moja iliyokuwa ikihitaji uharaka wa kufanyiwa marekebisho na badala yake uletwe kikao kinachofuata lakini serikali ilitia pamba masikioni.

Vifungu vinavyopendekezwa kurekebishwa katika sheria hii sio tu vinaleta mkanganyiko katika utendaji wa kazi bali vimeletwa kudhibiti sekta binafsi katika kuleta maendeleo. Bunge likipitisha mapendekezo haya ni hatari sana kwa mustakabali wa CSOs na taifa letu, nawaunga mkono wadau kuwa mapendezo haya yasitishwe na utafiti wa kina ufanyike

Kambi rasmi ya upinzani bungeni inalishauri Bunge lako tukufu kutoa muda wa kutosha wa kuchambua miswada na kushirikisha wadau ili kuepuka kutunga sheria zisizotekelezeka lakini pia kuepusha dhana ya nia ovu ambayo imekuwa ikitafsiriwa na wengi

Mapendekezo haya yana sheria nyingi zinazogusa jamii yetu moja kwa moja. Asasi za kiraia zinatoa mchango mkubwa kuisaidia serikali katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi na kujitathmini katika utendaji wake wa kila siku

Ally Saleh, Mbunge wa Malindi, CUF

Sikubaliani na wanaosema hakuna madhara ya Muswada kuletwa kwa hati ya dharura. Madhara yapo kwa sababu hatukupata muda wa umakini wa kuupitia Muswada

Hata msemaji wa mwisho aliuliza kwanini kwenye Sheria ya Uwakala wa Meli huwezi kupata leseni ukiwa mmiliki lakini bahati mbaya wadau wa eneo hili hatukuwapata. Wanaosema kanuni inasema hata bila wadau tunaweza kuendelea madhara yake ndo haya

Dharura hii najua imekuja kwa sababu IMF na World Bank walikuja kuchangia Muswada wa Takwimu. Mwanasheria Mkuu aliieleza kamati kuwa ilibidi wawithdraw na kuiandika upya Sheria baada ya kuwasikiliza, tulikuwa tumekwama. Sasa angalau imekuja 'a better version'

Zitto Kabwe

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Kabwe amesema Serikali ya Tanzania imewasikiliza Benki ya Dunia (WB) kwa kuleta marekebisho ya Sheria ya Takwimu baada ya kuzuia Dola za Marekani bilioni 1.15.

Zitto ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 27, 2019 wakati akichangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 3 wa mwaka 2019. Amesema kwa mara nyingine katika Bunge hilo la Tanzania imepelekwa sheria ambayo inakwenda kuminya uhuru wa Watanzania.

Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo, amesema walianza na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya vikokotoo vya pesheni na haki za wafanyakazi . “Huu ni mwendelezo wa sheria wa kukandamiza Watanzania. Ni bahati mbaya kuwa wananchi walio wengi ni masikini sana wakizungumza na hata wabunge wao wakizungumza hayasikilizwi,” amesema.

Amesema walizungumza kuhusu kifungu 24 A na B cha Sheria ya Takwimu kuwa kinaleta matatizo makubwa ya kunyima haki za watu lakini hawakusikilizwa. Hata hivyo, amesema juzi Benki ya Dunia ilizuia fedha Dola za Marekani bilioni 1.15 wamesikilizwa.

Zitto alisema Serikali ya awamu ya tano imekubali jambo ambalo wananchi na wapinzani walilipigia kelele lakini hawakusikilizwa. Amesema sheria hiyo imebadilishwa leo hata mwaka haijatimiza na kwamba watu wale wale wanasimama na kuiambia Serikali kuwa ni sikivu.

Wala tusihangaike na Takwimu nina barua kutoka Ikulu na Wizara ya Fedha kumuomba Rais aruhusu kabla ya mkutano huu wa Bunge Sheria ya Takwimu irekebishwe na mmetii mmeileta imerekebishwa, mnawasikiliza zaidi mabeberu kuliko wananchi wenu walioikataa sheria hii

Aidha, amesema Serikali ya Tanzania inafanya marekebisho Sheria ya Makampuni ikiwemo kukifanyia marekebisho tafsiri ya neno kampuni. Amesema nchi zote za Jumuiya ya Madola zinatafsiri moja ya neno kampuni. “Inaenda kuunganisha kampuni na mwenye kampuni kuwa kitu kimoja, jambo ambalo tutachekwa duniani na hakuna mtu atakayekuja nchi hii kuwekeza fedha zake ili kutengeneza ajira, ili kulipa kodi,” amesema.

Amesema yeye anafahamu marekebisho hayo yameletwa kwa sababu Serikali inahangaika na Kampuni ya Acacia. Ameitaka Serikali kwenda kupambana na kampuni hiyo kwa utaratibu wa kiutawala badala ya kuharibu nchi kwa ugomvi wa kampuni moja.

“Kwanini mnatutia aibu duniani kwa kuleta sheria za ovyoovyo namna hii, kwa nini halafu mnampa wizara kijana smart inno kwenda kuhangaika na mambo ya kijinga kijinga kama haya,” amesema.
 
Mbona naona Kifungu namba 26, 27 na 28 vina contradict? Inawezekana vipi, umkamate, ufanye upelelezi na utoe hukumu wewe mwenyewe? Je kwanini hawa waheshimiwa upeo wao wa kufikiria umepungua ama una udhaifu namna hiyo? Hizi sheria hawa watu wanazitunga wakiwa wanatoka usingizini ama wana hangover? Ni aibu sana kwa kweli.

Je kama katika sheria zetu za nchi tungewaachia Polisi, kukamata, Kushitaki na kutoa hukumu wao wenyewe je nchi hii ingekuwa wapi na wananchi wangapi wangekosa haki yao kwa sababu ya upungufu huu? Kwa marekebisho haya ya sheria hiyo hayaleti tija ama maana yoyote ile na hata ukienda mahakamani unapata ushindi wa bure kabisa.
 
Kwenye kupitisha miswaada na sheria mbalimbali ni bora ungewekwa utaratibu wa wabunge kupiga kura kuliko huu utaratibu ulipo sasa.

Kwa maana hiyo kura zingeamua mswaada fulani upitishwe ama la! kwa kuangali idadi ya wabunge na idadi ya kura.

Huu utaratibu uliopo sasa wa kuitikia 'Ndio' kisha spika anasema "waliosema ndio wameshinda umekaa kikandamizaji na wakizamani sana.
 
Kwahiyo mnatunga sheria inayo inyanganya mahakama mamlaka yake kikatiba?
Ngoja nimsubiri Omundi
 
kumbe sheria ya twakimu baada ya tunaowaita mabeberu wa WB NA IMF kuhamrisha ifanyiwe marekebisho hatimae serikali imekubari kufanya marekebisho, au Zitto sijamuelewa,
Hapo ndo utagundua kwanini? jiwe anamwita KABUDI ni WAPUMBUVUU na bado kabudi anashangilia ki zuzuu.

Wabunge walipiga kelekelee sana juu ya hiyo sheria ya takwimu ila kwa uzuzu wa KABUDI akatia pamba masikioni, wanao itwa MABEBERU wamewabana panapo uma sasa wamebarisha.

CCM ni mumiani wa TANZANIA. Yaleyalee magonga meza yaliyokua yanashangilia upitishaji wa sheria hii ndo haohao leo hii wanafanya marekebisho yake.

Natamani ifikie hatua ya jiwe kuanza kuwazabua MAKOFI hadharani mawaziri wake, maanaaa ukondoo umewazidi
 
Huu utaratibu wa kugombana na mtu mmoja unakwenda kutunga sheria ya kuumiza watu milioni 55 kiukweli utaligharimu taifa,nadhani ifike wakati tuache hizi mambo za kukomoana,huwezi kukosana na acacia ukaenda kutunga sheria za kumuathiri IPP ,kiukweli sio fair mkumbuke haya mnayoyafanya historia inayaandika.
 
Kwaio serikali inataka kuleta kichekesho cha dunia nzima wazungu waliona waitofautishe Sole Proproprietorship na Company maana Company ni mtu tofauti sasa hivi inamaana Soleproprietor na mwenye kampuni ni kitu kimoja
 
Mbona naona Kifungu namba 26, 27 na 28 vina contradict? Inawezekana vipi, umkamate, ufanye upelelezi na utoe hukumu wewe mwenyewe? Je kwanini hawa waheshimiwa upeo wao wa kufikiria umepungua ama una udhaifu namna hiyo? Hizi sheria hawa watu wanazitunga wakiwa wanatoka usingizini ama wana hangover? Ni aibu sana kwa kweli.

Je kama katika sheria zetu za nchi tungewaachia Polisi, kukamata, Kushitaki na kutoa hukumu wao wenyewe je nchi hii ingekuwa wapi na wananchi wangapi wangekosa haki yao kwa sababu ya upungufu huu? Kwa marekebisho haya ya sheria hiyo hayaleti tija ama maana yoyote ile na hata ukienda mahakamani unapata ushindi wa bure kabisa.
Ndiyo madhara ya dharura
 
Hapo ndo utagundua kwanini? jiwe anamwita KABUDI ni WAPUMBUVUU na bado kabudi anashangilia ki zuzuu.

Wabunge walipiga kelekelee sana juu ya hiyo sheria ya takwimu ila kwa uzuzu wa KABUDI akatia pamba masikioni, wanao itwa MABEBERU wamewabana panapo uma sasa wamebarisha.

CCM ni mumiani wa TANZANIA. Yaleyalee magonga meza yaliyokua yanashangilia upitishaji wa sheria hii ndo haohao leo hii wanafanya marekebisho yake.

Natamani ifikie hatua ya jiwe kuanza kuwazabua MAKOFI hadharani mawaziri wake, maanaaa ukondoo umewazidi

Unaweza kuwa sahihi kwa Maoni yako Mkuu lakini nyuma ya Pazia Mzee Jiwe anaweza kuwa mkorofi na hasikilizi au kuufanyia kazi Ushauri anao pewa.Na unakumbuka ile kauli yake ya kutotaka kupangiwa na Mtu.

Njaa pia ni tatizo linalo ondoa Msimamo na Akili za Mtu mbele ya anae mrushia Mnofu ,hasa ukizingatia aina ya Wananchi/Watawala tulio nao katika Nchi yetu.
 
Hapo ndo utagundua kwanini? jiwe anamwita KABUDI ni WAPUMBUVUU na bado kabudi anashangilia ki zuzuu.

Wabunge walipiga kelekelee sana juu ya hiyo sheria ya takwimu ila kwa uzuzu wa KABUDI akatia pamba masikioni, wanao itwa MABEBERU wamewabana panapo uma sasa wamebarisha.

CCM ni mumiani wa TANZANIA. Yaleyalee magonga meza yaliyokua yanashangilia upitishaji wa sheria hii ndo haohao leo hii wanafanya marekebisho yake.

Natamani ifikie hatua ya jiwe kuanza kuwazabua MAKOFI hadharani mawaziri wake, maanaaa ukondoo umewazidi
Washauri wapumbavu na rais alishalisema hili wazi wazi na wao wakakenua meno tu kama mazuzu.
 
Bunge KINYAA, Bunge DHAIFU linafanya kazi zake si kwa maslahi ya Watanzania bali genge la wahuni, majizi, mafisadi na WAUAJI linaloongozwa na kubwa la majizi, nduli, dikteta, fisadi, muongo, mtekaji, mtesaji na MUUAJI wa IKULU.

Siku ya Jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya majadiliano lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Namba 3) wa 2019.

Muswada huu unacover sheria takribani 8 ikiwemo Sheria ya Asasi za Kiraia, Makampuni na Vyama vya Kijamii. Katika kupita huko, Serikali imekubali kufanya marekebisho kadhaa kwenye Muswada

1. Kuweka utaratibu wa kujisajili kwa Makampuni na Asasi za Kiraia zitakazoshindwa kuhamisha usajili kutoka Kuwa Makampuni yenye hisa au Makampuni ya dhamana kwenda Asasi za Kiraia ndani ya miezi miwili iliyotolewa na Sheria.

2. Kufanya mabadiliko kuruhusu Taasisi za Imani/Za kueneza Imani kuendelea kusajiliwa na kuratibiwa na Sheria ya Vyama vya Kijamii

3. Kufanyia mabadiliko kifungu namba 25 cha Sheria ya Asasi za Kiraia ambayo inafafanua maana ya Asasi ya Kiraia ili kukidhi wigo wa Asasi zilizopo.

4. Kifungu namba 26 kinachompa Msajili wa Asasi za Kiraia nguvu ya kusitisha shughuli za Asasi ya Kiraia ikiwa inasubiri uamuzi wa Bodi ya Asasi, Kufanyia tathmini Asasi kila robo ya mwaka

5. Kifungu namba 27 ambacho kinampa nguvu Msajili kufanya upelelezi akitumia vyombo vya dola

6. Kifungu namba 28 ambacho kinazungumzia kufutiwa usajili kwa Asasi zitakazoshindwa kutimiza matakwa ya kisheria baada ya miezi miwili.

Ikiwa haya yamesemwa, bado haiko wazi ni mapendekezo yapi ya Wadau wa Asasi za Kiraia yamezingatiwa katika kufanya mabadiliko tajwa.

========

Katika Mjadala husika, Wabunge wa CCM kama ilivyo ada walikuwa wakiunga mkono hoja kwa kuzunguka huku na kule.

Wabunge waliochallenge Muswada ni Salome Makamba aliyetoa analysis rasmi ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Ally Saleh na Zitto Kabwe.

Salome Makamba

Kumekuwa na desturi ya bunge letu kutunga sheria zisizotekelezeka na hivyo kurudishwa bungeni katika kipindi kifupi ili kufanyiwa marekebisho, kambi rasmi ya upinzani inatasfiri desturi hiyo kama ni udhalilishaji wa bunge na wabunge

Wadau kadhaa walitoa wito kwa muswada huu kusogezwa mbele sababu hawakuona hata sheria moja iliyokuwa ikihitaji uharaka wa kufanyiwa marekebisho na badala yake uletwe kikao kinachofuata lakini serikali ilitia pamba masikioni.

Vifungu vinavyopendekezwa kurekebishwa katika sheria hii sio tu vinaleta mkanganyiko katika utendaji wa kazi bali vimeletwa kudhibiti sekta binafsi katika kuleta maendeleo. Bunge likipitisha mapendekezo haya ni hatari sana kwa mustakabali wa CSOs na taifa letu, nawaunga mkono wadau kuwa mapendezo haya yasitishwe na utafiti wa kina ufanyike

Kambi rasmi ya upinzani bungeni inalishauri Bunge lako tukufu kutoa muda wa kutosha wa kuchambua miswada na kushirikisha wadau ili kuepuka kutunga sheria zisizotekelezeka lakini pia kuepusha dhana ya nia ovu ambayo imekuwa ikitafsiriwa na wengi

Mapendekezo haya yana sheria nyingi zinazogusa jamii yetu moja kwa moja. Asasi za kiraia zinatoa mchango mkubwa kuisaidia serikali katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi na kujitathmini katika utendaji wake wa kila siku

Ally Saleh, Mbunge wa Malindi, CUF

Sikubaliani na wanaosema hakuna madhara ya Muswada kuletwa kwa hati ya dharura. Madhara yapo kwa sababu hatukupata muda wa umakini wa kuupitia Muswada

Hata msemaji wa mwisho aliuliza kwanini kwenye Sheria ya Uwakala wa Meli huwezi kupata leseni ukiwa mmiliki lakini bahati mbaya wadau wa eneo hili hatukuwapata. Wanaosema kanuni inasema hata bila wadau tunaweza kuendelea madhara yake ndo haya

Dharura hii najua imekuja kwa sababu IMF na World Bank walikuja kuchangia Muswada wa Takwimu. Mwanasheria Mkuu aliieleza kamati kuwa ilibidi wawithdraw na kuiandika upya Sheria baada ya kuwasikiliza, tulikuwa tumekwama. Sasa angalau imekuja 'a better version'

Zitto Kabwe

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Kabwe amesema Serikali ya Tanzania imewasikiliza Benki ya Dunia (WB) kwa kuleta marekebisho ya Sheria ya Takwimu baada ya kuzuia Dola za Marekani bilioni 1.15.

Zitto ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 27, 2019 wakati akichangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 3 wa mwaka 2019. Amesema kwa mara nyingine katika Bunge hilo la Tanzania imepelekwa sheria ambayo inakwenda kuminya uhuru wa Watanzania.

Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo, amesema walianza na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya vikokotoo vya pesheni na haki za wafanyakazi . “Huu ni mwendelezo wa sheria wa kukandamiza Watanzania. Ni bahati mbaya kuwa wananchi walio wengi ni masikini sana wakizungumza na hata wabunge wao wakizungumza hayasikilizwi,” amesema.

Amesema walizungumza kuhusu kifungu 24 A na B cha Sheria ya Takwimu kuwa kinaleta matatizo makubwa ya kunyima haki za watu lakini hawakusikilizwa. Hata hivyo, amesema juzi Benki ya Dunia ilizuia fedha Dola za Marekani bilioni 1.15 wamesikilizwa.

Zitto alisema Serikali ya awamu ya tano imekubali jambo ambalo wananchi na wapinzani walilipigia kelele lakini hawakusikilizwa. Amesema sheria hiyo imebadilishwa leo hata mwaka haijatimiza na kwamba watu wale wale wanasimama na kuiambia Serikali kuwa ni sikivu.

Wala tusihangaike na Takwimu nina barua kutoka Ikulu na Wizara ya Fedha kumuomba Rais aruhusu kabla ya mkutano huu wa Bunge Sheria ya Takwimu irekebishwe na mmetii mmeileta imerekebishwa, mnawasikiliza zaidi mabeberu kuliko wananchi wenu walioikataa sheria hii

Aidha, amesema Serikali ya Tanzania inafanya marekebisho Sheria ya Makampuni ikiwemo kukifanyia marekebisho tafsiri ya neno kampuni. Amesema nchi zote za Jumuiya ya Madola zinatafsiri moja ya neno kampuni. “Inaenda kuunganisha kampuni na mwenye kampuni kuwa kitu kimoja, jambo ambalo tutachekwa duniani na hakuna mtu atakayekuja nchi hii kuwekeza fedha zake ili kutengeneza ajira, ili kulipa kodi,” amesema.

Amesema yeye anafahamu marekebisho hayo yameletwa kwa sababu Serikali inahangaika na Kampuni ya Acacia. Ameitaka Serikali kwenda kupambana na kampuni hiyo kwa utaratibu wa kiutawala badala ya kuharibu nchi kwa ugomvi wa kampuni moja.

“Kwanini mnatutia aibu duniani kwa kuleta sheria za ovyoovyo namna hii, kwa nini halafu mnampa wizara kijana smart inno kwenda kuhangaika na mambo ya kijinga kijinga kama haya,” amesema.
 
Kwenye kupitisha miswaada na sheria mbalimbali ni bora ungewekwa utaratibu wa wabunge kupiga kura kuliko huu utaratibu ulipo sasa.

Kwa maana hiyo kura zingeamua mswaada fulani upitishwe ama la! kwa kuangali idadi ya wabunge na idadi ya kura.

Huu utaratibu uliopo sasa wa kuitikia 'Ndio' kisha spika anasema "waliosema ndio wameshinda umekaa kikandamizaji na wakizamani sana.
Hata wakipiga kura haisaidii! Wabunge wa ccm hawako huru bungeni na anaejaribu kwenda kinyume na msimamo huitwa na kuonywa. Ndio maana kamwe hutaona kura ya siri ikipigwa bungeni.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom